Umuhimu wa hiyo batoni ni pale unaposhukuru ya kuwa tatizo lako limefanikiwa. maforam ya zamani kulikuwaga hakuna hicho kitufe, na watu waliokuwa wanasaidiwa walikuwa wanaandika hoooooray senkyu, it worked senkyuuu, Well done na kuendelea yaani kama ni solution basi utakuta page tatu ni hayo senkyu yanajirudiarudia. ndo ikabidi hizi senkyuu za kuandika zirahisishwe na kuwekwa kitufe. ile thread iweze kueleweka. maana unaweza ukafungua page ya tatu unakutana na "thanks for the info"" thx" page nzima, unarudi nyuma ni "Oh! you are number one thanks", "thanks dude",Mkuu imekubali ahsante, unarudi nyuma ni hivyo hivyo sasa hata unakuwa huelewi thread ilikuwa na mada gani. nafkiri tutumie hicho kitufe cha Thanks ili thread iweze kusomeka vizuri. Itasaidia vilevile kuweka topic iliyotoa hiyo solution kuonekana vizuri kuliko kukutana na hayo ma senkyuu yaliyojaza page nzima. Nawaomba na Ma mods wawe makini katika hili.
Mimi nadhani katika hili tunajichanganya wenyewe
Hapa kuna mambo mawili tunachanganya
La kwanza ambalo mtoa mada ndio alimaanisha ni kuwa ukiomba msaada wa kitu ukapewa maelekezo nivizuri ukarudi na kutoa feedback kuwa nimefanya kama ulivyo nieleza na tatizo limekwisha, mfano mtu anaomba jinsi ya ku unstall let say karspersky inagoma kutoka wadau watampa solution tofauti kutokana na uelewa wa mtu, akifanikiwa harudi tena kusema jamani nimetumia njia aliotoa fulani ya kufanya hivi na hivi nimefanikiwa.
Lakini sasa mtu akifanikiwa anakula kona unamkuta jukwaa la mahaba nyinyi huku nyuma mnakazana kutoa masolution na kuanza kubishana.
Swala la pili ni kugonga thanx batani, hii inategemea na utashi wa mtu, kunawengine kwao kugonga thanx ni kama sumu na wengine tunatumia simu hii kitu haipo.
Nivizuri kufanya mrejesho ili wengine wajue namna uliofanya kupata ufumbuzi pia kumfanya alietoa ushauri afarijike kuwa ametoa mchango useful