Fisadi mwingine huyu

Mkuu, pamoja na yote sijaona maana ya BAK kubwatuka namna hiyo, ni vema akatoa sababu za msingi kwa Mbunge huyo kuwa fisadi, na hii iwe mbali na msharahara wake na marupurupu mengine yatokanayo wadhifa wake kama Mbunge.

Miye ni mmoja wa wale Wehu ambao hawaoni kwamba Kikwete anastahili kugombea tena 2010. Kwa hiyo kama huzijui sababu zilizofanya Mzindakaya awe katika kundi la mafisadi, basi sidhani kama utaweza kuelewa chochote mimi mwehu nikikueleza sababu hizo. Kama unamuona Mzindakaya ni malaika kila la heri tuache sisi wehu tuendelee kumuona Mzindakaya kama ni mmoja wa mafisadi wakubwa nchini na tuna sababu nyingi za kumuona Mzindakaya kama ni fisadi. Miye namfahamu huyu bwana kwa karibu sana tena kwa miaka mingi tu.
 
VETERAN politician Dr Chrisant Mzindakaya yesterday attacked critics of President Jakaya Kikwete's leadership, saying in most cases their accusations and complaints against him were not based on facts.

- Kwanza mbunge anasema kwamba complaints hazina facts! Halafu anakuja chini hapa anasema sio sawa kumshambulia Rais Kikwete peke yake, badala yake iwe ni viongozi wote:-

"It is also not proper to single out Mr Kikwete alone, instead of the entire leadership that collectively runs the country," said Dr Mzindakaya, the Member of Parliament for Kwela constituency (CCM), in Rukwa Region.

- Halafu anabadilika tena na kusema Rais alichaguliwa na viongozi wengine pia, ona hapa chini:-

He said Mr Kikwete was elected along with MPs, Councillors and other leaders at grass roots level. "The entire leadership is, therefore, collectively responsible

- Sasa unakaa na kujiuliza hivi hili taifa tulimkosea nini Mungu? Sisi wananchi wa Tanzania tumlimchagua Rais kuongoza taifa, yaani sisi wananchi na tukampa nafasi kikatiba kuchagua washauri wake na wasaidizi wa kutimiza lengo letu kwenye taifa, sasa leo tunaposema ameshindwa kazi tuliyompa, Mzindakaya anasema nini tena? eti tuwashambulie viongozi wote, wakati kamati ya bunge imeshasema wazi kwa kuwataja kwa majina wahusika wa Richimonduli na hata ikatoa ushauri wa nini kifanywe kisheria kuwaadhibu majambazi wakubwa kina Lowassa, Rostam, Msabaha, Karamagi, Mwakapugi, mpaka Hosea, sasa tulitegemea our Chief Law-Enforcement Officer, Rais wa jamhuri Kikwete awashughulikie haraka inavyotakiwa, sasa kama ameshindwa ashambuliwe nani madiwani?

- I mean wabunge wamefanya kazi yao, kuanzia kamati ya Mwakyembe, mpaka bunge zima limeipitisha ile ripoti, sasa Mzindakaya anataka tuwalaumu madiwani kwamba kwa nini ripoti haijfanyiwa kazi badala ya kiongozi tuliyemchagua kusimamia sheria za jamhuri yaani Rais wa jamhuri! Sasa kama huyu ni mbunge tena wa toka enzi za Mwalimu, sasa tutegemee nini kutoka kwa Rais? Maana hawa kina Mzindakaya ndio washauri wenyewe wa Rais, na believe me anawawakilisha wengi sana na hizi nonsense!

- Kwanza anasema hakuna facts, halafu anasema asishambuliwe Rais peke yake maana makosa sio yake peke yake na wengine pia, mweeee! Mungu mweeee! hivi tulikukosea nini hili taifa? Wa-Tanzania inabidi tuendelee kushambulia hapo hapo maana inaonekana this time message imefika, tulisema huko nyuma kuwa iko siku the buck itafikishwa inapotakiwa, yaani mezani kwa Rais na sasa imefika!

