BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
- Thread starter
- #21
Mkuu, pamoja na yote sijaona maana ya BAK kubwatuka namna hiyo, ni vema akatoa sababu za msingi kwa Mbunge huyo kuwa fisadi, na hii iwe mbali na msharahara wake na marupurupu mengine yatokanayo wadhifa wake kama Mbunge.
Miye ni mmoja wa wale Wehu ambao hawaoni kwamba Kikwete anastahili kugombea tena 2010. Kwa hiyo kama huzijui sababu zilizofanya Mzindakaya awe katika kundi la mafisadi, basi sidhani kama utaweza kuelewa chochote mimi mwehu nikikueleza sababu hizo. Kama unamuona Mzindakaya ni malaika kila la heri tuache sisi wehu tuendelee kumuona Mzindakaya kama ni mmoja wa mafisadi wakubwa nchini na tuna sababu nyingi za kumuona Mzindakaya kama ni fisadi. Miye namfahamu huyu bwana kwa karibu sana tena kwa miaka mingi tu.