Yanga ijifunze kutokana na mkwamo wa simba

Jbst

JF-Expert Member
Nov 29, 2020
1,922
3,951
Makala hii nimeitoa lwa abas mwalimu,nimeileta hapa ili wote tujifunze.nililua namuona Mo tapeli baada ya kusoma hii makala nimepata elimu na sina neno kanjbhai

YANGA IJIFUNZE KUTOKANA NA MKWAMO WA SIMBA

Na Abbas Mwalimu
0719258484

Jumanne tarehe 27 Disemba 2022.

Klabu ya Yanga ipo kwenye mchakato wa usajili wa wanachama wake kwa njia ya kidigiti.

Usajili wa wanachama ni muhimu sana katika kutoa tafsiri ya kiasi cha uwekezaji kwa klabu hiyo.

Umuhimu huo unakuja kutokana na sintofahamu ambayo imewakumba baadhi ya mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba.

Ifahamike kuwa bado kuna fukuto kubwa la sintofahamu juu ya uwekezaji wa mfanyabiashara maarufu na mwekezaji katika klabu ya Simba ndugu Mohammed Dewji maarufu kwa jina la MO.

Hivyo nao Yanga wanapaswa kuwa makini sana ili kuepuka sintofahamu hii.

Inafahamika kuwa uwekezaji wa MO katika klabu ya Simba unapitia kampuni yake ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited kwa kifupi MeTL.

Baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba wamekuwa wakihoji juu ya kiasi cha Shilingi Bilioni 20 za Kitanzania ambazo MO aliahidi wakati anaingia kuwekeza Simba.

Yanga wanapaswa kuwa makini yasije kuwakuta maswali haya.

Niliwahi kuandika makala tarehe yenye kichwa cha kifuatacho tarehe 18 Juni 2019:

'SIMBA MLIMUELEWA MO KUHUSU PRICE TO EARNINGS RATIO?'

Kwa bahati mbaya inaonekana wanachama, wapenzi na washabiki wa klabu hiyo hawakumuelewa MO pindi alipogusia ni nini Price to Earnings Ratio.

Hili la Price to Earnings linaweza kuwaathiri wanachama wa Yanga pia wasipokuwa makini.

Kwa maoni yangu, nitajaribu kufafanua maana ya Price to Earnings Ratio kwa kutazama changamoto ya uwekezaji katika klabu ya Simba. Nitazingatia zaidi mahojiano aliyowahi kufanya Mo na Voice of America (VoA).

Hoja hii ni muhimu pia kwa klabu ya Yanga ingawa wengi hawaipi umuhimu kwa sasa.

Kwenye ile clip iliyozagaa mitandaoni wakati ule ilimuonesha Mo akizungumza na waandishi wa habari kwenye kipande kilichorekodiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya America (VOA Swahili) Mo alisikika akisema maneno yafuatayo, ninayanukuu:

"Ishu yangu ni 20 Billion brother tusifanye masihara eeh! Unajua 20 billion naweza kununua bank! Acha ngoja nikwambie value of the club. Nenda kafanye valuation hata kwenye balance sheet yao wanaonyesha value ya majengo ni billion 3.8 billion 4. Brother ngoja nikwambie-trademark, unajua kwenye biashara ukitaka kununua biashara kuna kitu ambacho kinaitwa Price to Earnings Ratio ndiyo nini? Ngoja niwape somo kidogo." Clip ile iliishia hapo.

Kutokana na hapo alipoishia Mo kwenye somo Price to Earnings Ratio nami nimeona si vibaya nikapaendeleza ili walau watu tuweze kuelimika.

PRICE TO EARNINGS RATIO NI NINI?

Gibson (2008:339) katika kitabu chake "Financial Reporting and Analysis. Using Financial Accounting Information" amefafanua Price to Earnings Ratio kwa kueleza yafuatayo:

"Price to Earnings Ratio is a ratio that expresses the relationship between the market price of a share of common stock and that stock's current earnings per share."

Kwa maana nyingine ni kwamba "The price to earnings ratio (P/E) is the ratio for valuing a company that measures its current share price relative to its per share earnings (EPS)."

