Fei Toto kukata rufaa rasmi CAS aomba mchango wa pesa kwa Watanzania

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Aliyekimbia mshahara wa mil 4 anawaomba walala hoi wa instagram wamchangie pesa za kupeleka kesi CAS;

===

1685046037143.png

Picha: Feisal Salum (Fei Toto)

Feisal Salum katika ukurasa wake rasmi wa Instagram ameandika ujumbe ufuatao:

Ndugu zangu Watanzania na familia yote ya soka kwa Bara na visiwani. Mimi kijana wenu ambaye kwa miaka yote nimekua na nidhamu nje na ndani ya uwanja na kwa dhati nimeitumikia klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania na Zanzibar Heros.

Utiifu wangu umekua shubiri ya maisha yangu ya soka, nimevumilia nimeshindwa, sitamani tena mama yangu kutukanwa. TFF imeshindwa kunisaidia kupata haki yangu ya Kuvunja mkataba na Yanga hivyo nimeamua Kwenda Mahakama ya michezo CAS.

Nahitaji Mchango wa kila Mtanzania mpenda haki na maendeleo ya wachezaji wa Kitanzania ambao wamekua kimya na woga juu ya maslahi, Heshima na Haki zao. Naomba unichangie kadiri utakavyoweza ili niweze kupata pesa ya Kulipia gharama za kufungua Jalada la kesi yangu CAS ili kupata Haki yangu ya Kuondoka Yanga kwa kuvunja mkataba.

Tafadhali naomba unichangie ili nipate haki yangu itakayoniwezesha kutumikia kipaji changu na Timu za Taifa (Tanzania na Zanzibar) katika namna tofauti kwa manufaa yangu na Taifa. Shangazi Fatma Karume na wanasheria wengine watafanya kazi Bure.
 
Baada ya Club ya Yanga kumuandikia barua ya wito Feisal Salum iliyoambatana na mashtaka dhidi yake mchezaji huyo amejitokeza, na kueleza wazi kuwa atapeleka kesi yake CAS kwani amenyimwa haki yake ya kuvunja mkataba na TFF!

Ameomba achangiwe na wote wenye mapenzi mema ili aweze kupata fedha kwa ajili ya kufungua kesi, mawakili wake watafanya kazi bure!

Kwa yeyote mwenye chochote anaweza kumsaidia kupitia Lipa namba 5406394 Feisal Salum.

Haya sasa huu mtanange nani mshindi huko CAS…!? Yetu macho cha msingi tumpe dogo mpunga!
 
Dogo anaomba achangiwe aende cas

My take zile milion 100 zimeisha?

Je sisi wenye mshahara chini ya milion 4 tutamchangia vipi? Maana aliyekimbia mshahara kuzidi wetu!!;

Je Fatima Karume &co hawana pesa za kumkopesha ashinde kesi aje awalipe?

Duh Huyu dogo anatia huruma Sana

Kwahiyo tumtigopesa
 
WATANZANIA NAOMBA MNICHANGIE - FEISAL

Kupitia mtandao wa instagram mchezaji wa Yanga Feisal Salum amepost akiomba wapenda soka Nchini kumchangia ili apate fedha zakufungua kesi Mahakama ya kimichezo CAS dhidi ya klabu yake ya Yanga

Kiasi kinachohitajika ni zaiai ya milioni 55

20230525_185503.jpg
 
WATANZANIA NAOMBA MNICHANGIE - FEISAL

Kupitia mtandao wa instagram mchezaji wa Yanga Feisal Salum amepost akiomba wapenda soka Nchini kumchangia ili apate fedha zakufungua kesi Mahakama ya kimichezo CAS dhidi ya klabu yake ya Yanga

Kiasi kinachohitajika ni zaiai ya milioni 55View attachment 2634537
Nipe bank account number sasa hivi nifanye swift
 
Ujinga mtupu.

Hao CAS nao mnawaona wajinga hivi eti?

Huyu hata aende jehanamu hawezi sikilizwa. Hakuna mtu atakuruhusu uamke asubuhi eti sababu kajitokeza tajiri akupe hela basi uvunje mkataba katikati ya msimu.

Feisal unadanganywa na unadanganyika kindezi sana dogo.

Kitu kimoja ukumbuke, mwisho wa siku ni wewe ndio unaathirika na si mawakili wako, si Fatma Karume wala sio mashabiki wa kolowizad wanaokujaza ujinga. Hao niliowataja kila mtu yuko na ajira yake mind you!
 
Back
Top Bottom