Fetishism | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fetishism

Discussion in 'JF Doctor' started by X-PASTER, Nov 4, 2009.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Nov 4, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Fetishism

  Fetishism ni maradhi anayokuwa nayo mtu aliyeelemewa na mawazo ya ngono hadi kuwa na tabia ya kupenda vitu ambavyo anavihusisha na mtu wa jinsia tofauti na yake. Kwa tafsiri finyu, mtu mwenye maradhi haya hususan mwanaume huwa na mapenzi na vitu vinavyohusiana na mtu mwingine, hususan mwanamke, kama vile nguo za ndani au hata viatu. Mtu huyu akiviona vitu hivi anaweza kuvifuga nyumbani kama ambavyo watu hufuga ndege.

  Kama ni nguo ya ndani, labda iliyosahauliwa bafuni au iliyoanikwa, au hata iliyochorwa tu kwenye picha, au iliyotundikwa dukani ikiuzwa, basi humsisimua na kumfanya katika mawazo yake kuona zaidi ya kile anachokiona wakati huo.

  Mgonjwa wa maradhi haya anaitwa Fetishist, na vile vitu vinavyomvutia vinaitwa Fetish.

  Kwa tafsiri pana, Fetishism ni maradhi ya kujawa na wazo la zinaa kwa kupitia kitu (Fetish) fulani. Ukiacha tafsiri za kwenye vitabu, ambazo zinachukulia Fetish kuwa ni nguo za ndani tu au vitu, kwa upana wake, Fetish ziko nyingi mno. Tukitoa Fetish hizi, nguo za ndani na viatu, nitaziorodhesha Fetish nyingine ambazo huwaathiri wagonjwa hawa.

  Umbile la mwili la aina fulani pia linaweza kuwa ni kivutio (Fetish) kwa Fetishist. Umbile hili ni la mwili, kwa mfano wanawake wenye maumbo makubwa hasa sehemu za makalio huwa ni Fetish nzuri sana kwa wagonjwa hawa, na ndio maana magazeti ya habari za kipuuzi na ngono ambayo sasa hivi yamejaa katika jamii yetu na yanapendwa mno na wenye maradhi haya, huwa na picha za kuchora zenye wanawake wenye makalio makubwa kupita kiasi ili picha iwe na mvuto fulani. Stara ya Hijab humsaidia mwanamke asiwe ni Fetish kwa wenye maradhi haya.

  Harufu
  : Pia inaweza ikawa ni Fetish , hususan manukato. Mara nyingi wenye maradhi haya wanaposikia harufu ya manukato inawapa hisia ya "mwanamke mzuri". Mara nyingi manukato hutumiwa na wanawake wanaopenda kujipamba wakitoka nje ili watu wawasifie au wawapende. Wanawake hawa huvaa nguo za fahari na nyingine fupi (hasa za wendawazi) na hujipaka manukato.

  Hivyo mtu anaposikia harufu ya manukato, hata kama haoni mtu, harufu hiyo humpa hisia ya wanawake walio katika hali fulani ya mvuto wa zinaa. Ndio maana wanawake wa Kiislamu huambiwa wapake kila aina ya manukato kwa ajili ya waume zao ndani, lakini wakitoka nje wanaambiwa wasijitie manukato makali, ili wasije wakawafanya watu wachemkwe kwa kupata harufu watakayoihusisha na mwanamke, hasa wale wenye maradhi katika nyoyo zao.

  Kwa wanaume wenye maradhi haya, sauti ya mwanamke pia huwa ni Fetish. Kwa kawaida sauti ya mwanamke huwa ni tofauti na ya mwanaume, kwani ya mwanamke ni nyororo. Hivyo utofauti huu humfanya Fetishist kushtuka asikiapo sauti ya mtu mke, au huburudika tu kusikia mwanamke akiongea, kulia au kuimba. Kwa tahadhari ya kuwahemsha watu wenye maradhi haya, wanawake wanaaswa kurembesha sauti zao kwa waume zao tu, na wanapoongea nje, wazikaze sauti zao, kama aya katika Qur’an tuhabarisha:

