Umuhimu wa hiyo batoni ni pale unaposhukuru ya kuwa tatizo lako limefanikiwa. maforam ya zamani kulikuwaga hakuna hicho kitufe, na watu waliokuwa wanasaidiwa walikuwa wanaandika hoooooray senkyu, it worked senkyuuu, Well done na kuendelea yaani kama ni solution basi utakuta page tatu ni hayo senkyu yanajirudiarudia. ndo ikabidi hizi senkyuu za kuandika zirahisishwe na kuwekwa kitufe. ile thread iweze kueleweka. maana unaweza ukafungua page ya tatu unakutana na "thanks for the info"" thx" page nzima, unarudi nyuma ni "Oh! you are number one thanks", "thanks dude",Mkuu imekubali ahsante, unarudi nyuma ni hivyo hivyo sasa hata unakuwa huelewi thread ilikuwa na mada gani. nafkiri tutumie hicho kitufe cha Thanks ili thread iweze kusomeka vizuri. Itasaidia vilevile kuweka topic iliyotoa hiyo solution kuonekana vizuri kuliko kukutana na hayo ma senkyuu yaliyojaza page nzima. Nawaomba na Ma mods wawe makini katika hili.