Flagship Mobile Phone 2013: Ni Ipi Kali Kuliko Zote?

Flagship Mobile Phone 2013: Ni Ipi Kali Kuliko Zote?

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
Simu Bora 2013 Mpaka Sasa



​
Wakati kampuni mbili kuu zinazotamba kwa kutoa simu bora bado kutoa simu zao kuu za mwaka 2013, yaani Samsung Galaxy S4 na iPhone 5S/6, kampuni nyingine zote kubwa tayari zimeshatoa simu zao bora za mwaka huu. Samsung inatarajiwa kufanya uzinduzi wa Galaxy S4 jijini New York kiasi wiki mbili kuanzia sasa yaani tarehe 14/03/2013, kwa kawaida Apple hutangaza simu yao mpya kwenye mwezi Septemba. Baadhi ya wadau wa teknolojia na gajeti wanatarajia huenda Apple mwaka huu wakatoa simu mbili yaani iPhone 5S na iPhone 6, ikiwa hii ni sahihi basi iPhone 5S huenda ikatoka mwezi wa nne mwaka huu.

Kampuni ambazo tayari zimeshatoa simu zao bora za mwaka (flagship device) ni pamoja na Nokia, LG, Asus, HTC, Sony na Blackberry. Tutazipitia simu hizo kwa ufupi na kuzungumzia kivutio kikuu na jambo au mambo ambayo huenda yakakwamisha mauzo mazuri ya kila moja wapo. Pia tutachagua na kuchambua ni ipi bora kuliko zote kwa maoni yetu. Kiujumla kampuni nne kati ya sita hizi zimetumia OS ya Android wakati Nokia peke yao wametoa simu ya OS ya Windows Phone. Blackberry kama kawaida yao hutumia OS yao binafsi ambayo ni ya aina ya QNX, safari hii ni toleo nambari 10.

[TABLE="class: tableizer-table"]
[TR="class: tableizer-firstrow"]
[TH="bgcolor: #104E8B"][/TH]
[TH="bgcolor: #104E8B"]Blackberry[/TH]
[TH="bgcolor: #104E8B"]HTC[/TH]
[TH="bgcolor: #104E8B"]LG[/TH]
[TH="bgcolor: #104E8B"]Nokia[/TH]
[TH="bgcolor: #104E8B"]Sony[/TH]
[TH="bgcolor: #104E8B"]Asus[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD]Jina[/TD]
[TD]Q10[/TD]
[TD]One[/TD]
[TD]Optimus G Pro[/TD]
[TD]Lumia 920[/TD]
[TD]Xperia Z[/TD]
[TD]PadFone Infinity[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]OS[/TD]
[TD]Blackberry 10 OS[/TD]
[TD]Android Jelly Bean[/TD]
[TD]Android Jelly Bean[/TD]
[TD]Windows Phone 8[/TD]
[TD]Android Jelly Bean[/TD]
[TD]Android Jelly Bean[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Gamba[/TD]
[TD]Plastiki[/TD]
[TD]Aluminiam[/TD]
[TD]Plastiki[/TD]
[TD]Plastiki[/TD]
[TD]Plastiki[/TD]
[TD]Aluminiam[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kamera[/TD]
[TD]8 MP[/TD]
[TD]4 UP-Altra[/TD]
[TD]13 MP[/TD]
[TD]8 MP[/TD]
[TD]13.1 MP[/TD]
[TD]13 MP[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]RAM[/TD]
[TD]2GB[/TD]
[TD]2GB[/TD]
[TD]2 GB[/TD]
[TD]1 GB[/TD]
[TD]2 GB[/TD]
[TD]2 GB[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Disk[/TD]
[TD]16GB[/TD]
[TD]32/64 GB[/TD]
[TD]32 GB[/TD]
[TD]32 GB[/TD]
[TD]16 GB[/TD]
[TD]32/64 GB[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Prosesa[/TD]
[TD]Dual Core 1.5 GHz[/TD]
[TD]Quad Core 1.7 GHz[/TD]
[TD]Quad Core 1.7 GHz[/TD]
[TD]Dual Core 1.5 GHz[/TD]
[TD]Quad Core 1.5 GHz[/TD]
[TD]Quad Core 1.7 Mhz[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Uzito[/TD]
[TD]137.5 g[/TD]
[TD]143 g[/TD]
[TD]160 g[/TD]
[TD]185 g[/TD]
[TD]146 g[/TD]
[TD]141 g[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Wembamba[/TD]
[TD]9 mm[/TD]
[TD]9.3 mm[/TD]
[TD]9.4 mm[/TD]
[TD]10.7 mm[/TD]
[TD]7.9 mm[/TD]
[TD]8.9 mm[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kioo[/TD]
[TD]4.2"[/TD]
[TD]4.7"[/TD]
[TD]5.5"[/TD]
[TD]4.5"[/TD]
[TD]5"[/TD]
[TD]5"[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kioo (ppi)[/TD]
[TD]355 ppi[/TD]
[TD]469 ppi[/TD]
[TD]401 ppi[/TD]
[TD]332 ppi[/TD]
[TD]441 ppi[/TD]
[TD]441 ppi[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]MicroSD[/TD]
[TD]Hadi 64GB[/TD]
[TD]Hamna[/TD]
[TD]Hadi 64GB[/TD]
[TD]Hamna[/TD]
[TD]32 GB[/TD]
[TD]Hamna[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]LTE 4G[/TD]
[TD]√[/TD]
[TD]√[/TD]
[TD]√[/TD]
[TD]√[/TD]
[TD]√[/TD]
[TD]√[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]NFC[/TD]
[TD]√[/TD]
[TD]√[/TD]
[TD]√[/TD]
[TD]√[/TD]
[TD]√[/TD]
[TD]√[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

(Uchambuzi zaidi wa simu moja moja umerukwa, fuata link ya chini ili kuisoma makala kwa ukamilifu)


MSHINDI KATI YA SIMU HIZI​


Sisi katika Gajetek Tumeipa Ushindi Sony Xperia Z katika orodha hii, Ifuatayo ni mfuatano wa simu hizi kwa ubora na sifa kuu nzuri :

1. Sony Xperia Z - haiathiriwi na maji na ina umbile bora kabisa kati ya hizi. Sony pia wametumia teknolojia ya Bravia kuiboresha simu hii na inarusha video kwenda kwenye TV za Sony bila ya kutumia waya, pia ni remoti ya TV zote za Sony.

2. Asus PadFone Infinity - Ni simu na tablet kamili, mtumiaji huokoa matumizi ya sim kadi mbili kwa kutumia simu hii.

3. HTC One - inaonekana ni yenye ubora kimaumbile (quality) na HTC Sense na Blink Feed ni kivutio kizuri. Na ina kasi sawa na simu mbili za juu kwa prosesa.

4. LG Optimus G Pro - Ni fablet yenye kuvutia ikiwa na kioo chenye ukubwa wa 5.5"

5. Nokia Lumia 920 - Ina simama kipekee kwa kuwa na OS ya Windows Phone, software yake ya kamera ni kivutio kikubwa.(uzito, unene na uchache wa apps umeiangusha Nokia Lumia 920 kiasi fulani)

6. Blackberry Z10 - Software mpya ya simu hii bado ina bugs tulipoijaribu hivi karibuni, pia uchache wa apps umeiangusha simu hii. Lumia na Z10 ndio simu zilizotumia prosesa zisizo na kasi (dual core 1.5 MHz) na zilzosalia zote zina quadcore.


Tunaamini wapo ambao watakao kuwa na maoni tofauti katika mlinganyo huu, tafadhali toa maoni yako chini ya makala hii, ni ipi orodha yako wewe kwa ubora kati ya simu sita hizi na tupe sababu ya ile uliyoichagua namba moja yako ikiwa si Sony Xperia Z10.

Makala hii ni mukhtasari, soma makala hii kwa ukamilifu kwenye link hii kabla ya kutoa maoni:
Gajetek - Gajet na Teknolojia: Simu Bora 2013 Mpaka Sasa

 
nokia ametoa simu Gan This Year!! from What I Know Bado Kabisaaa coz Lumia 920 Ilizinduliwa September Last Year Akimtangulia Week 1 Apple!! Ila nokia Alichelewa kui release Tofaut na Wenzao Apple Ambao Wali fanya Fasta Kuipeleka Mitaan... Nokia Alikuja Kuipeleka Mwanzon Mwa November... So sidhan Kama Ni Sahihi Kusema Nokia Ameshatoa Flagship Yake Mwaka Huu!! i Hope Umenielewaaaa

Pia Ww Umechukulia Vgezo Vp Kuipa Ushinda Xperia Z!!! maana Mm Najarbu Kum compare Na Htc Naona Kwa Specs Kazidiwa!! nme Wa Compare Hawa Coz Ndo Waliozinduliwa This Year Pamoja Na Asus Na Pia Wanatumia Os Moja So Ni Rahisi Kuwa Judge!!!
 
hapa ngoja Chifu Mkwawa aje maana naona nokia ipo hapa na kama imedhalilishwa vile.
 
nokia ametoa simu Gan This Year!! from What I Know Bado Kabisaaa coz Lumia 920 Ilizinduliwa September Last Year Akimtangulia Week 1 Apple!! Ila nokia Alichelewa kui release Tofaut na Wenzao Apple Ambao Wali fanya Fasta Kuipeleka Mitaan... Nokia Alikuja Kuipeleka Mwanzon Mwa November... So sidhan Kama Ni Sahihi Kusema Nokia Ameshatoa Flagship Yake Mwaka Huu!! i Hope Umenielewaaaa

Pia Ww Umechukulia Vgezo Vp Kuipa Ushinda Xperia Z!!! maana Mm Najarbu Kum compare Na Htc Naona Kwa Specs Kazidiwa!! nme Wa Compare Hawa Coz Ndo Waliozinduliwa This Year Pamoja Na Asus Na Pia Wanatumia Os Moja So Ni Rahisi Kuwa Judge!!!

naona umeanza kabla chief mkwawa hajatia mkono
 
kwa kamera na simu kutoingia maaji naona sony wapo juu lakini pia samsung galac=x s 4 pia una kab=va laku=e limetoka ambalo linaizuia hiyo simu isiingie maji so bado ni bilbila ktk ishu ya waterproof ila nokia kawapiga bao kwenye wireless charging
 
Bado mapema sana kutafuta simu bora ya mwaka, Labda mpaka tusubiri Q3 iishe ndo tutasema nani ni nani
 
Napenda kuona Africa watu wanafanya reviews zao zinazoangalia mazingira ya Africa.

Sio mtu ananunua simu kwa sababu kasoma review CNet simu imesifiwa kwa WiFi wakati bongo WiFi mpaka hoteli ya kitalii.
 
nokia ametoa simu Gan This Year!! from What I Know Bado Kabisaaa coz Lumia 920 Ilizinduliwa September Last Year Akimtangulia Week 1 Apple!! Ila nokia Alichelewa kui release Tofaut na Wenzao Apple Ambao Wali fanya Fasta Kuipeleka Mitaan... Nokia Alikuja Kuipeleka Mwanzon Mwa November... So sidhan Kama Ni Sahihi Kusema Nokia Ameshatoa Flagship Yake Mwaka Huu!! i Hope Umenielewaaaa

Pia Ww Umechukulia Vgezo Vp Kuipa Ushinda Xperia Z!!! maana Mm Najarbu Kum compare Na Htc Naona Kwa Specs Kazidiwa!! nme Wa Compare Hawa Coz Ndo Waliozinduliwa This Year Pamoja Na Asus Na Pia Wanatumia Os Moja So Ni Rahisi Kuwa Judge!!!

Ni kweli kwamba Nokia wametoa Lumia 920 mwishoni mwa mwaka jana, na this year wametoa simu mbili tu ambazo zimechoka kiasi kwamba hazifai kuingia katika orodha hii (Lumia 52- na 720). Kuna sababu mbili tumeiingiza Lumia 920 kwenye orodha hii:

1. Kama Nokia watakuwa consistent kama zilivyo kampuni nyingine ina maana flagship device yao itatoka tena mwishoni mwa mwaka huu hivyo haitakuwa na nafasi ya mauzo kwa mwaka huu bali mwakani.

2. CEO wa Nokia Corporation Mr. Stephen Elop akizungumza kwenye interview na Sky News kwenye MWC hivi karibuni ameeleza wazi kuwa line up ya Lumia devices imekamilika. Na ameeleza wazi kuwa Lumia 920 ndio flagship yao ya mwaka huu.

Hivyo kinyume na Apple na Samsung ambao S3 na iPhone 5 ni simu zao za mwaka jana Nokia Lumia 920 ndio inategemewa ku-drive reputation na sales za kampuni hiii.

Pia kuna mdau amezungumzia Wireless charger, ni kweli hichi ni kivutio lakini si practical, kwa sababu wireless charger iko slow mno, kwa nini nitumie wireless charger ambapo simu yangu itajaa chaji baada ya masaa 9 wakati nikitumia ya wire chaji inajaa baada ya masaa 2 au 3?

Mwisho kabisa nikumbushe kuwa Nokia iko karibu na mkiani kwa sababu kati ya simu hizi sita:

1. Nokia ni nene (pana) kuliko zote

2. Lumia 920 ni nzito kuliko zote (hali ya kuwa sio kubwa, actually ni ya pili kwa udogo)

3. WP ni OS ya pili kwa uchache wa apps baada ya BB OS.

4. Processor yake ndio slowest kuliko zote (sawa na BB Z10)

5. Pixel per inch (PPI) ni chache kuliko zote

6. Kamera yake ina pixel chache kuliko zote, sawa na BB Z10 (ukizingatia kwamba HTC One ina Ultrapixel badala ya megapixel)

Hivyo sababu pekee hawakukaa mkiani kabisa ni kwamba Blackberry Z10 nao wamechemsha katika mambo mengi zaidi.

Katika Corporate management kuna kitu kinaitwa CI (Competitive Intelligence) yaani kampuni kujaribu kufanya uchunguzi kujua wapinzani wanafanya nini, Nokia wanaonekana wako so "poor" kama kampuni katika eneo hili ndio maana wameshindwa ku-anticipate specs za hali ya juu ambazo simu mbali mbali itakuja nazo mwaka huu na kuifanya simu yao kuonekana mediocre phone. Nadhani wakati umefika Nokia waamke na wabadili mkakati au wataendelea kuanguka kimauzo.
 
Bado mapema sana kutafuta simu bora ya mwaka, Labda mpaka tusubiri Q3 iishe ndo tutasema nani ni nani

Ni kampuni mbili tu ambazo zimebakia kutoa simu zao bora (flagship device), yaani Apple na Samsung, lakini kampuni zote ambazo zimeingizwa katika orodha hii hazitarajiwi kutoa simu bora zaidi kwa mwaka huu. Kwa mfano Nokia wametangaza simu mpya Lumia 520 na 720 ambazo ni za hali ya chini kuliko Lumia 920. Kwa ufupi hapa tunaangalia ni nani atashikilia namba 3, kwani matarajio ni kuwa S4 na iPhone 6 (ikiwa watatoa 6 na sio 5S) ndio zitakaa namba 1 na 2) kama ilivyokuwa mwaka jana na mwaka juzi.
 
maoni yangu ni hivi... >> Nokia bado hajatoa flagship phone yake mwaka huu, hiyo Lumia 920 imekuwepo tangu mwaka jana. >> Nokia na BB wana kazi kubwa sana as watu wengi wanaonunua simu wanasikiliza reviewers wa internet na magazeti, na hawajui kutofutisha specs au OS. wanavutiwa sana ni vitu kama screen size, dpi, app store. hii tabia ya kufwata upepo ulianza na wapenZi wa iPhone (which we all know are ---- phones) yaani iSheeps, na sasa kuna wa android fandroids. nokia wakati wake (siku za s60v3 na s60v5) walikuwa na fans wengi sana lakini wamewapoteza kwa android na BB ilikuwa ni nkitu cha kuonyesha uwezo wa kimfuko, lakini siku hizi not so much kwa kuwa kila manufacturer an simu za bei ghali >>simu kwa opinion yangu hazihitaji quad core procesors. hata computers za sasa hivi hazina programs zinazo profit from many processors. (mfano games nyingi zinatumia two processors na ukitumia quad core processor huoni increase in perfomance) na more processors= more power consumption. >>HTC One kwa maoni yangu ndo the best of the latest phones. nimechukia kuwa haina hot swappable MMC lakini pixels zake, new camera na aluminium zimenivutia sana regards, leh
 
Last edited by a moderator:
Napenda kuona Africa watu wanafanya reviews zao zinazoangalia mazingira ya Africa.

Sio mtu ananunua simu kwa sababu kasoma review CNet simu imesifiwa kwa WiFi wakati bongo WiFi mpaka hoteli ya kitalii.

Ni hoja nzito kaka, na sisi katika Gajetek tuna mtazamo wa kuzungumzia teknolojia na bara la Afrika, ndio maana miongoni mwa makala zetu ni pamoja na makala kama vile:

1. Gajetek - Gajet na Teknolojia: Apple yafungua AppStore Tanzania

2. Gajetek - Gajet na Teknolojia: Laptop a Mionzi ya Jua Madukani

3. Gajetek - Gajet na Teknolojia: Mtego wa Mbu, Eneo la Eka 1

4. Gajetek - Gajet na Teknolojia: Teknolojia Yapata Kasi Barani Afrika

5. Gajetek - Gajet na Teknolojia: Mustakbali wa Tanzania na Cloud

6. Gajetek - Gajet na Teknolojia: Microsoft na Huawei wazindua Simu ya Afrika

7. Gajetek - Gajet na Teknolojia: Simu Kupima Malaria

Hivyo unaweza kuona kwamba makala hizi si makala za CNET na Engadget au Gizmodo, bali ni makala za Bara letu, na pamoja na ukweli kwamba bado tuko nyuma kiteknolojia mimi siamini kwamba Bara la Afrika eti linahitaji simu za hali ya chini, kama ambavyo walivyofanya Microsoft na Huawei katika issue ya "Huawei 4 Afrika" huku wakitoa taswira kwamba kwa kufanya hivyo ndio wametoa kifaa chenye kuendana na mazingira yetu, hii si sahihi.
 
