Fiesta fursa inafaida gani kwa jamii?

Fiesta fursa inafaida gani kwa jamii?

issakwisa6810

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2014
Posts
309
Reaction score
84
Kumekuwa na mambo yanayo endeshwa na tigo fiesta na clouds media kwa kusema sijui wanafundisha au kumjengea uwezo wa uchumi mimi napinga kwa herufi kubwa nimefuatilia muda mrefu semina zao wao zao kuleta watu walio fanikiwa tu kujigamba bila kuwapa njia za kujikwamua wale wajasiriamali wadogo kwanza kama kweli wako serious basi wangekuwa wanakuja na wataaalamu wa kufuga kuku, mabwana shamba wa kufundisha jinsi ya kuandaa bustani Mbalimbali sio kuleta watu wakujigamba.

Niambieni nikafanye nini nitoke nilipo sio kuniletea walio tusua hainisaidii bali inaniongezea stress, pili Hao mapatiner wao wa hiyo kampeni sio rafiki kabisa nawatu wa Hali za chini Hao LETSHEGO KWA JINA lingine faidika bank Hao waulize wafanyakazi watakuambia liba zao sijui asilimia ngapi kama sio 250%, kama wanania tujikombe basi waachane na kisa LETSHEGO na kina Nikki tuleteeni wataaalamu wa uzalishaji,

Mfano ufugaji kuku, ukulima wa muda mfupi wataaalamu wa fedha kama kufundisha Biashara sio kujisajili. Nawasilisha wananzengo
 
Wapo watu wenye mitaji hawajui wawekeze kwenye nini nadhani kupitia hiyo fursa watapata chakufanya......lakini zamaradi kaolewa.
 
Hao cloud wanawadanganya vijana wakitanzani amboa akili zao zimefyatuka yaani eti fursa presenters wanakuwa wakina young killer, Niki wa pili, Mr blue n.k mnaumwa vijana wakibongo.

Hao jamaa wanatafuta pesa siku kupitia ubwege wa watu.
 
mr blue anakufundisha ujasiriamali kweli.. au rubby??

ha ha ha
 
fursa kwa namna nilivyo ielewa mimi nikwamba wale majamaa pale hawakupi njia za kutoboa, lakini wanakupa hasira za kupambana na hali
yani ukisikia kijana mwenzako anaingiza 2m kwa wiki lazima utakomaa tu bila kupewa ramani
 
fursa kwa namna nilivyo ielewa mimi nikwamba wale majamaa pale hawakupi njia za kutoboa, lakini wanakupa hasira za kupambana na hali
yani ukisikia kijana mwenzako anaingiza 2m kwa wiki lazima utakomaa tu bila kupewa ramani
Tupeni njia tunakomaaje
 
Back
Top Bottom