Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,869
- 828,386
Unajua, maisha ya ndoa au mahusiano ni kama filamu ya action, lakini siku ukikutwa na "ushahidi" usio na maelezo, filamu inageuka kuwa ya mtihani mkubwa! Hebu fikiria, mkeo anafanya usafi, anasogeza kochi, ghafla anakutana na chupi ya kike ambayo haijawahi kuonekana kwenye bajeti ya nyumba hiyo tangu uhuru.
Hapo ndipo akili ya mwanaume inafanya "System Error".
Hill tukio lilimtokea jamaa yangu mmoja sasa ni marehemu (RIP mwamba)
Ilikuwa weekend Moja baada ya mke kurudi safari akawa anafanya usafi huku jamaa kajilaza kwenye kochi la jirani
Mara ghafla Mke akauuliza kwa sauti ya radi: "Baba nani, hii chupi ya nani?"
Jamaa kwa mstuko mkubwa lakini kwa utulivu wa bandia akauliza: "Chupi? Ipi? Ah, mbona kama kitambaa cha kufutia vumbi? Kwani fundi hakuacha hapo alipokuja kutengeneza TV?" (Hapo akijua kabisa fundi alikuja miezi sita iliyopita).
Mke akakaza akiuliza swali lile lile kwa ukali zaidi
Jamaa akaona abadili utetezi
"Mke wangu, unajua leo kulikuwa na upepo mkali sana? Inawezekana jirani alianika kule nje, upepo ukaipuliza, ikapita dirishani, ikazunguka sebuleni, kisha ikajikunja na kujificha chini ya kochi kwa usalama."
Mke akiwa kazidi kufura kwa hasira mpaka anatetemeka jamaa akaendelea na utetezi
"Hivi hujiulizi kwanini nguo zetu zinapotea kila siku? Hapa kuna majini! Leo wameamua kuleta badala ya kuchukua. Hii ni chupi ya majini, tusiiguse tuitie moto!๐๐ฟ๐คฃ
This time mke akiwa kanyanyua ufagio juu na kumwambia jamaa asiposema ukweli atamcharaza kisawasawa
Jamaa kwa kujifanya kakumbuka sasa akaropoka kindezi
"Ah! Kumbe ni hiyo? Si ndiyo aliyoisahau binamu yako Asha alipokuja wiki iliyopita? Alisema anaitafuta sana, ngoja nimpigie simu..." (Hapo akashika simu huku anatetemeka, akisali Asha asipokee).๐๐๐
Mungu bariki simu ya Asha ikawa haipatikani.. Sass mke katika kuikagua kama kweli ni ya Asha akagundua kitu kingine๐
"Lakini mbona ina jina lako limeandikwa kwa markerpen?".
Hapo sasa, jamaa alitamani ardhi ipasuke au ugeuke kuwa mbu upotee hewani๐คฃ๐คฃ๐คฃ.
Nilitwa kusuluhisha ile kesi na mambo yakaisha salama ila jamaa wakati ananisindikiza nikamshauri ahakikishe anapochepuka mchepuko unavaa nguo zinazofanana na za mkewe๐ au bora zaidi, asichepuke kabisa ili asije kutoa maelezo ya "upepo wa kisulisuli" uliopitisha nguo dirishani!๐๐๐