- I mean Rais wa jamhuri anaulizwa na kina Butiku na Quaresi, kwamba yeye kama Chief Law Enforcer wa Jamhuri hii, kwa nini majambazi wa Richimonduli wapo nje, yeye anajibu kwamba eti ni wivu na chuki, Sophia aliposema ni wivu na chuki kule kwenye kamati ya Mwinyi, tulidhani amepagawa kumbe sasa inaonekana kuwa huenda ndiyo lugha ya huko Ikulu, kwamba kila anayekosoa ana wivu na chuki ya kukosa Urais na u-First Lady, pleeease tulijua tu kuna siku yatawafika shingoni kuhadaa wanachi, kununua media, kuwatumia kina Tido Mhando na polls fake, kuwatumia waalimu wa mlimani, mihela ya Iran, kuwachafua kina Salim, yote haya ya yalikuwa ya nini kama kweli mlikuwa na uwezo wa kuongoza?

- Sasa saa imefika ya kuhesabiwa mnalia wivu na chuki, mkatishia weee kwamba Mtandao msipopewa uongozi basi taifa halitakalika wala halitaongozeka garademiti, sasa uongozi umewashinda mnalilia wivu na chuki, maana Quaresi naye aligombea urais sasa ana chuki za kuukosa na mkewe kukosa u-First Lady pure nonsense!, unajua inafurahisha sana mnavyoumbuka ingawa on the other hand pia inasikitisha sana kwa sababu mnaumbuka kwa ghrama ya migongo ya umasikini wa wanachi walalahoi!

Mungu Aibariki Tanzania!

Respect.

FMEs!

Miye ni mmoja wa wale Wehu ambao hawaoni kwamba Kikwete anastahili kugombea tena 2010. Kwa hiyo kama huzijui sababu zilizofanya Mzindakaya awe katika kundi la mafisadi, basi sidhani kama utaweza kuelewa chochote mimi mwehu nikikueleza sababu hizo. Kama unamuona Mzindakaya ni malaika kila la heri tuache sisi wehu tuendelee kumuona Mzindakaya kama ni mmoja wa mafisadi wakubwa nchini na tuna sababu nyingi za kumuona Mzindakaya kama ni fisadi. Miye namfahamu huyu bwana kwa karibu sana tena kwa miaka mingi tu.
Haijalishi ni kwa namna gani unamfahamu Mhe. huyo, zaidi inanifanya nikuone wewe ni zaidi ya mwehu kwa kuja na tuhuma za kwenye magazeti, ambayo kwa nafasi yao yameaumua kuwa tofauti na Mhe. kwa utashi wao binafsi.

Pengine kutokana na ufahamu wako au ukaribu wako na Mbunge huyo, kumekufanya uwe na chuki binafsi, hata hivyo kwa upande wetu tutasikia kelele zako pasipo majibu. Kwani huyo sio Mnyika ama Slaa ama Zitto kana kwamba ataweza kuja hapa na kukujibu.

Siwezi kukaa kimya na kukuacha ukipandikiza mbegu za chuki, dhihaka na kejeli huku ukijiita mwehu ili kupata huruma za wanaJF. Usipokuwa na ushahidi na tuhuma zako utaelezwa tu, na pengine ni vema kujua kwamba hapa sio genge la kupayuka tu! Hata hao magwiji wa kupayuka na kupaka matope serikali yetu huwa tunawapasha humu humu ndani.

Sio siri kwamba kuna ufisadi ndani ya serikali, ila ni vema kuja na hoja kamilifu juu wa ufisadi husika, zaidi ya madai ya kumjua mtu kibinafsi. Nchi haijengwi kwa majungu!
 
[Kibunango;693989]Ulofa na undumilakuwili umewajaa wengi humu... BAK huna hoja, umejichokea ile mbaya! Endelea na system yako ya kukopi na kupaste, ila usijitie kujua kwani hujui chochote![/QUOTE]

We kibunango pia ni walewale tu, fisadi, ingawa ni bado uchwara, sijui mmetumwa nyie, mnanikera na hilo li-chama lenu la mafisadi, sasa unamtetea mzindakaya ili iweje. Nyie wote Mafisadi tu.
 
We kibunango pia ni walewale tu, fisadi ingawa ni bado uchwara, sijui mmetumwa nyie, mnanikera na hilo li-chama lenu mafisadi, sasa unamtetea mzindakaya ili iweje. Nyie wote Mafisadi tu.
Mtizame na huyu! Sijui katokea shamba gani! Hivi kuna fisadi uchwara na fisadi tajiri? Ulofa mwingine unatia shaka!
 
