Festo Sanga: TANESCO imezidiwa, 'Man Power' yao ni ndogo, ziwepo Taasisi 3 zinazosimamia suala la umeme

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,876
12,129

Tunapozungumza leo, uwekezaji uliopo nchini wa viwanda na migodi (Mfano Mgodi wa Geita kwa siku moja unatumia umeme wa Mkoa mzima wa Njombe, huo ni mgodi mmoja tu je tuna migodi mingapi?, hapo hatujazungumzia Viwanda na matumizi binafsi).Vilevile namna serikali ilivyosambaza kwa ukubwa Umeme vijijini (REA) zaidi ya Vijiji elfu 11 vimefikiwa na umeme kati ya Vijiji elfu 12 vyote nchini, ni wazi TANESCO lazima izidiwe na isaidiwe.

Mapendekezo yangu ni kuwa, huu ni wakati sahihi wa kuwa na mamlaka/walaka ya Uzalishaji -Generation(kufua umeme),wakala/mamlaka ya kusafirisha (Transmission) umeme (Gridi ya Taifa na gridi zingine) na wakala/mamlaka ya Kusambaza umeme (Distribution).

Mitambo ikizimika, gridi ya Taifa ikipata shida, Mwananchi asipoingiziwa umeme, mita zisipopatikana kwa wakati, nguzo ikianguka, umeme ukiwa low voltage,Mzigo wote huu unaelekezwa TANESCO.

Ukiangalia nguvu kazi ya TANESCO, bajeti yao, uhaba wa ofisi na vitendea kazi kwenye ngazi ya wilaya n.k ni wazi muhimu kuangalia namna ya kuisaidia TANESCO.

Mfano mzuri wa Usambazaji (distribution) uliofanyika hivi karibuni na kuwafukiwa wananchi wengi ni uwe wa REA nchini, umeme umewafikia watu wengi kwa muda mfupi. Je hatuoni kufanya hivyo kwenye Uzalishaji na usafirishaji kuwa na shirika au mamlaka zinazohusika?

Maoni yangu kwa Taifa langu Mama Tanzania.

Festo Richard Sanga
Mb-Makete
 
Tunapozungumza leo, uwekezaji uliopo nchini wa viwanda na migodi (Mfano Mgodi wa Geita kwa siku moja unatumia umeme wa Mkoa mzima wa Njombe , huo ni mgodi mmoja tu je tuna migodi mingapi?, hapo hatujazungumzia Viwanda na matumizi binafsi).Vilevile namna serikali ilivyosambaza kwa ukubwa Umeme vijijini (REA) zaidi ya Vijiji elfu 11 vimefikiwa na umeme kati ya Vijiji elfu 12 vyote nchini, ni wazi TANESCO lazima izidiwe na isaidiwe.

Mapendekezo yangu ni kuwa, huu ni wakati sahihi wa kuwa na mamlaka/walaka ya Uzalishaji -Generation(kufua umeme),wakala/mamlaka ya kusafirisha (Transmission) umeme (Gridi ya Taifa na gridi zingine) na wakala/mamlaka ya Kusambaza umeme (Distribution).

Mitambo ikizimika, gridi ya Taifa ikipata shida, Mwananchi asipoingiziwa umeme, mita zisipopatikana kwa wakati, nguzo ikianguka, umeme ukiwa low voltage,Mzigo wote huu unaelekezwa TANESCO.

Ukiangalia nguvu kazi ya TANESCO, bajeti yao, uhaba wa ofisi na vitendea kazi kwenye ngazi ya wilaya n.k ni wazi muhimu kuangalia namna ya kuisaidia TANESCO.

Mfano mzuri wa Usambazaji (distribution) uliofanyika hivi karibuni na kuwafukiwa wananchi wengi ni uwe wa REA nchini, umeme umewafikia watu wengi kwa muda mfupi. Je hatuoni kufanya hivyo kwenye Uzalishaji na usafirishaji kuwa na shirika au mamlaka zinazohusika?.

Maoni yangu kwa Taifa langu Mama Tanzania

Festo Richard Sanga
Mb-Makete
Mawazo ya watu wavivu haya. Ni kama yale ya kugawa mikoa au wilaya kila kukicha. Tatizo la Tanzania liko kwenye utendaji na siyo kwenye ukubwa wa mashirika. Hivi kukiwa na wakala wa uzalishaji kukiwa na ukame akakojoa hiyo mvua? Si mara kwa mara huwa wanasema tatizo la umeme linatokana na ukame? Kwani wanashindwa nini kuweka hizo idara hata kama Tanesco itabaki kuwa moja?
 
Huu ni uvivu wa kufikili yani kuongeza taasisi.kwani Tanesco walisema umeme kukatika shida ni kuwa taasisis ya ni kubwa sana.mbona hawa wabunge wanafanya vitu tofauti kabisa na shida iliyopo.
Na haya mapendekezo yanatakiwabkutoka kwa wataaramu husika sio wanasiasa.
Ni uvivu wa kufikili kabisa.
 
Back
Top Bottom