  "...basi msilegeze sauti, asije akatamani mtu mwenye maradhi katika moyo wake, na semeni maneno mazuri".
  Q33:32

  Kwa wagonjwa wengine, hata mwandiko huwa ni Fetish. Kwa kawaida, miandiko ya wanaume na wanawake huwa inatofautiana. Katika jamii yetu tumezoea kwamba mwandiko wa herufi zinazolalia kushoto ni wa kike, basi Fetishist akiwa mwanafunzi atakwambia daftari likiandikwa na mwanamke linasomeka na kueleweka vizuri zaidi. Vile vile, hawa wagonjwa hupenda marafiki wa kalamu, na wanaweka masharti kwamba rafiki huyo ni lazima awe mwanamke wa umri fulani, basi miandiko ile humridhisha, akawa hana kazi ya kufanya zaidi ya kusoma na kurudia kusoma barua za wanawake asiowajua.

  Fetish nyingine huwa ni picha, hasa za wendauchi. Wenye maradhi haya ukiingia vyumbani mwao utakuta wamebandika picha za watu waliovaa vichupi na sidiria tu. Hayo ndio mapambo waliyonayo. Pia wenye maradhi haya hupendelea magazeti ya picha za ngono (ponography), au magazeti ya upuuzi yenye manyang’unyang’u na mafindo findo na zile wanazoziita "chachandu" ili mradi maradhi haya ni kichaa cha aina fulani kilichowakumba watu wengi, wengi wao wakiwa ni wenzetu.

  Nyimbo za aina fulani pia huwa Fetish . Mara nyingi Fetishist hupenda kusikiliza na kuimba nyimbo zinazoamsha hisia za ngono. Hapa na wanawake pia wanakuwa Mafetishist . Katika jamii yetu, taarabu kwa mfano zilikuwa na nyimbo zenye mashairi mazuri yenye nasaha na maliwazo mbalimbali mazuri, lakini sasa hivi taarab imevamiwa na watu "wa kuja" ambao hawana asili na taarab, basi wamechafua taarab kwa kuingiza nyimbo za kifuska, na kwa bahati mbaya nyimbo hizo, hata redioni hazipigwi kwa ubaya wake, lakini utazikuta zinapigwa majumbani. Utamkuta mwenye maradhi kakaa anasilikiza, tena wengine na vibalaghashia vyao, anatingisha kichwa kwa raha ya wimbo wa matusi, na wanawake walio karibu, hadi mabinti wadogo nao wanaisaidia redio kaseti katika kumliwaza au kumhemsha mgonjwa.

  Sehemu ya mwili, hasa wa mwanamke, pia inaweza kuwa ni Fetish kwa wenye maradhi haya, hasa sehemu za mapaja na kifua. Hapa wenye maradhi haya hufaidi sana wanapoishi kwenye jamii yenye wendauchi. Nywele pia huwa ni Fetish ya ajabu. Utakuta wanaume wengi wa Kiafrika hupendelea nywele za Kizungu.

  Kasumba iliyojengeka miongoni mwa Waafrika malimbukeni ni kwamba kila kitu cha Kizungu ni kizuri, basi hata nywele. Kwa kujua hili, kwamba wanaume wa Kiafrika huvutiwa sana na nywele za Kizungu, ndipo wanawake wengi mno huzibadilisha nywele zao (kwa vile hufurahia kuwa Fetish Object), wakaweka dawa za ajabu ambazo nyingine huwafanya wanuke vibaya, nyingine huwanyonyoa nywele, na nywele zinaponyonyoka ndipo wanapoamua kuunganisha nywele za brashi au kuvaa manywele ya bandia (wigs).

  Ukimkuta mwanamke kavaa chupi ya mtoto ya mkojo kichwani ujue anaogopa nywele zake zikingiia maji zitaharibika na zikiharibika hawezi kuwa mteja wa Mafetishist. Mwanamke wa Kiislamu hawezi kufanywa chanzo cha starehe ya wanaume wenye maradhi ya Fetishism. Kwa hiyo huvaa hijab, inayomstiri mwili mzima, haonekani mapaja, kifua wala nywele zake. Kwa hiyo ni Uislamu tu ndio unaoweza kuleta ponyo ya maradhi haya na mengineyo.
   