- Kwanza mbunge anasema kwamba complaints hazina facts! Halafu anakuja chini hapa anasema sio sawa kumshambulia Rais Kikwete peke yake, badala yake iwe ni viongozi wote:-

- Halafu anabadilika tena na kusema Rais alichaguliwa na viongozi wengine pia, ona hapa chini:-

- Sasa unakaa na kujiuliza hivi hili taifa tulimkosea nini Mungu? Sisi wananchi wa Tanzania tumlimchagua Rais kuongoza taifa, yaani sisi wananchi na tukampa nafasi kikatiba kuchagua washauri wake na wasaidizi wa kutimiza lengo letu kwenye taifa, sasa leo tunaposema ameshindwa kazi tuliyompa, Mzindakaya anasema nini tena? eti tuwashambulie viongozi wote, wakati kamati ya bunge imeshasema wazi kwa kuwataja kwa majina wahusika wa Richimonduli na hata ikatoa ushauri wa nini kifanywe kisheria kuwaadhibu majambazi wakubwa kina Lowassa, Rostam, Msabaha, Karamagi, Mwakapugi, mpaka Hosea, sasa tulitegemea our Chief Law-Enforcement Officer, Rais wa jamhuri Kikwete awashughulikie haraka inavyotakiwa, sasa kama ameshindwa ashambuliwe nani madiwani?

- I mean wabunge wamefanya kazi yao, kuanzia kamati ya Mwakyembe, mpaka bunge zima limeipitisha ile ripoti, sasa Mzindakaya anataka tuwalaumu madiwani kwamba kwa nini ripoti haijfanyiwa kazi badala ya kiongozi tuliyemchagua kusimamia sheria za jamhuri yaani Rais wa jamhuri! Sasa kama huyu ni mbunge tena wa toka enzi za Mwalimu, sasa tutegemee nini kutoka kwa Rais? Maana hawa kina Mzindakaya ndio washauri wenyewe wa Rais, na believe me anawawakilisha wengi sana na hizi nonsense!

- Kwanza anasema hakuna facts, halafu anasema asishambuliwe Rais peke yake maana makosa sio yake peke yake na wengine pia, mweeee! Mungu mweeee! hivi tulikukosea nini hili taifa? Wa-Tanzania inabidi tuendelee kushambulia hapo hapo maana inaonekana this time message imefika, tulisema huko nyuma kuwa iko siku the buck itafikishwa inapotakiwa, yaani mezani kwa Rais na sasa imefika!

- I mean Rais wa jamhuri anaulizwa na kina Butiku na Quaresi, kwamba yeye kama Chief Law Enforcer wa Jamhuri hii, kwa nini majambazi wa Richimonduli wapo nje, yeye anajibu kwamba eti ni wivu na chuki, Sophia aliposema ni wivu na chuki kule kwenye kamati ya Mwinyi, tulidhani amepagawa kumbe sasa inaonekana kuwa huenda ndiyo lugha ya huko Ikulu, kwamba kila anayekosoa ana wivu na chuki ya kukosa Urais na u-First Lady, pleeease tulijua tu kuna siku yatawafika shingoni kuhadaa wanachi, kununua media, kuwatumia kina Tido Mhando na polls fake, kuwatumia waalimu wa mlimani, mihela ya Iran, kuwachafua kina Salim, yote haya ya yalikuwa ya nini kama kweli mlikuwa na uwezo wa kuongoza?

- Sasa saa imefika ya kuhesabiwa mnalia wivu na chuki, mkatishia weee kwamba Mtandao msipopewa uongozi basi taifa halitakalika wala halitaongozeka garademiti, sasa uongozi umewashinda mnalilia wivu na chuki, maana Quaresi naye aligombea urais sasa ana chuki za kuukosa na mkewe kukosa u-First Lady pure nonsense!, unajua inafurahisha sana mnavyoumbuka ingawa on the other hand pia inasikitisha sana kwa sababu mnaumbuka kwa ghrama ya migongo ya umasikini wa wanachi walalahoi!

