Fisadi Benjamin Mkapa yuko na fisadi Edward Lowassa

Fisadi Benjamin Mkapa yuko na fisadi Edward Lowassa

Rev. Mtikila

R I P
Joined
Dec 1, 2008
Posts
3
Reaction score
34
Salaam Wana wa Tanganyika'
ILI UCHAGUZI MKUU UIOKOE NCHI YETU

Marufuku aliye na doa la ufisadi kujihusisha!
04/7/2015

FISADI BENJAMIN MKAPA YUKO NA FISADI EDWARD LOWASA


Tunanena kwa ushujaa kuhusu uokoaji wa Nchi yetu katika uchaguzi mkuu huu, tukikumbuka jinsi Mungu alivyoruhusu maangamizo ya utawala wote wa Ghana, yaani Rais Kutu Acheampong na vigogo zaidi ya 300 chini yake, kwani wengi wamepokea unabii kwamba yale yalikuwa mawingu tu, mvua yenyewe itanyesha katika nchi hii!

Uchunguzi wetu umebaini kwamba Fisadi Benjamin Mkapa, ambaye mwaka 2005 aliizimisha kikatili kamati ya maadili ya CCM, na kutumia ubabe wake kumpa Urais Jakaya Kikwete, kufuatia ushenga mzito wa mafisadi Rostam Aziz na Edward Lowasa, katika Uchaguzi Mkuu huu Fisadi Ben Mkapa anataka kushawishi uongozi wa chama chao kwamba utumike ubabe ule alioutumia yeye kumpa Urais fisadi Edward Lowasa!

Fisadi mwenza Rostam Aziz ambaye ni Mwajemi wa Jamhuri ya Kiislamm ya Iran, alihusika na kufilisi bila huruma shirika la Taifa la viwanda vya ngozi, kufilisi mradi mkubwa wa kilimo uliokuwa umeanzishwa Rufiji kwa msaada wa Serikali ya kwao Iran ukawa mtaji wake wa kuunda kampuni yake ya Caspian, akapenyeza mkono wake katika uporaji wa hazina ya madini ya Taifa letu.

Fisadi Rostam Aziz alishirikiana na fisadi Edward Lowasa kulifilisi Taifa letu kwa kampuni feki ya Richmond, na baadaye akalifilisi Taifa letu dola za Marekani zaidi ya 100 milioni kwa kampuni ya Dowans.

Mafisadi Edward Lowasa na Rostam walilifilisi Taifa mamia ya mamilioni ya dola za Marekami, kwa kutumia kampunio ya Vodacom. Fisadi Rostam Aziz alihusika hata katika kuua Shirika letu la Reli, na ndiye anayetuhumiwa kuleta vichwa 54 vya treni, kisha akavivushia Kenya, ili ikitimia ndoto ya urais wa Lowasa avirudishe na hata walitie mfukoni Shirika lote la Reli,

Fisadi Mkapa siyo tu alibariki uporaji wa Taifa letu wote huu wa mafisadi wenzake Edward Lowasa na Rostam Aziz, bali na yeye mwenyewe binafsi ndiye aliyewapokonya Watanganyika Benki yao maarufu (NationalBank of Commerce) akawapatia bure Makaburu, kwa maslahi yake binafsi! Saa ya ukombozi ni sasa!

Fisadi Mkapa ndiye aliyevunja Katiba ya Nchi Ibara ya 27 kwa kulifilisi Taifa letu mashirika yote 433 ya Umma, yaliyotoa ajira zaidi ya milioni sita wakiwa ni pamoja na wazalishaji wa mali ghafi na chakula kwa kilimo na fani zingine, watoaji wa huduma zote muhimu na mahitaji kwa wafanyakazi na jamii zao n.k mitambo ya thamani ya mabilioni ya fedha za kigeni ikang'olewa na kuuzwa nje na magabacholi. Kwa uharamia huu wa fisadi Ben Mkapa ajira nchini ilifutika, kwa kuuawa mashirika ya Umma, na kuuawa uzalishaji na hasa kilimo.

Fisadi Mkapa ndiye aliyelitendea Taifa letu ufisadi wa kipekee na wa kihistoria wa kupora majumba yote ya Serikali, akajigawia yeye na familia yake, akawapa na mafisadi wenzake, wakagawana majumba ya Serikali ya Wana wa Tanganyika! Kwavile Mkapa si Mtanganyika bali ni Mmeto wa Msumbiji, hawezi kuwa na uchungu na nchi yetu, kwa sababu uhanga kwa ajili ya utaifa wa mtu ni maumbile ya Mwenyezi Mungu! Saa ya ukombozi ni sasa!

Fisadi Mkapa ndiye aliyeanza kuitumia Ikulu ya Nchi yetu kwa madili ya biashara, mpaka kujibinafsishia migodi kama Kiwira, na kuwapa Makaburu na magabacholi wengine hazina ya madini ya Taifa letu, akaanzisha hata benki, akawapa ruksa familia yake kujitajirisha kwa kuitumia vibaya sana dhamana aliyopewa yeye na Taifa!.

