Filikunjombe: Serikali ya CCM imevaa miwani ya mbao

Filikunjombe: Serikali ya CCM imevaa miwani ya mbao

Jadi

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
1,494
Reaction score
864
Yaani kweli Bungeni ukuwasema wapinzani kwa lugha mbaya unasifiwa, kama jana Mkamia alivyoendelea baada ya kumtukana Sugu, leo Filikunjombe kalazimishwa kutoa neno miwani ya Mbao, ila ndo hivyo Waziri Mkuu hapo anapata machungu na kukumbuka yale majina ya wabunge waliosaini kutokuwa na imani naye, Filikunjombe alikuwa muwazi na si mnafiki kama wengine:rockon:
 
Anasema wanafanya mambo kwa - funika kombe mwanaharamu apite. Anasema Waziri Mkuu aliapa kuilinda katiba lakini sasa wanachokifanya ni kulindana tu.

Anasema bungeni kuna mawaziri 30 lakini wanaowajibika ni kama 10 na anaweza kuwataja.

Anasema tusifanye kazi za Nape Nnauye bungeni. Anasema tusiwabeze wapinzani kwa kila kitu.

Huyu jamaa anaonekana moyo wake hauko tena CCM.

Source: Bungeni leo asubuhi
 
Anasema wanafanya mambo kwa -
funika kombe mwanaharamu apite. Anasema Waziri mkuu aliapa kuilinda
katiba lakini sasa wnafanya kulindana.

Anasema bungeni kuna mawaziri 30 lakini wanaowajibika ni kama 10 na
anaweza kuwataja.

Anasema tusifanye kazi za Nape Nnauye kule bungeni. Anasema tusiwabeze
wapinzani kwa kila kitu

Huyu jamaa anaonekana moyo wake hauko tena CCM.

Mzee wa Miongozo (Mwalimu Lukuvi) hakuingilia kati kweli, baada ya makombora hayo?
 
Akichangia hotuba ya waziri mkuu amekataa kuunga mkono hoja,huku akisema serikali imevaa miwani ya mbao na kuziba masikio. Akawalaumu Ccm kwa kuwabeza wapinzani na kufanya kazi za Nape bungeni badala ya kupokea hoja za wapinzani na kuzifanyia kazi. Akasema wapo mawaziri ambao walikuwa upinzani na wameelewa wamerudi.
 
Awataka wabunge CCM waache kufanya kazi za NAPE na wawajibike badala ya kufanya SIASA BUNGENI. WASIPOPATA meli katika jimbo lake wataandamana muda wowote na mahala popote, amekataa kuunga mkono hoja ya waziri mkuu hadi mambo ayatakayo yatimizwe.

Njano5.
 
Mzee wa Miongozo (Mwalimu Lukuvi) hakuingilia kati kweli, baada ya makombora hayo?

Hakuingilia kati, naona walijikaza ila Spika alimwambia afute kauli yake ya miwani ya mbao, akafuta naona hapo pia ili kufunika kombe mwanaharamu apite!! Lakini msg delivered!
 
SAFI!! uPINZANI NDIYO KAMA HUU. SIYO KILA KITU WANACHOSEMA WAPINZANI NI KUTUPA KAPUNI. MBONA WANAYOYASEMA YANAAKISI UHALISIA WA MAMBO MTAANI??? CCM WANAISHI NCHI GANI, SIAMINI KAMA WANAISHI HAPA TANZANIA! Ops! Wao wanaishi kwa KUEPA....mh
 
Akichangia bunge na kutokuunga mkono hoja, kasema watu wa Rudewa wanahitaji vitu viwli tu
1. Meli ziwa nyasa kama alivyoahidi Raisi
2. Barabara ya lami

Kasema kama hivi vitu havitatekelezwa, wataandamana. Kasema wabunge wa CCM wabadilike, si kupinga kila kinachosemwa na upinzani, wachukuwe hoja zao na kuzifanyia kazi.


Hawa wanaotukana ni kuwa wanafanya kazi ya Nape, sasa mnataka nape afanye kazi gani??
 
Kama wabunge wote wa CCM wangekuwa kama Deo Filikunjombe bila shaka serikali îngewajibika. Hakuongea kama shabiki bali kama anayejua wajibu wake bungeni. Mimi amenifurahisha sana. Hakika Ludewa wana mbunge. Big up Deo.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Heshima kwenu wanajamvi,yaani tokea nimeanza kuangalia bunge la bajeti wiki iliyopita nimekuwa nikikerwa sana na baadhi ya wabunge ambao wanasimama kuchangia hoja ya bajeti tokea mwanzo wa hoja zaoa mpk mwisho ni wanaiponda bajeti nakuonyesha mapungufu yake katikakuwapelekea maendeleo wanachi alafu mwisho eti mbunge huyoyhuyo anunga mkono hoja tena kwa asilimia mia moja.

Huu ni upuuzi naomba nirudie tena huu ni upuuzi raia yangu kwa wabunge kama unaona bajetii haikusaidii wewe na wanajimbo wako kuwaleteeni maendeleo tafadhali usiounge mkono hoja hata kama wewe ni mwana CCM,

Naomba mfuate mfano wa deo filikunjombe mbunge wa ludewa(CCM) ingawaje yeye ni ccm lakini hajaunga mkono hoja ya mjadala wa bajeti ya ofisi ya waziri mkuu kwa sababu ya propaganda endelevu za ccm mfano meli,raisi aliahidi lakini kila siku anawapiga kalenda na chenga,naomba kuwasilisha
 
Yule jamaa ni jembe sio siri. CCM lazima watampiga chini awamu ijayo
 
Namkubali sana Filikunjombe,maana huwa hana mambo ya kusifia,ni kusema ukweli tu,kilichonishangaza wenzake hawampigii makofi,ila lusinde na wenzake wakitukana,wanashangaliwa
 
Moyo wa ukweli siku zote ni mafanikio na maendeleo. Utumwa ni dhambi, naukweli siyo upinzani wa maendeleo
 
Back
Top Bottom