Flaviana Matata: Wanasiasa Msitufanye Wapumbavu.

Feb 18, 2019
22
350
Mlimbwende na mwanamitindo mahiri wa kimataifa kutoka Tanzania Flaviana Matata, amewatolea uvivu wanasiasa ndumilakuwili ambao pindi wakiwa na madaraka hufanya maamuzi ambayo si sahihi au yasiyo na tija lakini pindi wanapoondoka madarakani wanayakana hayo maamuzi kwamba hayakuwa yao.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika yafuatayo; "Kuna wanasiasa wanatoa maamuzi wanajua kabisa yataumiza watu alafu wakishatumbuliwa ndo wanataka kutuaminisha wapo na sisi. Ebu mjifunze kutenda haki au kufanya maamuzi sahihi mkiwa mmekalia hivyo viti. We are not fools."

Baada ya saa moja akaongezea ujumbe wa kiingereza unaosema; “Super leaders are not just responsible for the words that comes out of their mouth, they take responsibility for how those words land as well”

Hii huenda imechagizwa na mawaziri watatu wa awamu ya tano ambao hivi karibuni walihojiwa na vyombo vya habari kwa nyakati tofauti na kukana kuhusika kwao moja kwa moja na baadhi ya sheria zilizotungwa pindi walipokuwa na madaraka.

Screenshot (7).png

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom