Flash Back Memories: Matukio ya Boarding School

....niliibiwa tranka zima baada ya kutoka likizo nikiwa na mazagazaga kibao tena kwa kuchelewa unakuta wenzako wote wapo juu ya mawe, jamaa wakachokonoa mpaka likafunguka then wakabeba mazaga yote, likizo iliyofuata sikubeba kitu zaidi ya hela tu, katika kulipiza kisasi nilihakikisha kila mtu nmemliza, hakuna tranka nililokuwa siwezi fungua, nlkuwa na funguo kama 30 hv kipindikile kufuli zote ni tri-circle
 
Ilikua kwenye Shule moja huko Moshi
Siku nimechelewa kuamka,kengele ya parade ikalia na mm sikuweza kufika kwa wakati na ukifika kwa kuchelewa ni fimbo za kutosha.

Sasa mimi nikaona njia itakayoniokoa ni kubaki bwenini tu. Sasa pa kujificha ni wapi? Basi,nikajitwika na kutaka kuingia darini! Nilianguka karibia nitenguke kiuno.

Kunyanyuka nikamuona mwalimu wa bweni anakuja. Huyu akikukamata ni hatari sana. Sasa shuleni huruhusiwi kufunga tranka,yote yanaachwa wazi! Nikafikiria fasta,nikachukua tranka moja kubwa na kumwaga vitu Kitandani.
Kisha mwanaume nikajitwika ndani. Nilikua mdogo na nilitoshea. Tatizo hewa sasa,haikua ikitosha. Ticha akafika akaanza kukagua kuanzia uvunguni mpaka darini.

Alipomaliza,akakaa kitandani akaanza kufuta viatu vyake. Kumbe anakanyagia tranka ambalo nipo humo. Alikaa muda mrefu kidogo huku mwenyewe hewa imekua nzito mno na nahema kwa shida. Nikaona hapa Malaika mtoa roho ananichungulia. Nilichofanya nikamuinua mguu na kutoka,aisee alitoka kutoka mbio lakini aliponiona alicheka sana.
Akanipeleka staff,walimu wote walicheka sana mpaka wakashindwa kunichapa. Hahahaha!


KUTUMWA KUPELEKA BARUA KWA DEMU WA Braza.
Kama kawaida,kuwa na mahusiano ya kitoto shuleni. Braza akamuandikia demu barua lakini wanasoma madarasa tofauti. Lile jamaa likaniita likanambia peleka hii barua kwa demu wake. Mimi nikaichukua na kuanza kuipeleka. Ilikua ni usiku muda tunatoka prep. Kumfikishia demu nikamkabidhi alafu nikaanza kumpa maelekezo. Ticha wa zamu huyo katokea. Alinilabua kofi moja hilo sijapata kuliona dunia hii.

KUINGIZWA STAFF NA KUCHAPWA KAMA MBUZI.
Shule yetu ilikua ya Kanisa,kuna kipindi wale wenye mahusiano mnaitwa. Taarifa za uhusiano wenu wanazipata kutoka kwa MaSPY!
Basi,siku hiyo unaitwa na kuambiwa una mahusiano na fulani kisha uwataje wengine ambao unawafahamu wana uhusiano.
Mkishawataja,mnaambiwa kumbatianeni. Kila mtu na mpenzi wake. Walimu wanakaa kila upande,mnachapwa balaa. Mwalimu anakuchapa popote isipokua kichwani. Acha kabisa aisee.
 
Kuna jamaa siku ya NECTA form 2 alitoboa akaja kulala saa 11 alfajiri, matokeo yake akaja kuamka saa 5 asubuhi baada ya kelele za tuliotoka kwenye pepa kuanza kusikika mitaa ya bwenini. hahahahaaaa
Kutoboa inabidi uwe na msuli hasa, kama huna, matokeo yake ndio kama hayo. Umenikumbusha classmate wangu mmoja, yeye alikua ana solve hesabu tu, na tukipiga pepa anapata C, anafeli masomo mengine yote lakini hesabu anapata C.
 
Nakumbuka ilikua Siku ya jpili nlikamatwa nimetoroka,yule ticha akanambia nirudi shule nikajiriport mwenyewe kwa rector(ile shule kosa la kutoroka ilikua ni kufukuzwa jumla)bas jtatu asubuhi akaniita ofsini akaniuliza kama nilijiriport,nikamwambia ndio rector amesema nijiandae nifunge mizigo yangu yote badae nikachukue clearance form niende nyumbani..sikua nmeenda kwa rector wala nini,basi yule ticha akaanza kujitete ooh mi skua serious,ooh tutakuwa tunawasiliana na misamaha kibao..nikamwambia poa bila ndo hivo ntpa shule nyingine tu..walimu wote ofsini walikua wananisikitikia,kimoyomoyo nlikua nawasikitikia wao zaidi.
 
Usela mzuri saaana huu
 
Bhuahahahahaha duh mkuu umenichekesha sanaa asee tupia na jina la iyo shule
 

Mkuu, Umenikumbusha longi Kinoma.
Life kama hili tuliliishi Tanga Technical School
 
Kudownoad Dawa ya mswaki
Kwamba Dawa ikiisha nachukua dawa ya mwezangu naminya inaingia kwenye tube ya Dawa yangu
 
Tulikuwa tunatoroka kwenda vijiji vya jirani kwenda kunywa pombe za kienyeji, tukikutana na mwalimu tunamnunulia pombe mpaka atosheke
Halafu kesho anakuchapa viboko, eti alikukuta unakunywa pombe!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hii itakua old moshi
 
kujificha ndani ya mitoma ili tuu usiende morning prepo SAA kumi na moja asubuh
 
Bhuahahahahaha dah nimecheka sanaaa asee uliamua kujificha kwenye tranka wew ni bonge la mjeda asee
 
Bhuahahahahaha dah nimecheka sanaaa asee uliamua kujificha kwenye tranka wew ni bonge la mjeda asee
N hatari Mkuu wangu,tcha anachapa viboko kama anakukata makalio. Alafu kulivyo baridi acha tu Mkuu wangu! Nilijitahidi sana,sema tcha aliendelea kukaa tu babake!
 
kutokana na chakula kibovu nilitumia sana chai na sana maandazi nikiyapaka blue band. Matokeo yake nikanenepa tofauti na mwanzo. Likizo niliporudi nyumbani mzee hakunielewa nilipomueleza HALI SHULENI MBAYA NA MATOKEO YAKE akapunguza zaidi pocket money akihisi nadanganya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…