Kwa tafsiri ya jumla ni kwamba:

Price to Earnings Ratio (P/E) ni uhusiano kati ya thamani ya soko ya bidhaa kwa ujumla kwa kulinganisha na mapato ya wakati uliopo ya bidhaa husika kwa hisa.

Kwa maana nyingine ni kwamba P/E inalenga kutazama ni kiasi gani cha pesa ambacho mwekezaji anaweza kuwekeza katika kampuni ili kupata shilingi moja ya mapato ya ile kampuni kutokana na uwekezaji huo.

Kanuni hii ya uwiano ilipata umaarufu kutokana na kuelezwa vema na Benjamin Graham ambaye alikuja kuitwa " Baba wa Uwekezaji wenye Tija" yaani 'Father of Value Investing.'

Benjamin Graham ndiye aliyemjengea ushawishi mkubwa Warren Buffet kuingia katika biashara.

Price to Earnings Ratio hupimwa kwa kuchukua mapato yote ya jumla ya kampuni kabla ya kutoa gharama nyingine dhidi ya thamani ya bidhaa katika soko kwa wakati huo.

Mfano wa Price to Earnings Ratio katika uwekezaji wa Mo kwa Simba linaweza kutafsiriwa hivi:

Mfano tujaalie kuwa klabu ya Simba iliripoti mapato yake yote ya jumla kwa mwaka 2018/2019 kuwa ni bilioni 2.

Mapato yote ya jumla kwa lugha ya kingereza huitwa 'basic or diluted earnings per share.'

Thamani ya bidhaa iliyo katika nyaraka yaani documented (siyo ya ile mdomoni) kwa mujibu maelezo aliyowahi kutoa Mo ni bilioni 4.

Kwa haraka hapo Price to Earnings Ratio itakuwa 2.

Yaani P/E=Market Value of the Club per share/Basic ama Diluted Earnings per share

Hivyo utachukua bilioni 4 utagawa kwa mapato ya bilioni 2 iliyopata club kwa mwaka.

Kwa mantiki hiyo uwekezaji katika klabu husika hauwezi kuzidi shilingi bilioni 2 za Kitanzania. Hiyo ni kwa mujibu wa hesabu P/E=Market Value.

Wakati wa mahojiano yale wakati ule walisikika baadhi ya waandishi wakimuuliza Mo kuhusu 'Thamani ya Brand ya klabu ya Simba' lakini je hiyo thamani ya klabu ilifanyiwa valuation na taasisi kama Price Water Coopers au Delloite kuona kuwa brand ya Simba ina thamani gani na ikawa documented?

Hivyo, suala la thamani ya klabu linapaswa kutazamwa kwa umakini na klabu ya Yanga ili wasije kukwama kwenye kupata thamani halisi ya klabu.

Ifahamike kuwa biashara ya uwekezaji hutazamwa kwa kitu kilichoelezwa kwenye nyaraka (Documents au Balance sheet) hivyo kama suala la brand halijatafsiriwa vizuri linaweza kuleta utata kwa klabu ya Yanga baadae.

Changamoto hii ya thamani ya klabu imewakuta watani wa Yanga kwa kuwa kitu ambacho kimo kwenye balance sheet ni thamani ya majengo na si brand ya klabu kama alivyowahi kubainisha Mo.

Kwa muktadha huo na kwa mujibu wa kanuni ya Price to Earnings Ratio si rahisi kimahesabu kwa Mo kuwekeza bilioni 20 kwa pamoja (at once) katika kampuni yenye thamani ya bilioni 4 na mapato ya bilioni 2?

Kwa klabu ya Yanga, je wanachama wanauona ukweli huu mchungu? Tukumbuke Mo ni mfanyabiashara msomi na hili somo la investment analijua vema sana. Ndiyo maana katika clip alisikika akisema 'Ngoja niwape darasa kidogo.' Huyu ni mtaalamu wa biashara kutoka Harvard. Hivyo wanayanga nao wanapaswa kulitazama hili kwa uzito wa pekee.

Damodaran. A (2002) katika kitabu chake "Investment Valuation: Tools and Techniques for Determining the Value of Any Asset" anaeleza kuwa, sababu ya wawekezaji kuwekeza ni kwamba wawekezaji hutarajia ukuaji mkubwa wa kampuni huko baadae na kama hawaoni dalili za ukuaji hupata tabu kufikiri kuhusu kuwekeza katika kampuni husika.

