Yupo CCM ila anajua wajibu wake kama mbunge,wa kuisimamia Serikali awapo Bungeni,huku akitanguliza maslahi ya wananchi waliomtuma na taifa lake mbele.Wabunge wengi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wapo bungeni kukitetea chama na hivyo ni kana kwamba hawana muda kabisa wa kutafakari hoja(hata zenye manufaa kwa taifa) zinapotolewa na mwakilishi wa wananchi bungeni kutoka chama cha upinzani-muda wote ni kutafuta tu namna ya kupinga na kushindana. Kwa mwendo huu ni vigumu sana kufika huko tunakotaka kufika katika maendeleo ni kama bunge ni sehemu ya mashindano na kutafuta kuchekesha.Wananchi tunayaona na kufuatilia kwa makini pamoja na kuyapima yote wanayofanya huko na ni jukumu letu kuyakumbuka bila kusahau na kuwaadhibu wabunge wote wa namna hiyo hapo mwaka 2015,hii ni bila kujali ni kutoka CCM au upinzani bali ni kwa wote wanaoonekana kutofanya kilichowapeleka bungeni.