Ngoja nikuambie moja moja.
Ni aibu Hospitali ya Taifa kupata vitanda mpaka zizuiwe pesa zilizochangiwa kwa tafrija ya Wabunge, zile pesa hazikuwa za mafungu ya serikali bali taasisi ndio zimechanga. Pamoja na jambo hilo kuwa zuri lakini ni aibu. Ni sawa uchangiwe pesa za Harusi kisha useme kwa vile shemeji yake bwana Harusi ana familia kubwa na hana chakula wala pa kuishi basi hakuna sherehe fedha hizi zinakwenda kununua chakula chake na kumjengea kibanda.
Kuhusu 9 December, wewe unaamini huu ugonjwa Paulo Makonda aka Kipindupindu ndio unaweza kuahirisha Isifanyike ili pesa zitumike kufanya usafi? Basi elewa sababu kubwa ni kuficha aibu ya kuja uwanjani Anayeitwa Rais wa Zanzibar ambaye alikuwa anangojewa kwa hamu ili lile lililotokea Bungeni liendelee. Na kwa vile pale hata umwite Ndugai hawezi kufua dafu kutuliza aibu hiyo ikaonekana ni bora kupotezea tuu.
Eti mama Lowasa hangeweza kutulia kama mama Janeth! Hilo naona niliache maana usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Yaliyo nyuma ya utulivu huo ungeyajua pengine usingepoteza muda wako kuandika.
Hata hivyo Magu anastahili pongezi kwa jinsi anavyoipopoa CCM bila kuitazama usoni kwa kutumia yaleyale waliyokuwa wanayasema wapinzani juu ya serikali kipindi cha awamu ya nne. Ameamua kuwasomesha namba mpaka hawana hamu kabisa. Sasa hivi hata wakitaka kwenda hapo Nairobi lazima kujaza fomu kama wanaomba mkopo wa biashara.