Fisadi Benjamin Mkapa ndiye aliyevunja Katiba ya Nchi yetu Ibara ya 26, Ibara ya 27 na Ibara ya 19 kwa kupokonya Chuo Kikuu cha TANESCO kilichokuwa kikizalisha wataalamu wetu wenyewe wa nishati, akawapa Waislam! Ndipo akaletwa Makaburu waliolifilisi shirika, pamoja na mafisadi wa CCM wa IPTL, SONGAS, RICHMOND ya fisadi Edward Lowasa n.k. Ndiyo maana hatuwezi kumshangaa fisadi Benjamin Mkapa leo akimpigia debe fisadi Edward Lowasa.

Fisadi Mkapa aliwapa Waislamu Chuo Kikuu cha TANESCO bure, lakini Wakatoliki akawakamua mabilioni ya fedha kwa ajili ya Chuo cha Benki cha Amon Nsekela Iringa, na Waluteri wakagharamia wenyewe Tumaini University na Waanglikana Saint John's University. Kwa uovu huu siyo tu alivunja Ibara za 26, 27 na 19 za Katiba ya Nchi, bali na Ibara ya 13 inayompiga marufuku ubaguzi au upendeleo.

Watanganyika wenye uchungu na Nchi yao wanaandaa Kesi nzito za kulirudishia Taifa lao Chuo cha TANESCO, mali zote za Shirika la Simu (TTCL), majumba yote ya Serikali yaliyofiusadiwa, na mashirika mengine muhimu ya Umma. Saa ya ukombozi ni sasa!

Fisadi Mkapa ndiye ambaye baada ya kuimaliza nchi yetu kiasi hiki alikabidhi urais kwa ubabe kwa Jakaya Kikwete, kwa ushawishi wa mafisadi Rostam Aziz na Edward Lowasa, kwavile kamati ya maadili ya chama chao isingempitisha. Kwani alikuwa amekataliwa hata na Mwalimu Nyerere kwamba hafai kabisa kuwa rais, kwa kutokuwa na hekima na mzigo wa kizalendo juu ya Nchi, kama alivyomkatalia hata Edward Lowasa kwa kuwa fisadi papa.

Mwalimu Nyerere alimpigia kampeni fisadi Benjamin Mkapa nchi nzima awe Rais baada ya Ali Hassan Mwinyi, kwa sababu hakumjua vizuri ingawa alikuwa mwanafunzi wake Saint Francis College Pugu. Mkapa alithibitika kuwa kinyume kabisa na mwalimu wake kiitikadi na kimaadili!

Hatukumbuki kumsikia fisadi Benjamin Mkapa akijitetea baada ya kutuhumiwa na baadhi ya wana familia wa hayati Mwalimu Nyerere kuhusika na kifo chake. Wala hatupendi kuamini kwamba vifo vya kutatanisha vya marehemu Amrani Kombe aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa na marehemu Horace Kolimba aliyehojiwa mpaka akafa kwa kusema "CCM haina dira, imepoteza mwelekeo" vilitokana na ukatili wake yeye Mkapa.

Lakini yale mauaji na unyama waliofanyiwa Wazanzibari mwaka 2001 kwa amri yake ni ukatili ambao sasa muda muafaka wa kumfikisha Mahakama ya Dunia The Hague.

Watanganyika wanahitaji Rais mwenye sifa zile alizotuagiza Mwenyezi Mungu katika Kumbukumbu la Torati 17:15-20.

Mungu Ibariki Tanganyika. DEMOCTRATIC PARTY (DP)


Mchungaji C. Mtikila MWENYEKITI-TAIFA
 

Attachments

Kwani ccm kuna ambaye siyo fisadi?mamvi atakufa kwa presha
 
Mchungaji asante kwa taarifa, ninakujua na ninakuamini kwa ujasiri na umahiri wako wa kufungua kesi mahakamani na kushinda.

Tumeshindwa kupata katiba mpya, kwa katiba tuliyonayo (1977), hatuwezi kuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki. Tunahitaji tume huru ya uchaguzi lakini tunahitaji pia demokrasia pana zaidi kwa kuwa na mgombea binafsi.

Nikuombe tafadhali uiombe mahakama itusaidie kutatua mgogoro wa mgombea binafsi na tume huru ya uchaguzi, wabunge wetu wametuangusha, wananchi hatuna imani na tume iliyopo. Mgombea binafsi angepunguza minyukano pia ndani ya vyama ambayo inatishia hata amani ya taifa hili.
 
Naona Rev.Mtikila umeamua kuja kwa kasi humu JF, vipi tuambie pia upo kambi ipi ya wanaCCM?
 
Mtikila katika ubora wake.karibu sana jf
 
Pelekeni Lowassa jera ili mliponye taifa letu maana genge la walanguzi linamtumia kufikia malengo yao,
 
Kumbe Mkapa nae ni mshezi huyo upande wa wezi wakati kuna vijana wake walimsaidi katika kipindi chake vizuri lakini hawaoni kama wanamaana bali anaungana na wezi ,
 
Kumbe anataka waigie wezi ili wasiwe na nguvu ya kufatilia issue yake ya Kiwira.
 
Back
Top Bottom