I miss you mahabuba

Al-Hadidy

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
1,404
3,063
Nakumbuka ilikuwa kipindi naenda kuanza high school Usagara wakati jk ndo anamalizia madaraka nilikuwa mimi na kitabu tu then nilikuwa katika vitu ambavyo haviniingii akilini ilikuwa ni wasichana.Nilikuwa sina hisia nao kali halafu nilikuwa nina aibu sana kwao,hii ilitokana na malezi ya nyumbani ya kidini kwa sana na kukatazwa kutoka nje labda iwe shule na sehemu ya ibada.

Kuna msichana mmoja hivi siku nafika class tulipangwa nae kukaa sehemu moja,she was so beautiful aliumbika kama mnavyojua watoto wa kitanga si haba ndani ya wiki ya kwanza nilikaa naye lakini unbelievably sikuongea nae chochote zaidi ya salamu ambayo alikuwa ananianza yeye one day uvumilivu ukamshinda,ile naingia class nakaa zangu mtoto kanisalimia kwa tabasamu tamu then akaniambia "halafu we kaka kwani huongeagi?.Nikamjibu " huwa siongei hadi niongeleshwe au niulizwe!",jibu langu lilimfurahisha sana.

Urafiki wetu ulianzia hapo ikawa kila sehemu shuleni tupo wote nikatokea kumzoea sana hadi home tukawa tunarudi naye then kumbe kimaajabu tunaishi jirani daaah!!!Alikuwa sometimes anakuja home tunajisomea hadi wazazi wakamzoea pia alikuwa na tabia njema wakampenda sana likizo ya December ilitutenganisha kidogo kwa kuwa alienda Dar kwa ndugu yake,January aliporudi tulionana skonga sio siri alifurahi alinikumbatia kwa muda mrefu na vicheko hadi wanafunzi wengine wakajua kuna kitu hapa sio bure.


Lile kumbatio lilinibadili hisia,moyo ulikuwa unadunda sana hadi usingizi nilikosa usiku nikatokea kumpenda sana na kumwambia nilikuwa nashindwa weekend ijumaa nikampigia simu night tukawa tunataniana nikamwambia 'kuna kitu nataka kukwambia' akajibu 'nambie tu'.Nikajifikiria nikamuuliza tena "hutokasirika?" ,akasema "inategemeana ila we sema tu"
Nikamwambia "nakupenda" akasema nirudie tena nikamwambia tena "I love you". Akakata simu nikawa nikipiga haipatikana Mara hapokei sio siri nikakujutia roho yangu.

Kesho yake asubuhi alikuja hadi home akiwa anaonekana hayupo sawa nikawa najaribu kujichetua ili hata afurahi lakini wapi.
Nikamuomba radhi kama neno lile lilimuudhi akadai nisijali sana,akaanza kunifungukia bwana kumbe anipenda pia alikuwa anafikiria,niliruka kwa furaha mapenzi yetu yalianzia hapo na hakuna aliyemtia stress mwenzake,she was my first love alinifundisha nini mapenzi na kila kitu alikuwa fundi kitandani sitamsahau.


Tulienda hadi tunakaribia kumaliza form six siku ya sherehe mambo yaliharibika,kumbe mzee wangu na baba wa demu wangu walikuwa na mabifu ya kibiashara kitambo na kuna vitu washawahi kufanyiana demu wangu alipandikizwa maneno na mzee wake hadi akatokea kunichukia Mimi na mzee wangu na inavyosemekana dingi ashawahi kusababisha kifo cha mama yake wa laaziz wangu.

Binafsi hata mzee nikimuuliza habari hizo hataki kunijibu anajibu wa mkato kuna kitu ananificha niliumia sana hata mtihani nilifanya kwa stress nilifaulu kwa uwezo wa mola mpenzi wangu akawa hanitaki tena,nikaenda jeshini miezi mitatu kurudi alishaondoka walihama na baba yake na sijui walihamia mkoa gani au nchi gani.