Huenda hili ndilo linalomsumbua Mo kichwani mwake akitafakari kuwekeza bilioni 20 katika klabu yenye thamani ya bilioni 4. Huenda pia likaja kuwakabili Yanga wasipokuwa makini hapo baadae.

Kwa mujibu wa Damodaran (2002) ni kwamba ili Simba imvutie Mo zaidi ni lazima iwe na uwezo wa kushiriki ligi ya mabingwa kila mara na kuchukua kombe hili hapo mapato yataongezeka na growth (ukuaji) itaonekana. Yanga nayo inapaswa kupita njia hii ili kuongeza mapato.

Lakini kwa upande wa Simba, jambo moja ambalo nadhani wanamsimbazi wanapaswa kufahamu ni kuwa katika suala la uwekezaji wa Mo wanazungumzia watu wawili.

Mtu wa kwanza ni Mohammed Dewji mwenyewe huyu ni mtu wa asili (natural person) na pili Mohammed Dewji Enterprises Limited (METL) huyu ni mtu wa kisheria (legal person). Kibiashara hawa ni watu wawili tofauti.

Wale waliosoma Accounts na Business Law nadhani watakuwa wanakumbuka zile General Accepted Accounting Principles kwa kifupi GAAP yaani kanuni za kiuhasibu zilizokubalika kwa pamoja. Hizi ni kanuni za kiuhasibu zilizokubalika na taasisi takribani zote za kiuhasibu duniani.

Kuna kanuni mojawapo katika GAAP inasomeka kama "The Business Entity Concept" ambayo inaeleza kuwa "Mfanyabiashara na biashara ni vitu viwili tofauti"

Mfanyabiashara ni mwanadamu yeye kisheria huitwa 'natural person' halafu kuna biashara nayo ambayo kisheria hutambulika kama mtu wa kisheria yaani 'legal person' hivyo basi kibiashara kuna mtu anaitwa 'MO' na kuna mtu anaitwa 'METL'

MO ana mikono, miguu, masikio, mdomo, pua, macho ,ulimi n.k kwa upande wake huyu METL ana pesa nyingi sana na rasilimali nyingine kibao lakini hana macho, masikio, mdomo wala pua. Yeye anamtegemea Mo kuona,kunusa,kusikia,kusema n.k.

Aidha, MO ni CEO kwenye makampuni ya METL Group hivyo kinakununi anakosa nguvu kwenye baadhi maamuzi mbele ya Bodi ya Wakurugenzi (Board of Directors) hasa yanayohusu fedha. Sijui kama hili linafahamika kwa watu wengi. Kwa upande wao Yanga nao inapaswa walitazame hili kwa kina.

Hivyo basi kwa upande wake Mo anapotaka pesa ni lazima amuombe METL. Kama kwa METL ratio za kuwekeza bilioni 20 zinakataa hawezi kumpa Mo hizo bilioni. Hapa ndipo wengi tunaposhindwa kuelewa.

Hii ina maana mbili. Mosi, ni maamuzi ya bodi ya wakurugenzi kama utaratibu wa uongozaji makampuni ulivyo duniani.

Ndiyo maana inasemekana kuwa fedha zinazoelezwa kuwa ni bilioni 20 za uwekezaji, zimewekwa katika akaunti ya muda maalumu (Fixed/Term Deposit) kama walivyopata kunukuliwa baadhi ya viongozi wa klabu wakati fulani.

Pili, kutokana na ukweli kwamba kanuni za kimahesabu zinagoma kuwekeza bilioni 20 katika biashara yenye mtaji wa bilioni 4.

Hivyo, ililazimu kuweka fedha hizo katika akaunti ya muda maalumu (fixed deposit) ili kupata faida ambayo ndiyo inaweza kutumika kama uwekezaji mbadala.

Hili wale wenzangu tuliofanya kazi benki watakuwa wananielewa vizuri.

Bila shaka watu wa benki wanakumbuka pia kuwa kwa kawaida uwekezaji katika mtaji wa biashara hufanyika kwa kiasi kisichozidi asilimia 70 ya mtaji uliopo. Hapa watu yafaa wajiulize, asilimia 70 ya Bilioni 4 ni kiasi gani?

Yanga wanapaswa kulitambua hili pia.

