Finally naanza upya maisha ya kujitegemea nikiwa mfukoni nina laki 8 tuu

Unasema kuna mtu kajitolea kukulipia 180k kwa mwezi ndani ya miezi 6? Yaani 180k * 6 months?

Tafuta chumba cha bei chee, mshiko mwingine peleka kwenye kuwekeza
 
Mzee hio kodi imekaaje?? 180k kwa mwezi au 180k kwa miezi yote sita?
Kama unakaa chumba cha 180k kwa mwezi. Utakuja kufulia na hutaamini.. watu wana maisha na walishajiestablish kishkaji na bado wanakaa mageto ya 50k.
 
Pambana kijana achana na hawa wanaokukatisha tamaa mala huwezi, mala sijui utashindwa kisa ulikua kwa bamdogo na vitu kama hivo.

Kwenye kufanikiwa naamini kuna juhudi lakini pia kuna bahati mkuu. Kuna watu wanahustle saana lakini matokeo 0, bahati imewapita kushoto lakini kuna watu wakigusa tu imo. Wewe pia una bahati mkuu usawa huu kupewa pesa hizo mkuu ni bahati ukizingatia mzee anajua hujawai kufanya biashara(umesema ulikua muajiliwa kiwandani). Pambana uiongeze hiyo pesa mkuu mimi naamini kila mtu akijitoa anatoboa tu, tena bahati yako ni kua una mwanzo mzuri huwazi kodi, pesa ya kuanzia maisha unayo pesa ya mtaji unayo.

Kaza buti mzebaba
 
Mie nilivyomaliza chuo, nyumbani niliondoka na kitanda na godoro tu. Hata hela ya code sikuwa nayo. Kuna mshkaji alikuwa na kodi ya miezi 6 ndio akalipa vyumba viwili miezi mitatu. So nilikuwa na miezi miwili tu ya kutake off ili niweze kujichanga na kupata hela ya kulipia miezi mitatu vyumba viwili. Mwanzo huwa ni mgumu but ukijipanga fresh, utatoboa.
You're so lucky unawashkaji wanaoeleweka, kwa sikuhizi ni rare sana
 
Safi sanaa hiyo pesa ukiichezea shauri yakoo
Anza kuuza hata vinywaji
 
Mungu atakubariki na utafanikiwa kwa uwezo wake,,,hyo pesa ni nying sana ukiwa na Malengo na ukituliza akili ,,,mi nakumbuka nilipewa laki 1 tu na nilitoka dar kwenda mkoa ambao sina ndugu wala jamaa.
 
Ona, dingi kampa 800k, msamaria kajitolea 180k *6months. Ñingetafuta chumba cha 80k then 100kx6 + 800k ningekuwa na 1,400k.
Ningeanzia hapo...kuna nyakati mambo yakiwa magumu unashuka chini uanze upya tu.
Mkuu nadhani hiyo 180000 ni kodi ya miezi yote sita kwa maana kila mwezi shilingi 30000.

Nipo tiyari kusahihishwa
 
Back
Top Bottom