Filikunjombe ataka Naibu Waziri aondoke na Wahandisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Filikunjombe ataka Naibu Waziri aondoke na Wahandisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jan 20, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  MBUNGE FILIKUNJOMBE AWAKATAA WAHANDISI MBELE YA NAIBU WAZIRI ATAKA NAIBU WAZIRI AONDOKE NAO,KISA UFISADI WA FEDHA ZA MIRADI

  [​IMG] [​IMG]
  Picha Kushoto: ​
  Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto) akimwomba naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri kulia kuondoka na mhandisi wa ujenzi na maji wa wilaya ya Ludewa kwa madi ni mchwa katika wilaya hiyo ya Ludewa


  Picha Kulia:
  Naibu waziri wa Tamisemi Mwanri katikati akiwa na mhadisi wa maji Bw. Nyandiga ambaye pia hatakiwi Ludewa (kulia)​
  [​IMG][​IMG]
  Daraja na Manda likiwa limevunjika kabla ya kuanza kutumika na limetumia zaidi ya mamilioni ya shilingi za wafadhili kutoka Japani hali iliyomchukiza mbunge na kutaka mhandisi wa ujenzi kuondoka wilaya hiyo.

  [​IMG] [​IMG]
  Picha Kushoto:
  Huu ni mradi wa umwagiliaji uliojengwa katika kata ya Lifua kwa zaidi ya milioni 500 ila maji hakuna na haufanyi kazi pamoja na kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Ludewa ,maradi mbao naibu waziri wa Tamisemi ameukataa na kutaka mkoa kuunda tume kuchunguza wizi huo,mradi huo ulibainika baada ya kufanya ziara ya ghafla ambayo haikuwepo katika ratiba​

  Picha Kulia:
  Mfereji wa kifisadi wa LIfua ambao umejengwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji bila kutimika kwa miaka miwili sasa


  [​IMG] [​IMG]
  Picha Kushoto:
  Naibu waziri wa Tamisemi na viongozi wakikagua daraja jipya linalojengwa mto manda baada lile la awali kubomoka bila kutumika

  Picha Kulia:
  Naibu waziri wa Tamisemi Mhe.Mwanri kulia akimwonyesha ubovu wa majengo ya umma mhandisi wa ujenzi Ludewa Bw Rashid Mtamila,kushoto​


  BAADA ya naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Tamisemi Aggrey Mwanri kuukataa mradi wa umwagiliaji katika kata ya Lifua wilayani Ludewa uliojengwa kwa zaidi ya shilingi milinio 500 bila kufanya kazi kutoka na kubomoka kabla ya muda na ule wa ukarabati wa nyumba ya mganga kata ya Lupanga iliyokarabatiwa kwa kiasi cha shilingi milioni 7 ,mbunge wa jimbo la Ludewa acharuka mbele ya naibu waziri amkataa mhandisi wa maji na mhadisi wa ujenzi ataka naibu waziri kuwapeleka jimboni Kwake ama jimbo la waziri mkuu Mizengo Pinda.

  Mbunge Filikunjombe aliwakataa wahandisi hao wawili Christopher Nyandiga wa maji na mhandisi wa ujenzi Rashid Mtamila katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa wakati wa majumuisho ya ziara ya siku mbili ya naibu waziri huyo katika kutembelea miradi ya kimaendeleo katika wilaya hiyo ya Ludewa.

  Mbunge Filikunjombe alimweleza naibu waziri huyo kuwa wilaya ya Ludewa imegeuzwa kuwa ni shamba la bibi kwa baadhi ya viongozi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakitumia vibaya nafasi zao kwa kuhujumu miradi ya kimaendeleo inayoibuliwa katika wilaya hiyo. Alisema kuwa kila wakati amekuwa akiwaonya watumishi wa wilaya ya Ludewa kufanya kazi yao kwa uadilifu ila baadhi yao wameshindwa kabisa kuonyesha uaminifu katika utendaji wa kazi yao.

  “Viongozi wenzangu na madiwani wangu wapo walionifuata kutaka niwatetee kwa uozo huu ila nasema heri kulaumiwa kwa kusimamia ukweli na kupinga ufisadi unaofanyika katika wilaya ya Ludewa ila nipo tayari kuendelea kufanya kazi na viongozi waadilifu “ Alisema kuwa wahandisi hao wameendelea kuwa kikwazo kikubwa katika wilaya ya Ludewa na kuwa miradi mbali mbali inayosimamiwa katika wilaya hiyo imekuwa ni mibovu na haina sifa japo imetumia fedha nyingi zaidi .

  Mapema asubuhi naibu waziri huyo alifanya ziara ya ghafla ambayo haikuwepo katika ratiba katika banio la mradi wa umwagiliaji wa Lifua ambalo umejengwa na kampuni ya Summer Communication kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 357 toka mwaka 2009/2010 bila kufanya kazi . Kitoa taarifa ya mradi huo mbele ya naibu waziri Mhandisi wa maji wilaya ya Ludewa Nyandiga alisema kuwa awamu ya kwanza ilitumia kiasi cha shilingi milioni 357,262,990 na mradi huo kukabidhiwa kwa Halmashauri toka mwaka 2010 japo hautumiki kutokana na kuvujisha maji.

  Wakati awamu ya pili mradi ulijengwa na kampuni ya Tan Direct Co.Ltd ya Dar es salaam kwa gharama ya shilingi milioni 227,613,136.15 kwa kazi ya kujenga mfereji wenye urefu wa mita 1725,usakafiaji wa eneo la kuingia na kutoka kwenye daraja hilo ,ujenzi wa vigawa maji vinne na ujenzi wa vianguko vya maji vinne na ujenzi wa kivusha maji kimoja na kuwa hadi sasa mkandarasi huyo amelipwa asilimia 64.9 ya fedha zote na kazi hiyo imefanyika kwa asilimia 73.2

  Akimhoji mkandarasi huyo naibu waziri huyo Mwanri alimtaka kueleza sababu ya kulipa mamilioni ya fedha katika mradi huo bila kufanya kazi na hauna maji katika kipindi hiki cha masika ,mhandisi huyo alikana kuwa yeye si msanifu wa mradi huo hivyo hawezi kujibia swali hilo. Akitoa majumuisho yake na maombi ya mbunge Filikunjombe ya kutaka wahandisi hao kuondolewa katika wilaya hiyo ya Ludewa naibu waziri huyo alisema suala hilo linawezekana kwani pia kwa upande wake hajapendezewa na ufisadi mkubwa uliofanyika katika miradi hiyo.

   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Madogo wanataka kupata fedha za haraka haraka hawa inakula kwao,lol!
   
 3. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jambo moja kuu la kukumbuka ni kuwa Ludewa kama Makete ni Wilaya za pembezoni na hazina watumishi wa kutosha. Kwa karibu miezi mitatu iliyopita tumesoma kwenye magazeti Mhe. pamoja na Baraza la Madiwani wakitaka watumishi muhimu waondolewe Ludewa na kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu uendeshaji wa Halmashauri hiyo hasa kwenye masuala ya utoaji wa zabuni na usimamizi wa kazi.

  Tunaweza tusimlaumu sana Mhe. kwasababu anataka ufanisi wa kazi lakini yapo maswali ya kujiuliza: Nafasi ya Mkurugenzi katika usimamizi wa shughuli za maendeleo ni nini na je Mkuu wa Wilaya kama mhimili msaidizi wa Halmashauri hiyo anafanya nini anapoona hali kama hii inatokea.

  Anakwenda vijijini? au anasubiri hadi waje mawaziri? Tuliona kwenye sakata la ununuzi wa Mahindi na mwisho ni muhimu kujiridhisha kama kuna ushahidi wa kutosha na wa msingi unaoweza kuwabana watendaji wanaotuhumiwa.

  Imesemwa kwenye vyombo vya Habari lakini hawajapewa fursa/haki yao ya msingi ya kujitetea. Otherwise tunakupongeza sana Candid Scope kwa kutuhabarisha kutoka Iringa. Unayoyaibua yanaibua pia changamoto nyingine nyingi zinazotukabili na sisi kwenye mikoa yetu.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Bwana Mpoki, waliobahatika kupangiwa kazi huko wilaya za pembezoni wameshazoea ulaji na hakuna wa kuwasuta. Hawa viongozi waandamizi kama wakuu wa mikoa na wilaya wanakula meza moja, ndio maana hawashtuki wala kuwashtukia.

  Mambo yanapowageukia wahandizi mkuu wa wilaya na Mkurugenzi wanaingia mitini, wanabaki kuslulibiwa peke yao wakati ulaji walishirikiana.
   
 5. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Candid scope ndo Filikunjombe mwenyewe nn? habari zote za mh mbunge huyu ndo huwa unazileta,,thanks lkn kwa updates/infos
   
 6. m

  mokomoko Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hila tunapaswa kuwa wazi wabunge wengine wanapenda sana kusifiwa tena kwa gharama yeyote hile, hivi mbona sijawahi kuona candic scope hakileta habari zenye walau kumkosoa mr huyu mwenye mapungufu mengi sana.
  kwanza deo anadhihilisha namna asivyo mtendaji mzuri kwa sababu yeye hawezi kukemea mambo kama haya yeye kama mbunge hila mpaka waziri aje au madiwani wasema hii inadhiirisha jinsi alivyo weak kyenye maamuzi magumu, si vizuri kufanya kazi kwa visa maana huyu mwandisi hajaondoka na waziri husika kwa maana hiyo wewe huwezi kazi maana kama ungekuwa unaweza kazi mboza mhandisi angeondoak siku hile hile jamaa anapenda sana kukusifia lakini nahisi yeye hayupo ludewa, na husipo angalia makundi yatakumaliza kisiasa, jaribukukutana na wapinzani wako ndani ya chama na ujishushe kwao wao wanaweza kukushauri vizuri kuliko hivi sasa watu wanapokuwa wanamwona katibu wako ndo mzuri zaidi kaa chonjo. hakuna haja ya kumhamisha mwandisi bali asimamiwe ipasavyo, wewe ndo mwenye jimbo utaamuru wafukuzwe wangapi? mbona wafanyakazi watakwisha wote sasa
   
 7. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huo ni unafiki wa mbunge, hivi madiwani walikuwa wapi kufuatilia mrdi huo katika kamati ya uongozi na fedha pamoja na baraza la madiwani? mbona walikuwa wanakagua miradi? huo hawakuuona hadi waziri aje?
   
 8. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Bongo bana, akitokea mpambanaji mnalaumu, wakitokea mafisadi mnalaumu.
  hamuoni kama Deo anafuata falsafa za CDM.
  Mnafikiri deo asingependa kukaa pale kijichi kwake na kula bia pale container? Deo chapa kazi bana
   
 9. F

  Fresh Air Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wa-tz tunapenda kuongoza kwa kutumia MBWA - Management By Walking Around - hivi tutafika kweli?
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Comment yako ungekuwa mgeni na Tanzania ningehitaji kukuelewesha, lakini kwa vile unajua uozo uliopo ndani ya serikali hii nashangaa kutoa upinzania wenye kuonyesha kama hujui mfumo uliopo wa kulindana.

  Ndani ya CCM na serikali yake kuna wapambanaji wazuri tu wanaojitahidi kwa moyo wote, lakini upinzani wanaoupata unaujua. Ya Mwakiembe na kundi lake we mgeni? Sita je? Unaona Nape alivyonyamazishwa? Sitaki kueleza mengi kwa vile we unaweza kunipa mifano zaidi.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mababu walioturithisha usemi huu kidole kimoja hakivunji chawa walishaona pengine zaidi ya tunayoona. Filikunjombe ni kama mbuzi aliyetupiwa ndani ya zizi la Fisi, mimi sishangai kwa kauli yako maana huenda uliyeleta comment hii ni wale waliopo ndani ya kundi lililogeuza Ludwa kuwa shamba la bibi, maana umeegemea upande mmoja tu na huoni upande mwingine.
   
 12. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Duh! Hizo nguzo za daraja zimeniacha hoi. Hata mie ambaye sio engineer could have done better kwa ku-google.
   
 13. N

  Njele JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hili daraja kama siamini vile, hali hii hata halijatumiwa, mhusika yupo lakini?
   
 14. K

  Kwaito Senior Member

  #14
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chonde usiudhalilishe uhandc,kama mambo ni rahc kwa ku-google basi vyuo vya uhandc vifungwe, thats just a technical failure
   
 15. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Madiwani huko Ludewa ni kama hawapo hivi, hivyo huwaachia viongozi wa halmashauri kufanya chochote bila kuhoji. Wengi wao shule hamna kabisa hivyo hawana logic. Mhe. Filikunjombe ni kama yupo peke yake hivi kupigania haki, pia pale ofisini pa halmashauri hawampendi eti wanadai anaziba riziki yao, Mbunge kazana tupo pamoja Kuleta maendeleo. Wengi walio chuma fedha Ludewa wanavitega uchumi vingi kama vyuo.
   
 16. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Filikunjombe ni kama tone ndani ya bahari, na ajue anakuwa na maadui wengi sana ndani nanje ya wilaya, anatakiwa kjuwa mgangalifu sana sasa hivi.
   
 17. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Jamani tusizibeze jitihada za Mh. Filikunjombe@ all
   
 18. T

  TUMY JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh. Filikunjombe kwa mtu ambaye amekuwa akimfuatilia kwa makini utagundua kwamba jamaa ni mpiganaji pia, fuatilia hoja zake mara kwa mara utaligundua hilo, mimi nimpongeze kwa ujasiri huo aliouonyesha kwani alichaguliwa ili atetee maslahi ya wananchi wake.BIG UP Mh. F.:poa. Mh. Mwanri nawe :poa huwa unawajibika sana.
   
 19. m

  mokomoko Member

  #19
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  usisemehe kuhusu mimi kuwa upande mmoja tu, je! uliwahi kuandika post yeyote inayomweleza deo masuala anayokosea?
  mbona mimi sijawahi kuona hilo, sema tu wewe mimi nakujua sana unaeandika post hizi na siku ukiendelea kumsifia mtu weak kama huyu ntakuweka wazi hili wanaludewa wakujue, kwa sababu, haiwezekani wewe unamsifia wakati hata mbolea ya ruzuku tu kashindwa kuifwatilia, sipo kwenye kundi lolote la ccm mimi hila mimi ni mwana cdm ahlisi na lazima hii wilaya watu wajue uozo wenu, kuna haja gani ya wewe kusubiri waziri haje? huo ni unafiki kwanza ulitembelea gepu kwa kutaka sifa tu maana mwandisi barua tayari ilikuwa imeandikwa ya kumwamisha kwenda sumbawanga na sababu za yeye kuhama tunazijua sasa wewe umetaka umaarufu wa kisiasa kupitia hilo kwa nini? tafuta kufanya mambo ya msingi, tulitegemea deo kuhoji juu ya mkurugenzi kutoudhuria vikao vya madiwani lakini upo kimya tu, bana hee!! mwache kusifiana ovyo
   
 20. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Mbunge ni diwan by default, kuweka record sawa
   
Loading...