Wewe msichana kama upo humu jf jaribu kurudisha moyo wako nyuma,ugomvi wa wazazi wetu sisi hautuhusu I'm still in love with you!!!
Hata kama upoJupiter rudi mara moja nimemiss tabasamu lako na joto lako pia.Niliwahi kuapa sitatoa chozi for the sake of love lakini yanatoka mengi oh my god!!!!

I MISS YOU LAAZIZ!!!!



SAMAHANI KWA STORY NDEFU SIKUTAKA KUACHA KITU
 
Nakumbuka ilikuwa kipindi naenda kuanza high school Usagara wakati jk ndo anamalizia madaraka.
Nilikuwa Mimi na kitabu tu then nilikuwa katika vitu ambavyo haviniingii akilini ilikuwa ni wasichana.Nilikuwa sina hisia nao kali halafu nilikuwa nna aibu sana kwao,hii ilitokana na malezi ya nyumbani ya kidini kwa sana na kukatazwa kutoka nje labda iwe shule na sehemu ya ibada.
Kuna msichana mmoja hv siku nafika class tulipangwa nae kukaa sehemu moja,she was so beautiful aliumbika kama mnavyojua watoto wa kitanga si haba.
Ndani ya wiki ya kwanza nilikaa naye lakini unbelievably sikuongea nae chochote zaidi ya salamu ambayo alikuwa ananianza yeye.
One day uvumilivu ukamshinda,ile naingia class nakaa zangu mtoto kanisalimia kwa tabasamu tamu then akaniambia "halafu we kaka kwani huongeagi?.Nikamjibu " huwa siongei hadi niongeleshwe au niulizwe!",jibu langu lilimfurahisha sana.

Urafiki wetu ulianzia hapo ikawa kila sehemu shuleni tupo wote nikatokea kumzoea sana hadi home tukawa tunarudi naye then kumbe kimaajabu tunaishi jirani daaah!!!Alikuwa sometimes anakuja home tunajisomea hadi wazazi wakamzoea pia alikuwa na tabia njema wakampenda sana.
Likizo ya December ilitutenganisha kidogo kwa kuwa alienda Dar kwa ndugu yake,January aliporudi tulionana skonga sio siri alifurahi alinikumbatia kwa muda mrefu na vicheko hadi wanafunzi wengine wakajua kuna kitu hapa sio bure.


Lile kumbatio lilinibadili hisia,moyo ulikuwa unadunda sana hadi usingizi nilikosa usiku nikatokea kumpenda sana na kumwambia nilikuwa nashindwa.
Weekend ijumaa nikampigia simu night tukawa tunataniana nikamwambia 'kuna kitu nataka kukwambia' akajibu 'nambie tu'.Nikajifikiria nikamuuliza tena "hutokasirika?" ,akasema "inategemeana ila we sema tu"
Nikamwambia "nakupenda" akasema nirudie tena nikamwambia tena "I love you". Akakata simu nikawa nikipiga haipatikana Mara hapokei sio siri nikakujutia roho yangu.
Kesho yake asubuhi alikuja hadi home akiwa anaonekana hayupo sawa nikawa najaribu kujichetua ili hata afurahi lakini wapi.
Nikamuomba radhi kama neno lile lilimuudhi akadai nisijali sana,akaanza kunifungukia bwana kumbe anipenda pia alikuwa anafikiria,niliruka kwa furaha.
Mapenzi yetu yalianzia hapo na hakuna aliyemtia stress mwenzake,she was my first love alinifundisha nini mapenzi na kila kitu alikuwa fundi kitandani sitamsahau.


Tulienda hadi tunakaribia kumaliza form six siku ya sherehe mambo yaliharibika,kumbe mzee wangu na baba wa demu wangu walikuwa na mabifu ya kibiashara kitambo na kuna vitu washawahi kufanyiana.
Demu wangu alipandikizwa maneno na mzee wake hadi akatokea kunichukia Mimi na mzee wangu na inavyosemekana dingi ashawahi kusababisha kifo cha mama yake wa laaziz wangu.
Binafsi hata mzee nikimuuliza habari hizo hataki kunijibu anajibu wa mkato kuna kitu ananificha.
Niliumia sana hata mtihani nilifanya kwa stress nilifaulu kwa uwezo wa mola.
Mapenzi wangu akawa hanitaki tena,nikaenda jeshini miezi mitatu kurudi alishaondoka walihama na baba yake na sijui walihamia mkoa gani au nchi gani.

