BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,379
- 8,123
Chanzo cha mgogoro huo ni uamuzi wa Serikali wa mwaka 2017 kuifutia kampuni hiyo leseni ya uendeshaji wa mradi wa uchimbaji Dhahabu wa SMP ambapo kampuni hiyo haikukubaliana na uamuzi huo. Mwaka 2020 ilifungua kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) nchini Uingereza ikiwakilishwa na kampuni ya uwakili ya Lalive.
PESA ILIYOLIPWA INGEWEZA KUTEKELEZA MIRADI IFUATAYO KWA ZAIDI YA ASILILIMIA 100%
Kiasi cha fedha kilicholipwa kwa kampuni ya Winshear Gold ni kikubwa kuliko Bajeti za Wizara hizi za mwaka 2023/24:
- Utamaduni, Sanaa na Michezo - Tsh. 35,445,041,000
- Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira - Tsh. Bilioni 54.1
- Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum - Tsh. Bilioni 74.2
1. Zahanati - 267 (Gharama ya Zahanati moja Tsh. Milioni 280).
2. Vituo vya Afya - 65 (Gharama ya Kituo kimoja Tsh. Bilioni. 1.15).
3. Magari ya kubeba Wagonjwa - 250 (Gari moja Tsh. Milioni 300) kila Mkoa ungepata Magari 9.
4. Madarasa - 3,750 (Darasa moja Tsh. Milioni 20).
5. Madawati - Milioni 2.5 (Dawati moja Tsh. 30,000).
6. Vipimo vya CT Scan - 83 (Mashine moja Tsh. Milioni 900).
7. Visima Vifupi vya Maji - 25,000 - 75,000 (Kisima kimoja ni kati ya Tsh. Milioni 1 hadi Milioni 3 kutegemea na eneo).
8. Mkopo wa Elimu ya Juu - Wanafunzi 18,750 (Kila Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza angepata 100% Tsh. Milioni 4).
9. Pembejeo za Kilimo - Mifuko 6,250,000 ya Mbegu za Mahindi 6,250,000 (Mfuko mmoja Tsh. 12,000).