Mungu Aibariki Tanzania!

Respect.

FMEs!

Sasa kama mheshimiwa raisi naye ana fikra za namna hii, kuna uongozi kweli???????????? What is ths wivu na chuki??? halafu watanzania tutegemee mabadiliko, maendeleo kutoka viongozi wa namna hiiii!!!!!!!!!!!!
 
Haijalishi ni kwa namna gani unamfahamu Mhe. huyo, zaidi inanifanya nikuone wewe ni zaidi ya mwehu kwa kuja na tuhuma za kwenye magazeti, ambayo kwa nafasi yao yameaumua kuwa tofauti na Mhe. kwa utashi wao binafsi.

Pengine kutokana na ufahamu wako au ukaribu wako na Mbunge huyo, kumekufanya uwe na chuki binafsi, hata hivyo kwa upande wetu tutasikia kelele zako pasipo majibu. Kwani huyo sio Mnyika ama Slaa ama Zitto kana kwamba ataweza kuja hapa na kukujibu.

Siwezi kukaa kimya na kukuacha ukipandikiza mbegu za chuki, dhihaka na kejeli huku ukijiita mwehu ili kupata huruma za wanaJF. Usipokuwa na ushahidi na tuhuma zako utaelezwa tu, na pengine ni vema kujua kwamba hapa sio genge la kupayuka tu! Hata hao magwiji wa kupayuka na kupaka matope serikali yetu huwa tunawapasha humu humu ndani.

Sio siri kwamba kuna ufisadi ndani ya serikali, ila ni vema kuja na hoja kamilifu juu wa ufisadi husika, zaidi ya madai ya kumjua mtu kibinafsi. Nchi haijengwi kwa majungu!

Ha ha ha wengine mnataka kutetea ambavyo hata havistahili kutetea kabisa. Nimeshakwambia mimi mwehu sasa cha ajabu kipi mimi kuwa mwehu. Sidhani kama utaukubali ukweli hata ukionyeshwa maana hata chongo utaita kengeza. Eti ushahidi wa magazetini si ushahidi!...LOL! Jina la bank limewekwa na kiasi alichochukua Fisadi Mzundakaya kimewekwa, bank husika haikukanusha habari hii kama ni uwongo lakini bado hutaki kuamini! Nenda katafute ushahidi wako ili uupinge ushahidi huu wa kutoka gazetini

Nadhani unakumbuka ile list ya mafisadi iliyotolewa na Dr Slaa na wote kumshinikiza afute kauli yake au watamfungulia mashtaka kortini kwa kuwaharibia "reputation" zao,lakini hakuna hata mmoja aliyethubutu kufungua kesi dhidi ya Dr Slaa kwa kuwekwa katika list ya wanaoifisadi Tanzania

Heri yangu mimi mwehu ninayetetea maslahi ya nchi yangu kuliko fisadi Kibunango anayeifisadi Tanzania na kuwakingia kifua mafisadi kila kukicha.

Kigumu chama cha mafisadi! Kigumu!
Mgumu fisadi Kibunango! Mgumu!

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~
Dk. Slaa amtumia makombora Mzindakaya

na Peter Nyanje, Dodoma na Irene Mark

MSEMAJI Mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, Dk. Willibrod Slaa, amemtumia makombora mazito Mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya (CCM), akimtuhumu kuwa ni miongoni mwa wabadhirifu wanaodaiwa kulisababisha taifa hasara ya sh bilioni 9.7.

Dk. Slaa, alisema Mzindakaya alisababisha hasara hiyo baada ya kushindwa kulipa mkopo kutoka Benki ya Standard Charted, uliokuwa umedhaminiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), shutuma ambazo Mzindakaya alizikanusha jana jioni, akisema hakudhaminiwa na BoT, bali Serikali Kuu ndiyo ilifanya hivyo.

Msemaji huyo wa kambi ya upinzani bungeni, alitoa makombora hayo jana wakati akijibu hotuba ya Waziri Mkuu kuhusu makadirio ya matumizi ya fedha katika ofisi yake na ile ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMA) kwa mwaka wa fedha 2007/08.