Kwa bahati mbaya sana hata mitaani kwetu watu wengi hatujui kanuni hizi.

Kwa mfano, utakuta mtu ana duka lake halafu hapo hapo familia ikitaka unga anawapimia bila ya kupatiwa pesa, anashindwa kuelewakuwa kibiashara yeye na hiyo biashara ni vitu viwili tofauti. Anapaswa kununua kama wanavyonunua wengine.

Mo kwa upande wake ni mfanyabiashara nguli na msomi, anaifahaku kwa kina hii 'Business Entity Concept'.

Kwa kuthibitisha hilo tazama ile video clip ambayo alizungumza na waandishi wa habari kwa makini utaona vitu viwili.

Kwanza utamuona Mo anayesema "Ishu yangu ni 20 billion brother..." halafu tazama kwa mbele kwenye upande wake wa kushoto utaona kitu kimesimamishwa mezani kimeandikwa METL huyu ni mtu wa pili ambaye wengi hatumuoni.

Kwa ufupi "Price to Earnings Ratio" inagoma. Kanuni ya biashara inagoma kukubaliana na matakwa ya Mo kwa kuzingatia mazingira yaliyopo sasa labda kwa baadae sana jambo ambalo kwa mujibu wa price to earning ratio wanasimba hawalielewi. Je Yanga wataelewa?

Kwake MO ishu kubwa kwake ni 'thamani ya klabu' "value of the club" ambayo ipo kwenye nyaraka za Simba zilizothaminiwa, kimahesabu (ya darasani).

Thamani ya klabu iliyopo kwenye nyaraka haiwezi kuendana na uwekezaji wa Bilioni 20.

Je Yanga wanaona umuhimu wa kubainisha thamani ya klabu kwa uweledi mkubwa ili kuepuka mkwamo huu?

Mdomoni Mo anaweza kuweka mzigo wa bilioni 20 lakini technically amekwaa kigingi kwa sababu kanuni ya value investing ya Benjamin Graham inagoma.

Si rahisi kuwekeza Bilioni 20 kwa mkupuo kwenye klabu yenye thamani ya Bilioni 4, kikanuni hesabu hazikubali. MO anaongozwa na hesabu si utashi wake hilo watu wanapaswa wafahamu. Vivyo hivyo hata wawekezaji wa Yanga wanaongozwa na hesabu na si utashi au mapenzi yao tu, wanayanga ni lazima watambue hili.

Kwa Yanga lipo la kujifunza hapa wasije wakakwama.

Ndiyo maana Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said ameona ili kuipa thamani klabu kabla ya kuleta wawekezaji basi ni lazima wajenge uwanja.

Uwanja utaipa Yanga faida mbili, mosi wenyewe utakuwa ni asset ambayo itakuwa sehemu ya thamani ya klabu. Pili, mapato yatokanayo na washabiki yatakuwa sehemu ya thamani ya klabu kwa maana ya uwezo wa biashara kuzalisha. Ni lini mradi utakamilika hilo ni suala la uongozi wa klabu.

Lakini jambo muhimu na njia ya mkato kwa Yanga kukwepa mkwamo walioingia Simba ni kupitia usajili wa wanachama.

Kama wanayanga wanatambua umuhimu wa kile alichoeleza Mo basi wanapaswa wajisajili kwa wingi ili thamani halisi ya klabu ionekane kwenye fedha zitakazokusanywa kutokana na usajili wa wanachama hao.

Vinginevyo watakuja kulalamika kama ambavyo mashabiki na baadhi ya wanachama wa Simba wanavyolalamika hivi sasa.

Hivyo ni lazima Yanga ijifunze kutokana na mkwamo huu wa Simba na hasa kwa mashabiki kujisajili kwa wingi ili baadae wasije kulalamika.

Asanteni.

Wenu:

Abbas Mwalimu (Facebook|Instagram|Twitter|Clubhouse)

+255 719 258 484

Uwanja wa Diplomasia (Facebook|WhatsApp)
 
Mimi katika yote uliyoeleza, shauku yangu ni kuona uwanja wa kuchezea mechi na pia mazoezi + hostel ya wachezaji vinajengwa kule Kigamboni, kama tulivyoahidiwa na viongozi wetu.

