Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,041
- 39,989
Habari za jioni mabibi na mabwana....
Habari za siku tele...
Poleni na hongereni na mishughuliko ya kutwa nzima. Ni kitambo kidogo tangu niseme kuwa Kasie is back, nilibanwa na jukumu flani hivi ambalo nshalimaliza na kesho narejea Dar.
Ni takriban wiki sasa niko huku Ikunglyubashashi kitongoji ambacho sio mbali sana na Koromije. Hii habari sio ya kisiasa ni moja ya matukio anayokutana nayo Kasie uso kuwa uso akiwa kwenye hamsini zake.
Ilikuwa hivi, Kasie bibi maringo pamoja na maringo na majivuno yake yote, anapenda kula vitu vitamu bin vizuri. Sasa tangu nifike hapo Ikungu... chakula changu ilikuwa ni samaki tuu. Kama kawaida ya Kasie kabla sijaagiza chakula huwa napenda kumuuliza chef au mpishi wa hoteli niliyofikia. Baada ya kusalimiana na chef mawili matatu nilimuuliza nikiagiza samaki atasindikizwa na kitugani kwenye sahani...
Siku hiyo chef akaniambia leo nakuandalia Fish Koromije.... mmmhh nikawa na shauku ya kula huo msosi wa Fish Koromije. Punde si punde masosi ukafika uuuhhhh wazungu wanasema the food was mouth-watering.... nilipomaliza kula nikamwambia mpishi naomba kwa siku hizi zilizobakia kila siku nile Fish Koromije hehehehe.
Fish Koromije ni samaki anakuwa amekaangwa kisha juu yake anamwagiwa source shatashata lililoungwa na karanga..... hii ni sababu nampenda wa Ikunglyubashashi maana si kuwa utamu ule wa Fish Koromije..... wa ikungulyabashashi wangu utamu wake ni zaidi ya Fish Koromije.
Kasie kwa upande mwingine ana asili ya Tanga ambako mapishi yanasifika, nilimuuliza chef anipe maelezo jinsi ya kupika Fish Koromije ili dadii wangu akija nimpikie msosi wa nyumbani kwao shurti ajilambe.
Pamoja na ukorofi, Kasie akipata nafasi huwa anapika barabara. Namshukuru chef wa Ikungu... kwa kutokuwa mchoyo na sasa nimeongeza ujuzi wa pishi la Fish Koromije.
Nimejikuta nimekumbuka Ile uzi wa Samaki anavipande 3......
Niwatakie usiku mwema nyote, kesho narejea ngamani Darisalama.
Alamsiki.