Nono
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 1,536
- 643
Ndugu Wana Jamii Forum,
Nawashukuru wote na nitakaribisha michango ili kuweza kuendesha kesi hii. Shida kubwa iko katika kutoa vivuli vya nyaraka nyingi ambazo tutatakiwa kuzitoa mahakamani pamoja na gharama za mawakili wenzangu ambao wamekubali kushirikiana nami katika kuendesha kesi hii.
Nawashukuru sana na tuzidi kusaidiana kuiokoa nchi yetu.
Asanteni
Rugemeleza Nshala
Tanzania ni yetu sisi na wajukuu wa wajukuu wa vitukuu vyetu. Tusipoilinda leo, hivyo vizazi havitairithi nchi. Hongera sana kwa ujasiri na uzalendo mkubwa. Tupo pamoja na tutasaidiana kwa hali na mali katika hili!
Roboti anaweza kutuandalia njia nzuri ya kuanza kubipiana katika hili! Shukrani.