Kiukweli sijisikii poa hata kidogo pale ninapoona vilabu vichanga kabisa kama Azam, Ihefu, Namungo, Geita Gold, nk. Vinamiliki viwanja vyao! Jambo hili halikubaliki hata kidogo.
 
Hii umeiweka kisomi na ki layman ili wote waelewe.

Mm nimeelewa kwamba una genge la mboga nje ya nyumba yako. Unapata hela 10 milioni unaenda kuwekeza hela hizo zote kwenye hilo genge ili uwe unapata faida kwa kushaeishiwa na watu kwamba hili genge lako la mbiga ni maarufu sana mtaani hapa na linapendwa na watu. Ni kichekesho kwa kweli.
 
Mkuu me ni yanga, nilikua namuona Mo kama ana watapeli simba..nilikua namuona Mo kama mswahili fulani anayeitumia simba tu.

Baada ya hii makala nimegundua MO anaendesha mambo kisomi na hafanyi mambo kufurahisha watu
 
Haswaa! Sio ww tu hata mm nimeelewa hili sakata toka kwenye makala hii. Nilkua naskia "thaman ya club, brand ya Simba, B20,...... n.k" nkawa sielewi kinachozungumzwa.

Basi kama ni hivyo Mo hana kosa. Sasa msomi Dokta Kigwangala haelewi hii concept?
 
Huwezi kujua thamani ya kitu bila kufanyiwa tathimini
Simba hawakuwahi kufanyiwa tathimini ya thamani yao .
Mali za Simba ni jengo ,, viwanja vya Bunju na fanbase yao na hata wajumbe wa mchakato wa mfumo Simba wanakiri kuwa waliendesha mchakato bila kujua thamani halisi ya Simba lakini mo alijua ni kitu Gani amelenga ndio maana alitamka kununua hisa 51 Kwa bilioni 20 na serikali iliposema vilabu vinatakiwa kuuza hisa 49 pesa yake haikubadilika lakini alikuwa mkali pale Azam walipotaka kuweka bilioni 40 Kwa miaka 10 kuwa ni ndogo kulinganisha na thamani ya brand ya Simba.

Kama Simba ingehusisha wataalamu wa uhasibu na soko la mitaji na uwazi Simba ingekuwa ya kisasa zaidi na Wala kusingekuwa na ugomvi wa hati ya jengo
 
Uzi una madini sana huu. Si kwa football pekee bali kibiashara na uwekezaji kwa ujumla. Kongole Mkuu, umeitendea haki professional yako!
 
Hii umeiweka kisomi na ki layman ili wote waelewe.

Mm nimeelewa kwamba una genge la mboga nje ya nyumba yako. Unapata hela 10 milioni unaenda kuwekeza hela hizo zote kwenye hilo genge ili uwe unapata faida kwa kushaeishiwa na watu kwamba hili genge lako la mbiga ni maarufu sana mtaani hapa na linapendwa na watu. Ni kichekesho kwa kweli.
Nimeshindwa kucheka!
Kwa hiyo mlinganyo kati ya Simba na bilion 20 ni sawa na genge la mboga mboga mtaani na milioni 10.
 
Hii umeiweka kisomi na ki layman ili wote waelewe.

Mm nimeelewa kwamba una genge la mboga nje ya nyumba yako. Unapata hela 10 milioni unaenda kuwekeza hela hizo zote kwenye hilo genge ili uwe unapata faida kwa kushaeishiwa na watu kwamba hili genge lako la mbiga ni maarufu sana mtaani hapa na linapendwa na watu. Ni kichekesho kwa kweli.
Nimeshindwa kucheka!
Kwa hiyo mlinganyo kati ya Simba na bilion 20 ni sawa na genge la mboga mboga mtaani na milioni 10.
 
Huwezi kujua thamani ya kitu bila kufanyiwa tathimini
Simba hawakuwahi kufanyiwa tathimini ya thamani yao .
Mali za Simba ni jengo ,, viwanja vya Bunju na fanbase yao na hata wajumbe wa mchakato wa mfumo Simba wanakiri kuwa waliendesha mchakato bila kujua thamani halisi ya Simba lakini mo alijua ni kitu Gani amelenga ndio maana alitamka kununua hisa 51 Kwa bilioni 20 na serikali iliposema vilabu vinatakiwa kuuza hisa 49 pesa yake haikubadilika lakini alikuwa mkali pale Azam walipotaka kuweka bilioni 40 Kwa miaka 10 kuwa ni ndogo kulinganisha na thamani ya brand ya Simba.

