Fisadi Mkuu wa Richmond yuko CHADEMA au yuko CCM?

Fisadi Mkuu wa Richmond yuko CHADEMA au yuko CCM?

hivi nani ambaye angeguswa/angetajwa na ripoti ya richmond serikali ingeanguka/kurudi kwenye uchaguzi mkuu?Jibu la hapa ndio bwana la mafisadi nchini
 
Jibu raisi sana,wala huitaji kufikiri,ata mtoto wa la pili anajua,hata mama ntilie na boda boda wanajua,NI LOWASA ambaye yupo Chadema

sijui unajitambua au ushabiki tu, yaana lowassa yupo juu ya sheria mpaka serkali inamuogopa?
 
Acheni woga! Lissu alishasema anayehusika na Ritchmod ni Jakaya Mrisho Kikwete!!
 
utata uko wapi wakati fisadi papa ni Lowasa kila mtu anajua bayana kuwa Lowasa ndiyo mwamba wa ufisadi.

Kila mtu nani nani na nani waorodheshe hapa. Acha kujitoa ufaham huyo bibi yako kijijini anajua lowasa richmond haimhusu.
 
Jiulize, kwa nini SiSiEm kwenye kampeni zao wanatumia neno FISADI, lakini kamwe hawatumii neno RICHMOND?
 
Tatizo Letu watanzania hatupendi kujiongeza...

-uchunguzi unaonyesha katika utumishi wa JK miaka mitano (5) alikuwa yupo nje ya nchi kutafuta wawekezaji na mingine ameitumia akiwa ndani ya nchi.
--swali ni wawekezaji gani hao aliokuwa anawatafuta?
^^jibu hapa ni kwamba alikuwa anajitengenezea dili za maana (RICHMOND, DOWANS na IPTL ESCROW )
^^^JK ndio richmond na richmond ndio JK. Wawekezaji wote aliowaleta wamekua chachu ya umaskini hapa nchini.
^^lowassa Alikuwa mbuzi wa kafara, hakuwa na namna ya kupingana na mamlaka za juu
>>funika kombe mwanaharamu apite..
 
Habari Wakuu?

Bado kuna utata uliojificha kuhusu nani aliruhusu kupitishwa/kusainiwa Mkataba mbovu wa Kampuni ya Kuzalisha umeme ya Richmond.
Kitendawili hiki tulitegemea kuwa kitateguliwa msimu huu wa kueleka Uchaguzi Mkuu 25-Oct-2015 hasa baada ya Lowassa kuihama CCM na kupewa ridhaa ya kugombea Urais kupitia Chadema/UKAWA.

Mpaka sasa haijafahamika ni nani alikuwa Mmiliki halali wa hii Kampuni kwa kutajwa jina bali imebakia kuwa mafumbo, mmoja akisema Mamlaka ya juu ndiyo yaliyoruhusu na mwingine akisema ni yule anayeongozana na Lissu kwenye Mikutano ya Kampeini huku wote wakikwepa kutaja majina.

Swali la kujiuliza, je,

1. Hawa watu wanajuana na wameamua kulindana?
2. Walishirikiana kwenye huu ufisadi?

Ipo wazi tu bosi wa richmond ni yule aliyejiuzuru. Eti alijuuzuru kulinda heshima tangu lini fisadi likawa na huruma na kwanini lowasa anaongea ujinga wakati alipojiuzuru hakusema na amesubiri mpaka amekatwa ccm ndio anabwabwaja utumbo. Tumeshaamua Tunamtaka Magufuri tu aje awanyooshe majizi na yatatajana yooye.
 
angekuwa hayupo ndani ya system ya chama dola(huyo muhusika wa Richmond) angekwisha pelekwa mahala stahiki, lakini ukiona linautata mpaka leo na mkuu ametajwa na hakuna hata aliye fikishwa kwa mashtaka, ujue mmmhh hapo pana mnuso wa mkuu, mana mbona upande wa chadema viongozi washapelekwa sana mahakamani kwa vikesi visivyo na msingi?
 
Huwezi kuwa serious kama unashindwa kuunganisha dot hapo.Mkuu alimuamini Lissu akamwambia amtaje na Lissu akamtaja na hakuna aliyetajwa hajabishwa sasa maswali ya nini tena?kama kuna cha kufanywa Mmiliki wa richmond.Rais ana nguvu ampeleke mahakamani basi nchi ipate haki yake.
 
Mbona hili liko wazi? EL alishasema kwenye moja ya vikao vya NEC ya CCM kwamba alitaka kuvunja mkataba lakini maagizo kutoka juu yalikataza hilo lisifanyike. Hilo alilisema akimwambia Mwenyekiti wake mbele ya kadamnasi ya wajumbe wa NEC. Mwenyekiti hakupinga tamko hili. Hili jambo liko wazi kabisa.
 
angekuwa hayupo ndani ya system ya chama dola angekwisha pelekwa mahala stahiki, lakini ukiona linautata mpaka leo na mkuu ametajwa na hakuna hata aliye fikishwa kwa mashtaka, ujue mmmhh hapo pana mnuso wa mkuu, mana mbona upande wa chadema viongozi washapelekwa sana mahakamani kwa vikesi visivyo na msingi?

Alikula shilingi ngapi vile?
 
kwa mawazo yetu sisi kina gogo la shamba kwamba mwenye hilo dili ni mkuu wa nchi ndio maana kila mtu anaogopa kumtaja lakini ingekuwa ni ni mtu wa kawaida angeshatajwa
Kwa hali ilivyo ufisadi wa richmond cha mtoto, kuna hii kitu ya kinyelezi. Eti mtambo kwa kuchakata gesi ni wa mtu binafsi! Gesi ya mtwara pia ni mtu binafsi, serikali itaambulia kodi tu! Wajameni TZ yetu.
 
Huwezi kuwatofautisha, Lowassa, Kikwete, Kingunge, Sumaye, Magufuli na CCM.!
 
Sasa hivi mambo ya kutuambia mtu fisadi halafu baadaye ndiyo mnakuja kutuletea na kutuambia ndiye ataleta mabadiliko mtu huyohuyo,mi nafikiri wananchi wanaojitambua hawatofanyiwa upumbavu tena.

Kaiba sh ngapi?
 
Sasa hivi mambo ya kutuambia mtu fisadi halafu baadaye ndiyo mnakuja kutuletea na kutuambia ndiye ataleta mabadiliko mtu huyohuyo,mi nafikiri wananchi wanaojitambua hawatofanyiwa upumbavu tena.

Lowassa sio chaguo la slaa au mbowe au chadema, wanasiasa kugeukana ni kawaida sana. Lakini huyu ni chaguo letu sisi tusio na vyama
 
Back
Top Bottom