Fid Q awachana wakina dada wanaowategeshea wanaume wao watoto

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515

Rapa Farid Kubanda 'Fid Q' ameibuka na kuwachana baadhi ya wakina dada wenye tabia ya kuwategeshea wanaume zao ili wapate watoto kwa kuwaambia hicho wanachokifanya hakina utofauti na unyanyasaji hivyo wanapaswa wabadilike katika hilo jambo.

Fid Q ameeleza hayo kupitia tinga namba moja kwa vijana EATV katika kipindi cha eNewz baada ya kuwepo wimbi kubwa la wanaume kukataa kulea watoto wao kwa kisingizio cha kusema hakuwa wamejiandaa katika kipindi hicho kuwa walezi wa mtoto.

"Huo ni ukatili na dhuruma, ongea na mtu mkubaliane na siyo umtegeshee mwenzako ili upate mtoto. Maisha siku hizi ni magumu sana, watu wanaishi kwa mipango na ratiba kamili ya mwaka kwa lugha nyepesi naweza sema watu wanaishi kwa 'principal'. Kwa hiyo ushauri wangu kwa wakina dada acheni ukatili na mjitahidi kuongea na wenza wenu ili muweze kupata kile mnachostahili katika mahusiani yenu", amesema Fid Q.

Mbali na hilo, Fid Q amedai hata kama umri wake unazidi kusogea mbele na kuwa mzee hayupo tayari kukurupuka kuingia katika ndoa.

"Siyo kitu cha kukimbilia maana wanasemaga bora ukosee kazi kuliko kukosea mke wa kuoa, kwa sababu ukikosea kuchagua mke wa kuoa anaweza kukuharibia maisha yako yote. Kwa hiyo tayari nina 'idea' na mtu ambaye anafaa kuolewa na mimi chamsingi tu nawaomba mniombee dua za kheri, ili nasi tuone kama tutaweza kutimiza moja ya suna kubwa za binadamu", amesisitiza Fid Q.

Muungwana
 
Kinachosababisha wakina dada kufanya hivyo ni uvivu wa kujituma. Wadada wa aina hiyo wanapenda mseleleko, hao usiombe uwe baba wa mtoto wao hata siku moja maana shida na matatizo yake yote itabidi utatue wewe kisa anambeba mwanao
 
Kama mwanaume hataki mtoto naamini anajua kujizuia asipate. Na hapo utakuwa umewaweza ma gold digger
 
Kabisa yani. Ila mtindo huo Ndio huwa na matokeo ya wao kuishi pamoja hapo Ndio tunapata ndoa za Bahati Mbaya
 
Huyu nae sikujua kama ni hamnazo.. sasa kama maisha magumu kinachomtuma afanye ngono zembe ni nini? Condom zipo mpaka za 500. Mwisho wa siku maisha haya kama mama humuelewi kukataa mtoto ni udume suruali lea mwanao acha mwanamke akikua unamchukua sio lazima afike 18 ukitumia sheria ipasavyo. Ndo upumbavu huu mama akihustle kulea mtoto akikua unaleta sharubu..... binafsi baba angenitelekeza ningemuignore mara buku ya yeye alivyonitelekeza. Mtu unalelewa na both parents lakini bado kuna vitu vinakaza sasa waza huyo mama anakulea mwenyewe na baba yupo tu hajafa anakula good time somewhere. Hata ubini ntabadilisha ni vema ukanikana mpaka kifo chako huna tofauti na sperm donner wa sperm banks huko.
 
Back
Top Bottom