Kama Simba ingehusisha wataalamu wa uhasibu na soko la mitaji na uwazi Simba ingekuwa ya kisasa zaidi na Wala kusingekuwa na ugomvi wa hati ya jengo
Haujasoma ukaelewa hii makala mkuu,, simba wao ktk documents au balance sheet yao inaonesha thaman ya club yao kama makala ilivoeleza.

Alafu pia makala imeeleza hata yanga wanaweza kuingia mkenge na wasipate thaman halisi ya club yao kama hawatotimiza mambo ya msingi kama kuwa na uwanja na kusajili wanachama wao kwa wingi.

Alfu pia hakuna muwekezaji anaeweza kuja kuwekeza kama unavofikiria, yeye atataka documents zinazoonesha mtaji wa kampuni na thaman na sio kujisemea tu ya mdomoni.

Kosa la Mo ni lipi kama simba wao walionesha ktk documents zao thaman yao ni bilion 3.8!! Soma hiyo makala vzr mkuu.
 
Mimi katika yote uliyoeleza, shauku yangu ni kuona uwanja wa kuchezea mechi na pia mazoezi + hostel ya wachezaji vinajengwa kule Kigamboni, kama tulivyoahidiwa na viongozi wetu.

Kiukweli sijisikii poa hata kidogo pale ninapoona vilabu vichanga kabisa kama Azam, Ihefu, Namungo, Geita Gold, nk. Vinamiliki viwanja vyao! Jambo hili halikubaliki hata kidogo.
geita gold watoe kwenye hiyo orodha hawana kiwanja chochote. kile ni kiwanja cha h/shauri.
 
Haujasoma ukaelewa hii makala mkuu,, simba wao ktk documents au balance sheet yao inaonesha thaman ya club yao kama makala ilivoeleza.

Alafu pia makala imeeleza hata yanga wanaweza kuingia mkenge na wasipate thaman halisi ya club yao kama hawatotimiza mambo ya msingi kama kuwa na uwanja na kusajili wanachama wao kwa wingi.

Alfu pia hakuna muwekezaji anaeweza kuja kuwekeza kama unavofikiria, yeye atataka documents zinazoonesha mtaji wa kampuni na thaman na sio kujisemea tu ya mdomoni.

Kosa la Mo ni lipi kama simba wao walionesha ktk documents zao thaman yao ni bilion 3.8!! Soma hiyo makala vzr mkuu.
Wewe ndio hujaelewa soma uelewe kama waliosimamia mchakato wanamsema hawafahamu thamani ya club ya Simba hiyo iliyowekwa kwenye balance sheet wameipata wapi?
Au nikuulize swali kingine unijibu Mo alitaka kununua hisa za Simba asilimia 51 Kwa billion 20 lakini serikali iliposema vilabu kama Simba na yanga vinaruhusiwa kuuza hisa zao asilimia 49 Mo alitoa ofa ileile ya billion 20 kama thamani ilikuwa kwenye balance sheet kwanini thamani ya hisa 49 na 51 zilingane? Naomba unijibu
 
Baada ya Mo kutoa offer ya bil 20 kununua hisa 51%, watu wa simba walipinga wakasema ni hela ndogo haiendani na thaman halisi ya simba.

Mo alikua akimjibu mwandishi aksema" bilion 20 naweza kununua bank" nenda pale simba wakuoneshe balance sheet yao thaman ni biliom 3.8... sasa nikuulize ww walipoombwa balance sheet ili muwekezaji ajue thaman yao hizo documetns ziliandikwa na nani? Maana unasema walikua hawajui.

Kwahyo simba ilijua Muwekezaji akija watamwambia tu simba ina thaman ya bilion 100 kwa mdomo na yeye atakuabali? Hakuna muwekezaji wa hivo duniani.

Kuhusu kwann Mo hakubadili offer baada ya serikali kusema simba na yanga wanatakiwa kuuza hisa zisizozidi 49% kwa muwekezaji hayo yalikua ni maamuzi na Mo mwenyewe ndo mwenye pesa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom