Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 1,745
- 4,277
Shirikisho la Mpira Duniani(FIFA) imekubaliana na pendekezo la kuongeza idadi ya timu zinazocheza Kombe la Dunia hadi kufikia timu 48.
Rais wa Fifa, Gianni Infantino na Marais wa Mashirikisho ya mpira sita ambayo ni wanachama wa FIFA walikubaliana katika mkutano uliofanyika Alhamisi jijini Zurich.
Pendekezo hilo litawasilishwa ili kuidhinishwa na Baraza la FIFA ambalo litafanya mkutano tarehe 9 Mei eneo la Manama, Bahrain siku mbili kabla ya Kongamano la 67 la FIFA.
Likiidhinishwa, Afrika (CAF) itapata nafasi nne zaidi ya tano walizonazo sasa katika michuano hiyo na itaanza kufanya kazi katika michuano ya 2026.
Michuano hiyo itakayokuwa na nafasi 48, itakuwa na nafasi 46 za moja kwa moja na mbili zitakazoamuliwa baada ya pambano baina ya timu sita(6) ambapo 5 zitatoka kila moja ktk Mashirikisho isipokuwa UEFA na timu moja kutoka Shirikisho la timu mwenyeji.
Zifuatazo ni nafasi pendekezwa za moja kwa moja kwa kila Shirikisho:
Confederation of African Football (CAF) – 9
Asian Football Confederation (AFC) – 8
North, Central American and Caribbean Football Confederation (CONCACAF) – 6
South American Football Confederation (CONMEBOL) – 6
Oceania Football Confederation (OFC) – 1
Union of European Football Associations (UEFA) – 16