Fiston Mayele na Litombo Bangala walichomfanyia Inonga ni kumkosea Heshima na kukiuka haki za Binadamu, TFF iingilie kukomesha hii tabia

Huu ni mpira inabidi uwe fair na haki za binadamu zizingatiwe na hata Fifa wanahimiza sana.

Cha ajabu klabu a Yanga inajiona ipo juu ya sheria na kufanya kinyume, Inonga akiwa baada ya mechi alikuwa anawahi kwenda kutafta sehemu ya mapumziko lakini ghafla mbele yake akazingirwa na wachezaji wa Yanga, Fiston Mayele na Litombo Bangala wakamvamia na kumfanyia shambulio la aibu,,

Tff ni wajibu kulichunguza hili

View attachment 2323275
Acha kulialia. Mjomba wenyu Karihia wa kule tifaifu. Anaugulia maumivu ya sindano mbili alizopewa leo bila ganzi....
 
Inonga jana kacharazwa yeye. Halafu kuanzia leo naacha kuchukulia mpira serious aisee utaniua jana hata usingizi umepaa na hivyo na mr nae ni simba kindakindaki basi kila mtu aligeukia upande wake. Itoshe kusema ntashangilia kwa kiasi.
 
Mpira ukiuchukulia siriaz unamtoa mtu mood hata kumuua jitahidi uwe unashabikia kiasi kama mimi niko poa hata timu yangu ipigwe naenjoy tu maumivu kidogo mno tena kwa dakika chache tu.
 
Weee naye chuki na hasira zimekujaaa ,hayo ni mawazo mgando ,, SA ujinga gan huo TFF iingilie utan wa hao wakongo ?
 
Weee naye chuki na hasira zimekujaaa ,hayo ni mawazo mgando ,, SA ujinga gan huo TFF iingilie utan wa hao wakongo ?
Jamaa ni Yanga hapa anataka anafanya utani kwa mpango wa nyuma ili makolo wajitokeze kusoma uzi na kuona video wazidi kukureka..
 
Mpira ukiuchukulia siriaz unamtoa mtu mood hata kumuua jitahidi uwe unashabikia kiasi kama mimi niko poa hata timu yangu ipigwe naenjoy tu maumivu kidogo mno tena kwa dakika chache tu.
Sure mkuu, ni ubatili mtupu
 
Mkuu tutulie tumefungwa wale ni wacongo wanataniana.
Tu deal na mambo yetu kama kocha asiye na mbinu n.k
 
Me ni Simba Ila nimefurah kufungwa na yanga ,huyu inonga huenda akapunguza sifa za kijinga kwenye issues za maana
Kwanini, usihamie yanga upate furaha kamili?, Kwasababu, tatizo siyo la Inonga peke yake. Hatahivyo, yanga inawachezaji mahiri kuliko Simba.
Kwahiyo, ushindi wa yanga hausabishwi na Nabi ila wachezaji wako vizuri uwanjani.
Ni ngumu sana ukampeleka NABI Mbeya kwanza halafu Mbeya kwanza ikafanya vizuri sana.
Ingawa sijui kama yanga itatoboa kimataifa. Ila mwaka huu kapewa timu vibonde(CAF).
 
Back
Top Bottom