Wewe msichana kama upo humu jf jaribu kurudisha moyo wako nyuma,ugomvi wa wazazi wetu sisi hautuhusu I'm still in love with you!!!
Hata kama upoJupiter rudi mara moja nimemiss tabasamu lako na joto lako pia.Niliwahi kuapa sitatoa chozi for the sake of love lakini yanatoka mengi oh my god!!!!

I MISS YOU LAAZIZ!!!!



SAMAHANI KWA STORY NDEFU SIKUTAKA KUACHA KITU
Love story. I wish ningekuwa ndani ya story yako. Ila pole mwaya. Labda atajitokeza. Japo hilo bifu LA wazaz ni pasua kichwa.
 
Love story. I wish ningekuwa ndani ya story yako. Ila pole mwaya. Labda atajitokeza. Japo hilo bifu LA wazaz ni pasua kichwa.
Shukrani mkuu
Nahisi kumchukia mzee baba nahisi yeye ndo chanzo cha yote,kunipotezea wife material wangu wa baadae
 
Nasema ivi kam haelewek fyeka

Hataki kukutafuta fyekaaa

Na kam hajarud baada ya wiki fyekelea mbaliiii
Mwaka sasa na nusu unaelekea wa mateso nimemtafuta kaniblock kwenye mitandao yote ya kijamiii
 
chinekeeee said:
Jikazee ..kutindinganya mambo
najitahidi kujikaza japo marafiki zangu wananicheka sana hasa wakikukumbuka kipindi cha o level nilivyojifanya mgumu nikidai sitakuja kuumia wala kulia kwa sababu ya mapenzi.
 
Haiwezi kuwa tamu kama ya D. sultan. Wao walianzia shuleni.
umeona ee kama love story in Harvard vile
Halafu iwe first love kuna moments fulani hivi huwa hazisahauliki haswa tukiwa tunakimbizana baharini kwa utani
 
Mwaka sasa na nusu unaelekea wa mateso nimemtafuta kaniblock kwenye mitandao yote ya kijamiii
Situation unayopitia ni zaid ya kitendawili. Hata ukionana na mahabuba wako sipati picha kitakachotokea. Ugomvi wa wazaz wenu ni kama umewawekea ukuta usioweza kubomoka mbele yenu. Wewe huna hatia, lakini, huyo bibie kweli ataweza kustahimili kutengeneza familia na mtu ambaye baba'ake amehusika katika kifo cha mama Yake!?? Yote kwa yote, nakutakia kila la heri
 
Situation unayopitia ni zaid ya kitendawili. Hata ukionana na mahabuba wako sipati picha kitakachotokea. Ugomvi wa wazaz wenu ni kama umewawekea ukuta usioweza kubomoka mbele yenu. Wewe huna hatia, lakini, huyo bibie kweli ataweza kustahimili kutengeneza familia na mtu ambaye baba'ake amehusika katika kifo cha mama Yake!?? Yote kwa yote, nakutakia kila la heri
Yah nawaza hilo asije kufikiria kufanya kisasi na moyo wake ulishajazwa sumu ya chuki hadi sikuamini kuwa ndo yule tuliefanya nae ya kufurahisha.
Then ndo aliyenitoa wenge la kitoto kuwa na hisia
 
Hhehehehehee Mahabat Mahabuba Mahaba....

Kila la kheri, acha mie nimpet pet wangu mwandani.

Nimekumbuka wimbo wa zamanii, siku hizi hata siusikii ukipigwa.....

TX Mpenz dokta wangu wa ndaniii. aayaa aayaa aaayaaa...
....amespeshalaizi kwenye upasuaji.....



Njoo uniopareti TX nipasueee pindua pindua kila kitu ndanii...

Yaaalaaah mahaabaa hayaaa.
 
Back
Top Bottom