Alisema malipo ya mkopo huo yanatokana na mkopaji kushindwa kulipa deni na kwa mujibu wa sheria, mdhamini wake ambaye ni BoT kulazalimika kulipa fedha hizo. Mbali na Mzindakaya, makombora hayo pia alitupiwa Gavana wa BoT, Daudi Balali.

Alisema, utafiti wa kambi ya upinzani unaonyesha kuwa, mwaka 2004, Mzindakaya alichukua mkopo wa sh bilioni 9.7 kwa ajili ya shughuli zake binafsi kutoka Benki ya Standard Charter kupitia Kampuni ya SAAFI na kudhaminiwa na BoT ambapo Gavana wa BoT ndiye mhusika mkuu katika tuhuma hizo.

Dk. Slaa alibainisha kuwa, hivi sasa, baada ya miaka minne ya deni hilo kutolipwa, BoT kama mdhamini, imewajibika kuilipa Benki ya Standard Charter fedha zinazotokana na kodi za wananchi.

"Mheshimiwa Spika, fedha alizokopa mheshimiwa Mzindakaya miaka minne iliyopita, alitumia kwa maslahi binafsi, lakini sasa zinalipwa na wananchi kupitia kodi na tozo mbalimbali kwa vile benki hiyo ni mali ya taifa," alisema Dk. Slaa.

Aidha, alieleza faraja ya kambi ya upinzani baada ya Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, kukiri kufahamu taarifa iliyotolewa bungeni kuhusu ubadhirifu mkubwa ndani ya BoT unaomgusa gavana, wafanyabiashara wengine, akiwemo mbunge huyo (Mzindakaya) kupitia kampuni anayomiliki.

Wakati akijibu hoja za Waziri Mkuu, Dk. Slaa mara kwa mara alikuwa akikatishwa na baadhi ya wabunge waliokuwa wakitaka ufafanuzi wa masuala yaliyozungumza ama kuthibitisha kauli alizokuwa akitoa.

Waliomkatisha Dk. Slaa ni Spika wa Bunge, Samuel Sitta, Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na mbunge, George Simbamwene.

Spika Sitta, alimuonya mara mbili Dk. Slaa, akimtaka kurejea kujibu hoja iliyokuwa mbele yake na si kuzumgumza masuala mengine na iwapo angeendelea kufanya hivyo angemzuia kuendelea.

Wakati Dk. Slaa anaendelea kuchangia hoja, Mzindakaya alionekana akituma ‘vinoti' kwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Spika Sitta.

Baadaye, Spika alisema mbunge yeyote anaweza kutoa hoja kama ameguswa na suala lililozungumzwa na akasema kwamba Mzindakaya ameomba apewe dakika 15 kabla ya kuahirishwa kwa kikao cha bunge kutoa hoja binafsi.

Akiendelea kuchangia, Dk. Slaa, alisema wakati akichangia hoja ya BoT, Juni 20, mwaka huu, Mzindakaya alitoa tuhuma nzito dhidi ya wabunge kwamba wanatakiwa kufanya uchunguzi wa jambo watakalolisema bungeni na kwamba takwimu za kwenye mtandao (internet) zilizotolewa na Dk. Slaa, kuhusu taarifa za Benki Kuu hazina ushahidi, na si sahihi.

Dk. Slaa, alinukuu kauli ya Mzindakaya aliyotoa bungeni kuwa: "Kama kuna mambo mazito na ambayo mbunge angependa kuyasema, mimi nafikiri kuhutubia habari za Internet haitoshi kuwa ndio ushahidi sahihi, kwa sababu baadhi ya mambo tunayoyafahamu sisi wengine tumefayafanyia ‘research' (uchunguzi)… kwanza takwimu si sahihi.

"Takwimu sio dola milioni 200, ni dola milioni 131, ndio takwimu sahihi. Pili, baadhi ya wafanyabiashara wanaweza wakatumia ujanja wa kuwatumia wabunge waje wawasemee mambo yao au tofauti zao katika biashara. Na jambo hili linahitaji kuliangalia… bahati nzuri habari hii naijua kutoka kwa mhusika mwenyewe…" Mwisho wa kunukuu.