 2. s

  seer Member

  #2
  Nov 6, 2009
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ungeiweka kwenye matangazo ingefit sanaaaaaaaaaaa!
   
 3. Q

  Qadhi JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2009
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Assalaam aleykum Akhiy X-Paster,
  Shukran kwa uchambuzi,binafsi nawaonea huruma sana hawa wanawake kwa taabu wanazojipa kisa wapendeze mbele ya wanaume tena ambao hata si halali yao,kila kukicha ku compete na fashion.Na siku hizi sehemu za kukaa wazi kwao zimeongezeka na ndivyo gharama za kuziremba hizo sehemu zinavyoongezeka.
  Imagine high-heeled shoes,dieting hadi kupata anorexia nervosa(Jay Lo,Mariah Carey....cjui nimepatia hayo majina,nakusudia maria keli),cosmetics,plastic surgery etc,ni taaabu tu kwenda mbele.Nakuja kuamini kuwa ni kweli mwanaume ni kiongozi wa mwanamke na lazima watatii kile wanaume wanataka/wanapenda.....,wamewalaghai wanawake kwa lugha ya kuwakomboa,kuwaweka huru n.k,kumbe jamaa wanataka wasipate taabu wanapohitaji kuridhishwa nafsi zao.Maua ya kuriwadha macho yao si lazima wayafuate bustanini,kila kona na kila mtaa yanajitembeza yenyewe tena ya kila namna na kila rangi,,natural,mkorogo...
  Rivert/convert muslim sisters wote wanasema miongoni mwa vitu wanavyoshukuru kuwa waislam ni kuepukana na psychopathology kutokana na kuwaza atoke vipi...,mostly wanatumia neno" now I'm judged by my brain rather my the length of my leg,the colour of my G-string..."

  Najiuliza sana hivi inakuwaje mwanaume rijali unaona si tatizo mkeo kujiremba na kwenda ofisini,sokoni,kwenye vikao....akijiremba anakuwa attractive,anavutia wanaume wengine..imekaaje hii sasa wazee,?,,,Grrrrrrriiiii

  Mtu asiyekuwa na wivu(including kuona kawaida mkeo awavutie kimapenzi wanaume wengine) in islam aitwa duyuth,na mafikio akhera ni mabaya,kwa sababu anaweza kuacha mianya ya zinaa.

  Alamsik
  Qadhi
   
 4. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  duh kazi ipo!
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Nov 8, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Matangazo tena...!?
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Nov 8, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160

  Wa Alaikum Salam wa rRahmatullahi wa Barakatuh


  Sadakta ya akhii Ndugu yangu Qadhi, shukran kwa mchango wako, maneno yako ni kweli kabisa. Lahiti wanawake wengi wangeusoka Uislamu na kutambuwa kuwa umekuja kumkomboa mwanamke kwa kumpa heshima 'adhiymu' japo makafiri hawalitaki ilo kabisa kwani kama ulivyosema hapo juu namna na itikadi za kimagharibi wanavyomfanya kuwa ni kinyago kwa kumtoa mbele ya matangazo ya biashara huku asilimia 90% kama si 99% ya faida hiyo ikiingia kwao hao wenye maradhi ya kupenda kuona nyuchi za wanawake.

  Hii yote imetokana na binaadamu kugandana mno na pumbazo za dunia. Hata kama wakipatiwa ukumbusho huukana na kufanana na mbwa ambaye akipigiwa ama asipigiwe kelele, yu-ahema tu. Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:

  Na kama Tungelitaka Tungelimnyanyua kwazo, lakini yeye aligandamana na ardhi (kutaka ukubwa wa kidunia akayatupa ya Akhera) na akayafuata matamanio yake.
  Basi hali yao ni kama hali ya mbwa; ukimpigia kelele (hukimbia na huku) anahema, na ukimwacha pia huhema. Hiyo ndiyo hali ya watu waliozikadhibisha Aya Zetu.
  Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari.

