Dah! We jamaa umenikumbusha mtoto Juliana aiseeee!!! Ndiye alinitoa tongotongo kuhusu mapenzi na mie ndie nilkata utepe mwanawani si mchezo acha za siku hizi za Kichina hata damu huioni!!!!
Pili, nikiwa nimeanza kazi baada ya kutoka chuo nilifall kwa binti mmoja hivi (jina kapuni), nilimpenda vibaya!!! Nikatangaza ndoa kumbe mwenzangu ananing`ong`a aiseee sitakaa nisahau. Nikampeleka home wakamtambua na home wakaanza kujipanga kwenda kwao kutoa posa, ndo hapo binti alianza mauza uza. Mara hivi mara vile, wasiende kwanza mi bado mdogo, mila za kwetu mpaka dada yangu aolewe kwanza na visa kibaooo!! Nilikoma aliponionyesha live ana mwanaume mwingine, sikutaka mapambano ila nilimfata mbele ya jamaa yake na kumuuliza nini msimamo wake akanijibu 'sikutaki' tena kwa jeuri kubwa!! Mzee nikasepa, nililia sana chumbani kwangu siku hiyo sitasahau ila baada ya hapo machungu yakaisha na maisha yakasonga.
Baada ya miaka mitatu alifanyiwa na mwanaume kama alivyonifanyia mimi, yaani jamaa lilijidai linamuoa likatoa mpaka mahari halafu likaoa demu mwingine ghafla!! Alidata serious, baada ya hapo akaanza kunitafuta nimsamehe ili turudiane keshajifunza na kutuma mpaka ndugu zake kwangu. Unajua ni nini? Sikuwa na mpango wa kuoa wakati huo, ila niliamua kuoa haraka haraka tena ndoa ya kifahari mbaya!!! Mpaka leo anajaribu kuivunja ndoa yangu aingie yeye coz anadai haoni mwanaume mwingine zaidi yangu ila kachemsha!!! Maisha yanamuona vibaya, umri unasonga, kazi hakuna, yaani anatia huruma but aliyataka nimsaidieje sasa???
Hayo ndo maisha ya mapenzi tunayopitia mpaka kufikia kutulia