Dk. Slaa, alisema: "Mambo kadhaa yamejitokeza na kwa kuwa yamesemwa bungeni, basi ni vema nikayazungumzia pia bungeni… kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kifungu cha 49(7), mbunge hatakiwi kuzungumzia jambo lolote ambalo yeye mwenyewe ana maslahi ya kifedha nalo, isipokuwa baada ya kutaja jinsi anavyohusika, na kiwango cha maslahi hayo."

Alihoji sababu ya Mzindakaya, kujikanyaga pale anapokiri kuwa takwimu sahihi ni dola milioni 131 badala ya dola milioni 200 ambazo ailitaka serikali ithibitishe ukweli kuhusu ubadhirifu huo.

"Au Mheshimiwa Mzindakaya, anaona ni halali kuibwa kwa dola milioni 131 ila siyo dola milioni 200? Kama takwimu zake zinathibitisha upotevu huo, ni vipi Mzindakaya anayejulikana hodari wa kulipua mabomu hapa bungeni na mtetezi wa wanyonge, leo awageuke na kuwa msemaji wa serikali katika kumtetea Gavana wa BoT?

"Kwanini Mzindakaya hakutamka lolote kuhusu maslahi yake katika jambo hili? Amekiuka kanuni ya bunge," alisema.

Aliongeza kwamba, Mzindakaya ameomba mkopo mwingine wa sh bilioni mbili (hakutaja kutoka benki gani), lakini ameomba kudhaminiwa na BoT na kusema kuwa, mkopo huo upo kwenye hatua ya kujadiliwa.

Alisema, hatua ya kujadiliwa kwa ombi la Mzindakaya kunatoa nafasi kwa BoT ama kuidhinisha udhamini wake ama la.

"Mheshimiwa Spika, hapa ieleweke kuwa hatuzungumzii uhalali au vinginevyo wa mkopo wa Mheshimiwa Mzindakaya… tunazungumzia kukiukwa kwa kanuni ya Bunge na dhana anayotaka kujenga Mzindakaya, dhidi ya baadhi ya wabunge kwa wananchi, yote haya ni mambo mazito sana," alisema Dk. Slaa.

Kauli ya Mzindakaya ilielekezwa kwa Dk. Slaa, kwa kuwa alinukuu taarifa ya Internet wakati akizungumza bungeni mwishoni mwa wiki na kwamba tafsiri ya Mzindakaya, inatoa dhana kuwa baadhi ya wabunge hawafanyi uchunguzi.

"Tafsiri ya Mzindakaya, inamaanisha kuwa baadhi ya wabunge ikiwemo mimi hatufanyi ‘research' (utafiti) ila yeye tu ndiye anayefanya ‘research'. Hili ni tusi kwa Bunge na Watanzania waliotutuma tuwasemee, pia analenga kuupotosha umma kuwa, kuna wabunge wanaokurupuka na kusema mambo bila kufanyia utafiti.

"…Mheshimiwa Mzindakaya hajaeleza kwanini awe na mawazo hayo potofu, au kwa vile yeye ni tajiri na sisi wengine anadhani ni malofa, hivyo ni rahisi kuhongwa na kununuliwa?" alihoji Dk. Slaa na kuongeza.

"Lakini hata yeye utajiri mbona kaupata kwa fedha alizokopa kwa dhamana ya BoT, ambazo Watanzania wote matajiri na maskini sasa wanazilipa kwa kodi yao kupitia BoT?

"Tukisema Mzindakaya anasukumwa na fadhila aliyopewa na gavana kwa kumdhamini mkopo wake wa zaidi ya sh bilioni 9 na kulipiwa deni hilo halafu anataka gavana huyo huyo amdhamini tena mkopo wa sh bilioni mbili nyingine tutakuwa tumekosea?

"Kwa niaba ya kambi ya upinzani, nawaachia wananchi kutoa hukumu ya nani hafanyi utafiti kati yetu sisi na Mzindakaya anayelenga kuficha uozo wa ndani ya Benki Kuu… uzalendo hauna gharama, unahitaji dhamira safi," alisema Dk. Slaa.

Alizungumzia pia suala la Kampuni ya Kagoda Agricultural Ltd, iliyosajiliwa Septemba 29, mwaka 2005 ambayo katika kipindi cha wiki nane ilipata fedha zaidi ya sh bilioni 30.8 kupitia External Service Debt Account na Benki Kuu, ambayo gavana ndiye msimamizi mkuu.