  Suratul-A’araaf: 176

  Kumekuwa na mitindo ya kutetea haki za wanawake kwa minajili ya kumtoa mbele ya kadamnasi bila ya kuangalia athari zake kimaadili na ubinaadamu. Kwa kisingizio hicho ndio tunapata haya mashindano ya urembo ambayo kwa hakika kabisa hayaendani na maadili yetu.

  Ushiriki wa wanawake kwenye nyanja hizi za urembo umeshuhudiwa kuwa na matokeo ya upotofu wa maadili na tabia mbovu kabisa za uzinzi. Ajabu kubwa, wanapohojiwa wanaeleza ya kwamba; mashindano ya urembo ni kipaji tu cha kazi kama zilivyo kazi nyingine! Jibu hilo laenda sambamba na wanamuziki. Wakisema kuwa kazi hizo sio uhuni na yafaa kwa vijana kushiriki kwa bidii zote. Jee, wataka tueleza ya kuwa kuvaa miniskirt na kaputula kwa mwanamke na kusuka na kutoga masikio kwa mwanamume sio uhuni? Mwanamume aliye jamadari mzima akivaa vidani na mapete mithili ya mwanamke ni sawa? Iwapi tofauti yao ya jinsia?

  Mwanamke wa Kiislamu ametukuzwa kwa kuwekewa kanuni maalum za kivazi ili asipotoshwe na jamii. Mwanamke wa Kiislamu hatakikani kuwa na uchu wa urembo nje ya kuta za mumewe na Mahariym wake. Badala yake, mwanamke anasukumwa mbele ya kioo cha saluni kwa dakika zisizopungua 120 huku ameridhika kuumbuliwa kwa kutolewa nyusi na kuchongwa meno. Baada ya hapo, kinachofuatia si chengine ila ni fitnah kwa wavulana waliopo vibarazani na kuwaingiza kwenye dimbwi la zinaa. Wanawake wengine wanaotoa miguu hapo saluni hupata hasara ya kuvutwa kushiriki kwenye mashindano ya urembo akidhani ni bahati nzuri kwake. Atatolewa mbele ya kadamnasi amevaa mithili ya mtu aliyekosa akili. Lengo kuu la kushiriki hayo mashindano sio chochote ila ni kupata macho ya watu, kujiuza kwa bei rahisi, umaarufu na tunuku.

  Huenda huyo mshiriki asiwe na athari za moja kwa moja, lakini jamii inaachiwa kovu baya kabisa na mabomu ya kuwapotoza vijana kujiingiza kwenye dimbwi hilo huku wakisaka hizo fedha na bahati mbaya ni wachache mno wenye kufikia huko aliyeshinda mshindi. Athari ya mambo haya sio ngeni kuziorodhesha kwa jamii yetu. Kwani tunashuhudia ongezeko la mimba zilizo nje ya ndoa, utoaji wa mimba kwa wanafunzi, ubakaji, wizi na mengineyo.


  Dawaam wa dawaam tuelewe kwamba, tutakuwa ni wenye kukhasirika kwa kukosa kufuwata mwongozo wa Mwenyezi Mungu.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Brothers Qadhi na X-Paster, salaam na amani iwe kwenu!!

  Paster umeleta mada kwa JF doctor, lakini naona kama inakuwa ngumu kuichangia kwani tayari mmeshaelekeza nguvu ule upande wa dini na mmenukuu aya' za kule sasa tunashindwa hata kuelewa tuchangiaje; kwa kurejea vya maandiko au kwa kurejea mabuku ya medicine na saikolojia?

  Mwongozo tafadhali!
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Nov 8, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu unaruhusiwa kuchangia vile unakavyoweza aidha kwa Kutumia reference za kitabibu au za kidini (Islam, Chistian, Jewish, Hinduism n.k).

  Basi ndugu yangu jisikie huru, kuchangia vile utakavyoweza...!
   
Loading...