Fine ya kuingilia mradi wa serikali(tanroads)

Fine ya kuingilia mradi wa serikali(tanroads)

Seran

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2025
Posts
12,110
Reaction score
35,914
Habari wana jukwaa,
Hii iwafikie wanaojua sheria za Tanroads
Naomba kuuliza wajuzi, hivi ikitokea kuna mradi wa ujenzi barabara njia imekuwa diverted na wewe ni mgeni eneo hilo kwa bahati mbaya ukapita ila ukashtuka haiko sawa ukaona ugeuze.

Unafika mbele kidogo kuna mtu katufata chap kwa haraka na boda nyuma anatusimamisha anadai twende tanroad tukalipe fine ya tsh 1,800,000/- tumeomba msamaha sana na kumwambia mmoja wetu ni mgonjwa kaja tu hospitali na hatukujua, hiyo pesa hatuna labda tusaidiane tu, haelewi huyu mtu, anauliza tumepungukiwa shingapi atusaidie! baadaye tukaanza kupiga simu kwa tunaowajua ili tufanyiwe wepesi tuendelee na safari zetu ndio akasema katusamehe tuendelee na safari!

Kwahiyo nataka kujua ni kosa kisheria kupita eneo lililozuiliwa kupita maana yake ni kuingilia mradi, na umeingilia huo mradi kivipi? Na kama unapaswa kulipa fine, hiyo fine ni shingapi?
 
1,800,00/- ni shilingi ngapi mkuu?😋

Hakuna namna, ni ama utoe rushwa uachwe uende zako au uilipe hiyo fine. Hawa jamaa wa tanroads au parking za manispaa ni wakuda sana!
 
1,800,00/- ni shilingi ngapi mkuu?😋

Hakuna namna, ni ama utoe rushwa uachwe uende zako au uilipe hiyo fine. Hawa jamaa wa tanroads au parking za manispaa ni wakuda sana!
Hahaha 1.8k mkuu, kwahiyo ni sheria kabisa ipo?
 
Ni kosa kisheria kupita eneo lililozuiliwa , na kama kuna uharibifu mlifanya ni halali kulipia faini kwa invoice maalumu.
 
Habari wana jukwaa,
Hii iwafikie wanaojua sheria za Tanroads
Naomba kuuliza wajuzi, hivi ikitokea kuna mradi wa ujenzi barabara njia imekuwa diverted na wewe ni mgeni eneo hilo kwa bahati mbaya ukapita ila ukashtuka haiko sawa ukaona ugeuze.

Unafika mbele kidogo kuna mtu katufata chap kwa haraka na boda nyuma anatusimamisha anadai twende tanroad tukalipe fine ya tsh 1,800,000/- tumeomba msamaha sana na kumwambia mmoja wetu ni mgonjwa kaja tu hospitali na hatukujua, hiyo pesa hatuna labda tusaidiane tu, haelewi huyu mtu, anauliza tumpungukiw ashingapi atusaidie! baadaye tukaanza kupiga simu kwa tunaowajua ili tufanyiwe wepesi tuendelee na safari zetu ndio akasema katusamehe tuendelee na safari!

Kwahiyo nataka kujua ni kosa kisheria kupita eneo lililozuiliwa kupita maana yake ni kuingilia mradi, na umeingilia huo mradi kivipi? Na kama unapaswa kulipa fine, hiyo fine ni shingapi?
Kiukweli kabisa mama mdogo ni kosa kisheria na faini ipo na kama mngeenda Tanroads kweli faini ingewahusu ila pia brother kaka maana najua huyo boya hakuwa mwanamke ni janaume na hapo lilitaka mkilikata hela chap iwe ya kusafushia vumbi la barabara .

Pole sana kwa hayo ila hongera kwa kuyamaliza salama
 
1.8k ni Tsh. 1800. Unamaanisha hivyo? Sasa si mlipe muondoke zenu😅😅😅
Fine za Tanroad ni kubwa sana, sio kama za polisi(usalama barabarani)
Bwana wewe umeelewa kikubwa inahitajika faini!😀 Hizo fine ni kubwa sana masikini hatuna hiyo pesa kwa harakaharaka hivyo au nikupe acc utulipie mkuu😎
 
Faini ipo ma mtu, wanasema kutokujua sheria hakukufanyi ushindwe kuhukumiwa kwa hiyo sheria, bora mliyamaliza juu kwa juu mngeenda ofisini ingekua worse
 
Kiukweli kabisa mama mdogo ni kosa kisheria na faini ipo na kama mngeenda Tanroads kweli faini ingewahusu ila pia brother kaka maana najua huyo boya hakuwa mwanamke ni janaume na hapo lilitaka mkilikata hela chap iwe ya kusafushia vumbi la barabara .

Pole sana kwa hayo ila hongera kwa kuyamaliza salama
Hahahaa Kumbe? Na ndio hiyo gharama yenyewe au kuna nyingine tofauti?

Asante mkuu..
 
Back
Top Bottom