Alisema, taarifa hiyo inaonyesha kuwa mikataba tisa ilisainiwa kati ya Oktoba 18 na 19 mwaka 2005 na makampuni 12 ya nje chini ya mkataba na Kampuni ya Kagoda.

Aliongeza kuwa, ipo haja ya kufahamu undani wa kampuni hiyo na iwapo wamiliki wake waliorodheshwa kwenye daftari la BRELA, ama kuna vigogo nyuma yake.

Aidha, amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete, katika kukabiliana na watumishi wabadhirifu, ili kupambana na vitendo vya rushwa.

Alisema, maswala hayo ni muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu, na hivyo kambi ya upinzani inapenda kupata majibu ya kina na si majibu ya kisiasa ambayo hayana manufaa kwa taifa.
 
Sasa kama mheshimiwa raisi naye ana fikra za namna hii, kuna uongozi kweli???????????? What is ths wivu na chuki??? halafu watanzania tutegemee mabadiliko, maendeleo kutoka viongozi wa namna hiiii!!!!!!!!!!!!
Nyambala,'
Hata sishangai. Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa alipokuwa anaapisha baraza lake la kwanza la mawaziri aliwaambia huu ndio wakati wenu wa kula.
 
on the other hand pia inasikitisha sana kwa sababu mnaumbuka kwa ghrama ya migongo ya umasikini wa wanachi walalahoi!

Salim alipenda kusema ni Wavuja jasho... hiyo hapo juu ni ya Mtikila. Hii ni heshima yake kwa wale wanaohangaika katika Taifa hili, na sio kebehi kwao kama Mtikila alivyowatambua. Itachukua muda mrefu kutenganisha wehu katika nchi hii!
 
...Weye mwenye hiyo bendera inayonuka uchafu mwingi bora ufunge domo lako ! Kwani ni uongo huyo mzee mchovu hakupewa mkopo kinyemela, na vipi ule mradi hewa wa kusindika nyama za nzi...?

Si amepora mashamba ya wananchi kule kwao.....!! Na kule Kigoma je ? Acha hizo wewe mshamba usiyejua lolote !! Huyu mzee choka ile mbaya, na sasa anatafuta sababu za kijinga ili aendelee kuganga njaa....maana kila mtu alishamshiti- alihongwa wakati ule akijifanya mzee wa mabomu..!. Muulize hata mwanaye Simon atakupa ukweli jinsi huyu alivyoishiwa, na hata zile dili zake za usangoma hazina nguvu tena ! Kama ni kuruka kwa nyungo, wapo wakali wengine siku hizi.....
 
Mi naona mambo haya ya ufisadi msiyaandike humu tena, nikiangalia wanangu wakaribia kwenda shule sina hata senti, halafu mnaniambia watu wameiba pesa na hawajafanywa chochote, naumia sana.
 
Inashangaza sana akiguswa fisadi la ssm tu utaona jinsi wanassm wa hapa forum wanavyomtetea. Yaani kuna mtu ataniambia kuwa Mzindakaya si fisadi?? Mzindakaya ni fisadi la kutosha na la nguvu kabisa!! Facts zipo!!! Tafuta riport ya PCB enzi hizo na lile deni la kiini macho kule BOT!!!

Kingine ni hovyo si mtendaji, amekuwa katika ubunge kabla hata sijajliwa mtoto, na leo nina wajukuu hakuna kitu cha maana amefanya Bungeni kwake zaidi ya kuwatishia watu wanaotaka kiti chake!!!!! Anawatishia kwa njia gani!!! Jibu kapuni.!!!!

Jamani tuweke itikadi pembeni tuwe wakweli na si kutetea hata uozo. Rafiki mzuri ni yule anayeona ukweli na kuukemea. Hebu nyie wanassm oneni ukweli na mkosoane na mambo yatakuwa shwari. Yaani utaona mtu kama makamba anaropoka mbele ya vyombo vya habari upupu tu eti anatetea chama. Utafikiri speed governor za ubongo zimekatika!!!! Kulaleki.
 
