Ninachukulia kama umeishi huko miaka mingi?
Je unajihisi mgeni(imposter syndrome) mpaka hivi leo? Unapakumbuka nyumbani? Kuna ubaguzi wowote unapata kama mhamiaji?
New York City pamekuwa nyumbani sasa. Takriban miaka 30 sasa. Nimesoma, nimenunua nyumba, nimeanza maisha, mpaka move to suburbs na naelekea kustaafu niko viunga vyake.
Najihisi mgeni?
New York City kuna wageni wengi sana, wa kutoka kila kona ya dunia, kiasi kuwa mgeni si ajabu. Meya wa sasa Mamdani ni muhindi kazaliwa Kampala Uganda.
Ugeni uliniisha nilipoanza kuwaelekeza watu njia. Hata mwaka mmoja ulikuwa haujafika tangu nilipoingia.
Nyumbani napakumbuka. Lakini nikija huko najiona mgeni pia, rafiki zangu wengi wametawanyika. Upanga na Oysterbay, mitaa yangu ya miaka ya 1980s na 1990s mwanzoni si sawa na leo.
Nyumbani kila nikitaka kurudi naahirisha sasa miaka 14 sijarudi.
Na October 29 2025 ndoyo kabisa imenifanya nione sijakosea kutokuwa na tamaa sana ya kurudi hata likizo.
Tatizo lingine ni kwamba wazazi wangu wanakuja huku karibu kila mwaka, inapunguza sababu za kurudi nyumbani.
Kuhusu ubaguzi.
Ubaguzi unapigwa vita sana na ni tusi kubwa sana mtu akiambiwa mbaguzi, ni vigumu kuukuta wa wazi ingawa wa chinichini kuuondoa kabisa ni vigumu, lakini New York City, by virtue of its population and bihgest city nature, is probably one of the least racist place in the US.
New York City ni mjinwa kimataifa, nimepata nafasi za kuongoza projects za kimataifa bila kubagukiwa, bila ya kuwa na godfather, kwa uwezo wangu tu watu wameangalia CV wakanipa kazi. Kwa namna ambayo hata Tanzania pengine ningeweza kubagukiwa zaidi ya New York City.