Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
MBUNGE FILIKUNJOMBE AWAKATAA WAHANDISI MBELE YA NAIBU WAZIRI ATAKA NAIBU WAZIRI AONDOKE NAO,KISA UFISADI WA FEDHA ZA MIRADI
Picha Kulia:
Picha Kushoto:
Picha Kulia:
BAADA ya naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Tamisemi Aggrey Mwanri kuukataa mradi wa umwagiliaji katika kata ya Lifua wilayani Ludewa uliojengwa kwa zaidi ya shilingi milinio 500 bila kufanya kazi kutoka na kubomoka kabla ya muda na ule wa ukarabati wa nyumba ya mganga kata ya Lupanga iliyokarabatiwa kwa kiasi cha shilingi milioni 7 ,mbunge wa jimbo la Ludewa acharuka mbele ya naibu waziri amkataa mhandisi wa maji na mhadisi wa ujenzi ataka naibu waziri kuwapeleka jimboni Kwake ama jimbo la waziri mkuu Mizengo Pinda.
Mbunge Filikunjombe aliwakataa wahandisi hao wawili Christopher Nyandiga wa maji na mhandisi wa ujenzi Rashid Mtamila katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa wakati wa majumuisho ya ziara ya siku mbili ya naibu waziri huyo katika kutembelea miradi ya kimaendeleo katika wilaya hiyo ya Ludewa.
Mbunge Filikunjombe alimweleza naibu waziri huyo kuwa wilaya ya Ludewa imegeuzwa kuwa ni shamba la bibi kwa baadhi ya viongozi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakitumia vibaya nafasi zao kwa kuhujumu miradi ya kimaendeleo inayoibuliwa katika wilaya hiyo. Alisema kuwa kila wakati amekuwa akiwaonya watumishi wa wilaya ya Ludewa kufanya kazi yao kwa uadilifu ila baadhi yao wameshindwa kabisa kuonyesha uaminifu katika utendaji wa kazi yao.
Viongozi wenzangu na madiwani wangu wapo walionifuata kutaka niwatetee kwa uozo huu ila nasema heri kulaumiwa kwa kusimamia ukweli na kupinga ufisadi unaofanyika katika wilaya ya Ludewa ila nipo tayari kuendelea kufanya kazi na viongozi waadilifu Alisema kuwa wahandisi hao wameendelea kuwa kikwazo kikubwa katika wilaya ya Ludewa na kuwa miradi mbali mbali inayosimamiwa katika wilaya hiyo imekuwa ni mibovu na haina sifa japo imetumia fedha nyingi zaidi .
Mapema asubuhi naibu waziri huyo alifanya ziara ya ghafla ambayo haikuwepo katika ratiba katika banio la mradi wa umwagiliaji wa Lifua ambalo umejengwa na kampuni ya Summer Communication kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 357 toka mwaka 2009/2010 bila kufanya kazi . Kitoa taarifa ya mradi huo mbele ya naibu waziri Mhandisi wa maji wilaya ya Ludewa Nyandiga alisema kuwa awamu ya kwanza ilitumia kiasi cha shilingi milioni 357,262,990 na mradi huo kukabidhiwa kwa Halmashauri toka mwaka 2010 japo hautumiki kutokana na kuvujisha maji.
Wakati awamu ya pili mradi ulijengwa na kampuni ya Tan Direct Co.Ltd ya Dar es salaam kwa gharama ya shilingi milioni 227,613,136.15 kwa kazi ya kujenga mfereji wenye urefu wa mita 1725,usakafiaji wa eneo la kuingia na kutoka kwenye daraja hilo ,ujenzi wa vigawa maji vinne na ujenzi wa vianguko vya maji vinne na ujenzi wa kivusha maji kimoja na kuwa hadi sasa mkandarasi huyo amelipwa asilimia 64.9 ya fedha zote na kazi hiyo imefanyika kwa asilimia 73.2
Akimhoji mkandarasi huyo naibu waziri huyo Mwanri alimtaka kueleza sababu ya kulipa mamilioni ya fedha katika mradi huo bila kufanya kazi na hauna maji katika kipindi hiki cha masika ,mhandisi huyo alikana kuwa yeye si msanifu wa mradi huo hivyo hawezi kujibia swali hilo. Akitoa majumuisho yake na maombi ya mbunge Filikunjombe ya kutaka wahandisi hao kuondolewa katika wilaya hiyo ya Ludewa naibu waziri huyo alisema suala hilo linawezekana kwani pia kwa upande wake hajapendezewa na ufisadi mkubwa uliofanyika katika miradi hiyo.
Picha Kushoto:
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto) akimwomba naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri kulia kuondoka na mhandisi wa ujenzi na maji wa wilaya ya Ludewa kwa madi ni mchwa katika wilaya hiyo ya Ludewa
Picha Kulia:
Naibu waziri wa Tamisemi Mwanri katikati akiwa na mhadisi wa maji Bw. Nyandiga ambaye pia hatakiwi Ludewa (kulia)
Daraja na Manda likiwa limevunjika kabla ya kuanza kutumika na limetumia zaidi ya mamilioni ya shilingi za wafadhili kutoka Japani hali iliyomchukiza mbunge na kutaka mhandisi wa ujenzi kuondoka wilaya hiyo.
Picha Kushoto:
Huu ni mradi wa umwagiliaji uliojengwa katika kata ya Lifua kwa zaidi ya milioni 500 ila maji hakuna na haufanyi kazi pamoja na kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Ludewa ,maradi mbao naibu waziri wa Tamisemi ameukataa na kutaka mkoa kuunda tume kuchunguza wizi huo,mradi huo ulibainika baada ya kufanya ziara ya ghafla ambayo haikuwepo katika ratiba
Picha Kulia:
Mfereji wa kifisadi wa LIfua ambao umejengwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji bila kutimika kwa miaka miwili sasa
Picha Kushoto:
Naibu waziri wa Tamisemi na viongozi wakikagua daraja jipya linalojengwa mto manda baada lile la awali kubomoka bila kutumika
Picha Kulia:
Naibu waziri wa Tamisemi Mhe.Mwanri kulia akimwonyesha ubovu wa majengo ya umma mhandisi wa ujenzi Ludewa Bw Rashid Mtamila,kushoto