...Weye mwenye hiyo bendera inayonuka uchafu mwingi bora ufunge domo lako ! Kwani ni uongo huyo mzee mchovu hakupewa mkopo kinyemela, na vipi ule mradi hewa wa kusindika nyama za nzi...?

Si amepora mashamba ya wananchi kule kwao.....!! Na kule Kigoma je ? Acha hizo wewe mshamba usiyejua lolote !! Huyu mzee choka ile mbaya, na sasa anatafuta sababu za kijinga ili aendelee kuganga njaa....maana kila mtu alishamshiti- alihongwa wakati ule akijifanya mzee wa mabomu..!. Muulize hata mwanaye Simon atakupa ukweli jinsi huyu alivyoishiwa, na hata zile dili zake za usangoma hazina nguvu tena ! Kama ni kuruka kwa nyungo, wapo wakali wengine siku hizi.....

Safi sana mkuu Mafuluto. Yaani umenena vilivyo. Nilitaka kuzungumzia habari zake za tungulu nikapata kigugumizi kidogo. Thenkiyuuuuuuuu. Na nimekupatia hapo juu "thanks".
 
Arudishe feza yetu aliyochotewa BOT, aah wanaudhi kweli hawa, sasa anaona bora ajipendekez pendekez tu
 
Inashangaza sana akiguswa fisadi la ssm tu utaona jinsi wanassm wa hapa forum wanavyomtetea. Yaani kuna mtu ataniambia kuwa Mzindakaya si fisadi?? Mzindakaya ni fisadi la kutosha na la nguvu kabisa!! Facts zipo!!! Tafuta riport ya PCB enzi hizo na lile deni la kiini macho kule BOT!!!

Kingine ni hovyo si mtendaji, amekuwa katika ubunge kabla hata sijajliwa mtoto, na leo nina wajukuu hakuna kitu cha maana amefanya Bungeni kwake zaidi ya kuwatishia watu wanaotaka kiti chake!!!!! Anawatishia kwa njia gani!!! Jibu kapuni.!!!!

Jamani tuweke itikadi pembeni tuwe wakweli na si kutetea hata uozo. Rafiki mzuri ni yule anayeona ukweli na kuukemea. Hebu nyie wanassm oneni ukweli na mkosoane na mambo yatakuwa shwari. Yaani utaona mtu kama makamba anaropoka mbele ya vyombo vya habari upupu tu eti anatetea chama. Utafikiri speed governor za ubongo zimekatika!!!! Kulaleki.
hapo umenena,,mzinakaya ni fisadi mkubwa sana mimi namjua fika tunakaa jirani ufipa amepora maelfu ya maekari ya ardhi rukwa na kigoma kawanyanganya wanyonge ardhi zao,pia katika katavi national park ana maeneo ya game reserve analeta wazungu wanajizolea rasilimali zetu mwisho atatumalizia wanyama wetu,katavi kuna maovu makubwa yanafanyika kushinda hata huko loliondo mnapopapigia kelele kila siku,nendeni mpanda mkajionee wasivyofaidika na rasilimali zao,inauma sana.
 
...Weye mwenye hiyo bendera inayonuka uchafu mwingi bora ufunge domo lako ! Kwani ni uongo huyo mzee mchovu hakupewa mkopo kinyemela, na vipi ule mradi hewa wa kusindika nyama za nzi...?

Si amepora mashamba ya wananchi kule kwao.....!! Na kule Kigoma je ? Acha hizo wewe mshamba usiyejua lolote !! Huyu mzee choka ile mbaya, na sasa anatafuta sababu za kijinga ili aendelee kuganga njaa....maana kila mtu alishamshiti- alihongwa wakati ule akijifanya mzee wa mabomu..!. Muulize hata mwanaye Simon atakupa ukweli jinsi huyu alivyoishiwa, na hata zile dili zake za usangoma hazina nguvu tena ! Kama ni kuruka kwa nyungo, wapo wakali wengine siku hizi.....
Umenena kweli mkuu, hata mabomu aliyokua akifyatua ilikua kwa maslahi binafsi. Watu walikua wakimtumia kudefend madhambi yao au kuwaumbua wenzao kwa kumpa hongo akaropoke kwa sababu upstairs hamnazo.
 
When I have laid the land most desolate because of all their abominations which they have committed.

Mene mene tekel !!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom