Fitina: Nani katika hawa alimdanganya Dkt. Magufuli kuwa Drone za kuzimia moto ni Camera

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
“Zana za zimamoto ziko outdated , Fikiria Moto uanze PSPF tower floor ya 20 hakuna gari litazima moto kule,Isipokuwa drones,kwa bahati mbaya waliomuelezea mkuu wetu walimdanganya kuwa drone ni camera na zimesainiwa mabilion kumbe ni ndege ndogo za kuzima moto“-Mh Kangi Lugola.

Hii ni kauli ya aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ambaye alikuwa anapenda sana kiki na kuonekana kiherehere kwelikweli , Kauli hii imenifikirisha kidogo na kunianya nifukue makaburi. Ukifuatilia mtirirko wangu hapo chini nilipoHIGHLIGHT kwa rangi nyeusi au Nyekundu, inaonekana wazi kabisa Kangi na Andengenye walikuwa na mpango mzuri wa maboresho ye jeshi Zimamoto ndo maana hawakufanya kwa siri , watu wengi walipewa dodoso na mwishowe hata JPM alipewa mwishoni kama approval. Ila hii dili ya hivi vifaa ilikuwa ni mtego uliokuwa unakuja kummaliza Kangi kwani alichukiwa sana hasa kwa kuwabana na kuwapelekesha Manyota na wakijaribu kumgusa alikuwa akikata sana mauno kwenye masherehe na kumsifu Mkuu, ndo maana alikuwa hagusiki kwa sifa alizokuwa anatoa kwa mkuu.

Rais Magufuli alisema Andengeye alisaini mkataba huo ambao haujapangwa kwenye bajeti na haujapitishwa na Bunge ambao ulilenga kununua vifaa mbalimbali vya zima moto zikiwamo ‘drones.’ Lakini tujiulize , je yeye JPM ni mikataba mingapi na matumizi mangapia alifanya na ya hayakupangwa kwenye bajeti wala kupitishwa na bunge?. Ndo maana na huu nao walimpelekea sababu angeupenda angeuthibitisha. Too bad haukuwa wa ujenzi ama kujenga structure,daraja au barabara.

Rais Magufuli alisema wakati wa vikao na kampuni moja ya Romania, wahusika wote wa Tanzania waliokuwa wanakwenda katika majadiliano walikuwa wanalipwa Dola 800 za posho ya vikao na tiketi za ndege.“Naibu waziri (mambo ya ndani- Hamad Masauni) anajua, ingawaje hakuhusishwa sana alikuwa anapewa nakala ya madokezo ananyamaza, angeweza akaja hata mapema serikalini akaeleza ninaona dokezo limetolewa na waziri wangu (Lugola) linahusu hiki. Sifahamu kwa nini alitulia,” alisema Rais Magufuli huku Masauni aliyekuwapo akisimama na kuinama kwa heshima.

Naibu katibu mkuu(Ramadhani Kailima) amehusika sana, tangu kuanza kwake mpaka mwisho, kuna watendaji wengine kwenye jeshi la zima moto wamehusika, ndiyo hao wengine walikuwa wanakwenda kwenye vikao wanapewa dola 500, dola 300 na wanapewa Laptop. Waziri aliyetumbuliwa (Lugola) analeta kibarua anasema nithibitishe tu, nathibitishaje kitu ambacho sikijui, unakwenda wizara sijui ina mapepo, nenda kasimamie na yale utakayoweza kubadili kayabadili na wanaoweza kuondolewa kawaondoe,” alisema Rais Magufuli.

Analysis: Hapo JPM alisema Andengenya amesaini Mkataba huo, si kweli haukusainiwa , Ndo maana hapa Mwisho Kangi alikuja kwa JPM kwa ajili ya kuthibitisha. Kwa hiyo maana yake wao walikuja na proposal ya walichokuwa wakijadiliana ambayo muamuzi alikuwa yeye JPM. Posho za Vikao Ddola 500 mpaka 300 kwa wenzetu si hela nyingi , hapa JPM alihukumu kwa hisia. Kiongozi wa kiserikali kupata Dola 300 ya posho nchi ya ugenini si kubwa ni ya kawaida. Kupewa Laptop si big deal pia kwa wenzetu ni kama kupewa Notebook. Na sidhani kama ni zawadi inayoweza kumstua Waziri au makatibu wake. Hap JPM alituhadaa kuteka hisia zetu tu. Katika Ubanaji Matumizi ilikuwa sawa kupewa Posho huko, Labda walipoitwa kwenye Presentation na mijadala walikubaliana Posho itatoka upande wa Mzabuni. Ilikuwa sawa pia kwa ubanaji matumizi.

Ajabu katika wote waliotajwa kuhusika:

Andengenya aliteuliwa Mkuu wa Mkoa Kigoma
Masauni alibaki Naibu Waziri
Ramadhani Kailima alibaki Nibu katibu Mkuu
Kingu ni kwa sababu alijiuzulu mwenyewe, ni mwanajeshi na hakutaka Uswahiliswahili tena kulinda heshima yake
Mwisho wa siku ni Lugola Pekee aliyetolewa Nje na JPM. Hili lilikuwa ni zengwe maalum na walioratibu tunaweza kuwajua hapo chini

E6ChklpVIAEZCVY.jpg


Kiuhalisia kilichomng`oa Lugola ni Hiki:
Turejee siku Simbachawene anaapishwa
JPM alimsifu Simbachawene kwa hotuba nzuri aliyoitoa akisema, “umezungumza vizuri hapa, kwamba wewe (Simbachawene) huna nyota hata moja, hivi vyombo vya ulinzi na usalama vina namna yake ya kuviongoza.Ndiyo maana Waziri Mwinyi amekaa sana Wizara ya Ulinzi, hawezi kusimama pale mbele na kuwatukana mabrigedia hawa, anajua jinsi ya kufanya nao kazi, katumie mbinu hizo hizo,”

“Ndiyo maana mnaona wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wana uwezo wa kuripoti moja kwa moja kwa Rais, sasa ukishapima hayo, hii inaweza kukusaidia sana jinsi ya kuongoza.” (Hapa Simbachawene anatishwa kuwa hao wanaongea na Rais pia, asijione yuko juu yao)

“Najua wewe ni mwanasheria, ulipoanza hapa kuzungumza nikamwona IGP (Simon Sirro) anatingisha kichwa, nafikiri amefurahi sana,” alisema Rais Magufuli huku IGP Sirro akisimama akiwa na uso wa tabasamu na kupiga saluti ya utii kwa Amiri Jeshi Mkuu huyo wa nchi. (Inafikirisha hapa, JPM alihitaji sapoti ya Vyombo vya Dola kenye Uchaguzi, nadhani tunaelewana)

“Saa nyingine alikuwa anakuja kwangu (IGP) analalamika anasema nimeshaambiwa hawa niwatoe, lakini amri haizungumzi hivyo, nikamwambia bwana nenda kawatoe, lakini kiukweli saa nyingine siyo utaratibu na mara nyingi tukifuata utaratibu itatusaidia,”
(Hapa Simbachawene anapigwa stop kuwachukulia hatua Manyota Ingawa Rais Magufuli hakumtaja kwa jina Lugola, lakini alifahamika kwa kuadhibu, kurekebisha, kushusha vyeo na kuwajibisha wakosefu huku mara kadhaa akitoa maagizo kwa IGP Sirro ya kuhamisha makamanda wa polisi.Katika kipindi cha siku 571 cha Lugola kukaa ndani ya wizara hiyo kuanzia Julai Mosi, 2018 hadi Januari 23 alipotenguliwa, alifanya ziara mbalimbali mikoani na kuendesha vikao kazi vya taasisi zilizo chini yake na alishuhudiwa akiwafukuza vikaoni makamanda wa polisi, kuagiza washushwe vyeo, wengine kuwekwa mahabusu na kuhamishwa.)

Mwisho kwa jicho la tatu lenye kufikirisha namtazama Sirro na Kingu,Namtazama Masauni kisha Kailima, then najiuliza ni nani alipeleka Waraka wa Hayati Aboud Jumbe Mikononi mwa Hayati Mwalimu Nyerere?

I stand to be corrected!

Niwatakie Wiki Njema Wanabodi
Shujaa Mwenazake
Chato, Geita
 
Dikteta alikuwa hapitishi mkataba wowote ambao hana 20%

Na alikurupuka , hasa ndo maana alikazia kuwa Drone ni Camera. Kiuhalisia haikuwa hivyo.

JPM alikuwa anapenda kusema "Mikataba ya Hovyo" . It was better mkataba wenyewe angeimwaga hadharani tuone uhovyo wake.

Na shida ya tatu,mkubwa hapingwi wala hakosolewi na mteule. Ndo maana kina Andengenye wakaamua kukaa kimya.
 
Na alikurupuka , hasa ndo maana alikazia kuwa Drone ni Camera. Kiuhalisia haikuwa hivyo.

JPM alikuwa anapenda kusema "Mikataba ya Hovyo" . It was better mkataba wenyewe angeimwaga hadharani tuone uhovyo wake.

Na shida ya tatu,mkubwa hapingwi wala hakosolewi na mteule. Ndo maana kina Andengenye wakaamua kukaa kimya.
Mgao kwake uliuwa mdogo. Over
 
Licha ya kuwa na PhD bado aliamini drone ni Camera
hatuwezi jua specs za drone zilizotaka kununuliwa maana drone zipo za aina tofauti lakini kwa ufahamu wangu mpaka sasa drone hutumika na na vikosi vya zima moto ku identify hot-spots ili waweze kufanikisha kuzimamoto,zaidi huona wana tumia helkopta maaana zaweza kubeba maji mengi kwa kazi hiyo
 
Back
Top Bottom