maoni yangu ni hivi... >> Nokia bado hajatoa flagship phone yake mwaka huu, hiyo Lumia 920 imekuwepo tangu mwaka jana. >> Nokia na BB wana kazi kubwa sana as watu wengi wanaonunua simu wanasikiliza reviewers wa internet na magazeti, na hawajui kutofutisha specs au OS. wanavutiwa sana ni vitu kama screen size, dpi, app store. hii tabia ya kufwata upepo ulianza na wapenZi wa iPhone (which we all know are ---- phones) yaani iSheeps, na sasa kuna wa android fandroids. nokia wakati wake (siku za s60v3 na s60v5) walikuwa na fans wengi sana lakini wamewapoteza kwa android na BB ilikuwa ni nkitu cha kuonyesha uwezo wa kimfuko, lakini siku hizi not so much kwa kuwa kila manufacturer an simu za bei ghali >>simu kwa opinion yangu hazihitaji quad core procesors. hata computers za sasa hivi hazina programs zinazo profit from many processors. (mfano games nyingi zinatumia two processors na ukitumia quad core processor huoni increase in perfomance) na more processors= more power consumption. >>HTC One kwa maoni yangu ndo the best of the latest phones. nimechukia kuwa haina hot swappable MMC lakini pixels zake, new camera na aluminium zimenivutia sana regards, leh


Big up kaka, hoja za msingi sana, ni kweli wakati mwengine uvumbuzi wa teknolojia unakuwa unawafanya manufacturers kuwahadaa watumiaji wa vifaa, ndio maana utaona simu mbali mbali zina matatizo ya charger kwa vile processor zinazotumiwa ni power hungry. It is difficult to get the balance right sometimes kwa vile kuna apps za simu ambazo zinahitaji power kutokana na graphics za hali ya juu na multiple activities, hasa katika games.

Ndio maana mimi binafsi nilivutiwa sana pale Snapdragon ilipotoka na quadcore ambazo zina core ya ziada (5 cores) ambapo ya ziada hufanya kazi peke yake pale mtumiaji anapotumia light weight functions kama kusoma email na ku-surf net. Na unapocheza game kwa mfano basi ndio simu ina activate core nne. Hivyo unapata good gaming experience na pia una-save betri.
 
maoni yangu ni hivi... >> Nokia bado hajatoa flagship phone yake mwaka huu, hiyo Lumia 920 imekuwepo tangu mwaka jana. >> Nokia na BB wana kazi kubwa sana as watu wengi wanaonunua simu wanasikiliza reviewers wa internet na magazeti, na hawajui kutofutisha specs au OS. wanavutiwa sana ni vitu kama screen size, dpi, app store. hii tabia ya kufwata upepo ulianza na wapenZi wa iPhone (which we all know are ---- phones) yaani iSheeps, na sasa kuna wa android fandroids. nokia wakati wake (siku za s60v3 na s60v5) walikuwa na fans wengi sana lakini wamewapoteza kwa android na BB ilikuwa ni nkitu cha kuonyesha uwezo wa kimfuko, lakini siku hizi not so much kwa kuwa kila manufacturer an simu za bei ghali >>simu kwa opinion yangu hazihitaji quad core procesors. hata computers za sasa hivi hazina programs zinazo profit from many processors. (mfano games nyingi zinatumia two processors na ukitumia quad core processor huoni increase in perfomance) na more processors= more power consumption. >>HTC One kwa maoni yangu ndo the best of the latest phones. nimechukia kuwa haina hot swappable MMC lakini pixels zake, new camera na aluminium zimenivutia sana regards, leh
Hivi hao HTC wana simu za chini ya laki tano.?
 
Hivi hao HTC wana simu za chini ya laki tano.?


HTC Desire C Kama laki 3 hivi unaweza kuipata. Inatumia Android (ICS)

Kioo 3.5", kamera 5mp, 4Gb internal storage na memory card slot...

Unknown.jpeg

Pia wana HTC Windows Phone 8S kama laki tano hivi.
wp8s3viewsblue.jpg
 
Back
Top Bottom