Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 32,280
- 44,418
5 Inches Smartphone
@Chief Mkwa wa ninakunukuu "Yap dell huyu huyu dell strike ndo ilikua simu/tablet ya kwanza kua na nchi 5" Hii sio kweli wala sio sahihi. Smartphone yenye 5 Inches Screen ya kwanza sio Dell, HTC ndio waliokuwa wa kwanza kutoa simu yenye 5 inches Screen inaitwa HTC Advantage. Ilikuwa ina-run Windows Mobile 5, kabla ya iPhone na Android kutoka. Simu hii ilikuwa branded T Mobile Ameo na imetoka Machi 2007.
View attachment 85293
JBL Speaker
Huwezi kuwapa credit Nokia kwa kutoa accessory kwa ushirikiano na kampuni nyingine. Ukweli ni kwamba kama unataka kuzungumzia accessories basi iphone hawashikiki. Wana toys, wana vifaa vya matibabu, wana mpaka TV.
Wembamba na Uzito
Hapa nakubaliana na wewe 100% kwamba Nokia ni madhubuti, lakini tulipozungumzia wembamba na uzito (hasa wembamba) tulikuwa tunazuzungumzia form factor. Nokia Lumia 920 ni kijitofali fulani hivi.
Powerful Prosessors
Ukitaka kujua umuhimu wa processor ni kwamba developers wenye kutengeneza game zenye kuhitaji power na graphics hawatengenezi game za WP. Kwa upande wa iPhone utaona games zinakosa features fulani kwa sababu developers wanajua kuwa iPhones hazina powerful processor. Angalia experience ya game. Kama una access ya devices angalia Experience na feature za Riptide GP Kwenye iPhone au iPad halafu linganisha na Quadcore device yoyote kama vile Nexus 7 au Transformer Prime. Ndio utajua maana ya kuwa na powerful processor kwenye device. Vile vile Hivyo sleekness na ufasta wa Lumia 920 sio suala la hadnset yenyewe bali ni OS (WP 8) ambapo wanaostahiki credit ni Microsoft sio Nokia.
Maps
Uki-search kwenye Appstore neno "Maps" unapata hits 8,201 katika iPad na kwenye iPhone unapata Hits 17,120. Na uki-search kwenye Play Store (Android) unapata hits 30,664. Sasa sifahamu kwa nini unadhani kwamba Nokia maps ni advantage kwa simu hiyo. Pia nakuhakikishia ukitaka feature yoyote ambayo inapatikana kwenye maps basi ipo kwenye android na iOS, iwe turn by turn navigation, 3D maps, POIs, Traffic Info, Photo Nav, Coordinates n.k.
Wireless Charger
Kwanza Nokia sio wa kwanza kutoa device yenye wireless charger, the Dead "Palm Pre" ilikuwa na feature hii time back. Again hata kwa Lumia 920 hizi ni accessories tu ambazo kwa mfano iPhone tangu enzi za 3GS kulikuwa accesory inaitwa Power Mat na inafanya wireless charging. Hivyo kwa vile utahitaji kuinunua wireless charger (kwa vile haji na simu kwenye box) huwezi kuipa advantage simu yenyewe.
Nokia Market Share
Nilipozungumza kuwa Nokia kwa sasa wana poor performance nilikuwa namaanisha hivi
View attachment 85294
Nokia wana-play kwenye 6% ya Windows Phone (ambapo sio yao peke yao) na (6% ya others) ambapo pia sio yao peke yao. Nadhani utajua kama wanacheza. hata hivyo hili tulilizungumza kwa kirefu sana kwenye discussion nyingine nikakuonyesha kuwa Faida ya Nokia ni $ 1.024 bl, ambapo ni sawa na HTC, halafu ukizingatia kuwa Nokia Simu sio main business yao. Na Nokia inashika nafasi ya pili kwa mauzo kwa sababu ya kuuza vimeo vya £14 na simu kama Nokia Asha, lakini sales performance yao katika High End Phones ni kichekesho.
Camera
Kuhusu kamera; well I salute Lumia camera, lakini bado ni 8MP
Mwisho kabisa usidhani kama naandika haya kwa sababu mimi ni mtumiaji wa Android, binafsi ni mtumiaji wa iOS.
Sometime natamani kuwe na kitu kinaitwa yaliyomo yani mfano huu
-umuhimu wa wireless charge
-camera
-....
Sababu unaongea hichi then mtu anabend mada ili kuvutia upande wake
wewe umesema wireless charge haina umuhimu nikakupa umuhimu ushahama kwengine unakandia jbl power up rudi kwenye madaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
then pia
umeieka camera ya nokia inferior kwa megapixel ndogo sasa hivi umegeuka sikuelewi big up za nini na mwanza umekandia????
then it doesnt matter nani wa kwanza ila cha muhimu ni kwamba 5 inch ilikuwepo ila watu hawakuijali sababu tu katoa samsung faster imekua maarufu
processing power
developer wavivu always watataka power kubwa kutengeneza magemu mazuri na haina maana game zuri linahitaji processor na gpu kubwa bali ni visingizio tu. Then sometime pia ujue why utafute game zuriiiii la kucheza hata masaa manne mfululizo kwenye simu?? Utakua unafanya kazi kweli? Magame ya simu yanatakiwa yawe simple tu ili kupass time pale inapohitajika.
maps
mkuu hapa unahitaji lecture hebu niskilize vizuri. Duniani kuna kampuni 3 maarufu za ramani. (mpaka mwaka 2008). Zinaitwa
-navteq
-teleatlas (atlas zile ramani wengi tunazijua)
-tomtom
hizi kampuni tatu ndio zikawa zinasuply data kwa makampuni mengine ukaona vitu kama google map.
Mwaka 2008 nokia akainunua navteq(kampuni kubwa ya ramani). Aliinunua dola bilion 8 na upuuz (zaidi ya trilion 13 budget yetu ya kibongo)
google kuona vile akaona nokia atanipita sababu ni mpinzani wangu akaamua kuiacha navteq (baada ya kununua data nyingi) kuanzia mwaka 2008 google akaachana na kuchukua data za navteq.
Navteq sasa hivi ndo inajulikana kama nokia map. Yeye ni muuzaji data wa ramani. Na hawa ndio wateja wa nokia map
-asilimia 80 ya magari yote duniani yanatumia nokia map. (toyota, volkswagen............)
-makampuni kibao kama oracle na microsoft
so mkuu unapozungumzia navteq unazungumzia open source ya kulipia ya ramani hata wewe ukitaka unapewa data unatengeneza ramani zako zinaitwa millah map.
Hizo ramani unazoziona playstore na appstore nauhakika zaidi ya 50% zinatumia engine ya nokia map.
Usifkiri ni kitu cha mchezo kwa individual kutengeneza ramani, ramani sio game mkuu kua najua kucode basi ntangeneza inahitaji matrilion ya hela kuzunguka dunia nzima.
Thats why unaona nokia map itabaki nokia map the most accurate map in the world
nnachowapendea nokia technology wakiizindua sio siri wanaelezea kila kitu hebu angalia hapa mkuu ramani zinavyotengenezwa then nambie hao developer 10,000 wametengeneza hizo ramani?
Nokia, Navteq show us how a map is made - CNET Mobile