Mashabiki hata wale wasiompenda Floyd Mayweather wacharuka baada ya kushindanishwa na Terence Crawford

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,454
21,158
Ifike pahala huyu jamaa wamuache apumzike maana kwa mambo yanayoendelea sasa ni kumkosea adabu bondia bora wa muda wote na wa vizazi vyote Floyd Sinclair Joy Money Mayweather Junior .

Nimesikitishwa sana na baadhi ya watu kumlinganisha Floyd na Terence eti baadhi yao wana amini Terence angeweza kumkalisha Floyd kama wote wangekuwa kwenye Prime zao.

Wenyewe wanadai Crawford angeweza kumpiga Floyd kwenue version yake yoyote kuanzia anaitwa Pretty boy mpaka sasa Money May , kwa kweli bila kumung'unya maneno hizi ni dharau, furaha isizidi kipimo namna hiyo.

Uzuri nimefurahi kuona hata wale haters wa Floyd nao wamekataa ujinga huu, na kukiri hakuna uwezekano wowote wa Terence kumpiga Floyd na sio tu kwenye prime yake hata kwa Sasa Terence hana uwezo wa kumpiga Floyd.

Hilo pambano moja aliloshinda dhidi ya Errol Spence isiwe kigezo cha kumkosea adabu Floyd.

Screenshot_20230803-135331_1.jpg
 
Back
Top Bottom