Fedha zetu ziko salama NBC? Nimekombwa hela jana!

Chromium

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
589
185
Naombeni msaada wa namna ya kutatua kadhia hii ya benki yetu ya NBC. Jana asubuhi nimechukua fedha wakati naenda kazini. Nikaomba na mini statement. Nikaweka kadi (Master Card) kwenye wallet. Nimerudi jioni benki kuchukua kiasi kingine, kutahayaruki fedha haifiki ile niliyoitegemea! Nikaomba statement nyingine. Ikaonekana fedha imekuwa withdrawn asubuhi (wakati nikiwa kazini na ATM yangu)!

Leo nimewaendelea benki. Nimewaeleza hawanipi ushirikiano wa kutosha. Baada ya kuonana na Meneja, anadai kumbukumbu zinaonyesha hela imetolewa na kadi yangu lakini na "Non local NBC ATM". Kwa mujibu wa maelezo yake maana yake ni kwamba fedha imetolewa kwingine na sio NBC ila kwa kadi yangu! Ananituhumu kuacha kadi mahali na mtu mwingine ameitumia kufanya uhalifu. Lakini ninachojua, kadi ilikuwa na mimi kazini na sikulewa aseme kuna mtu alinipekua! Baada ya kuomba ushahidi unaothibitisha kwamba hela hiyo nimetoa mimi kama anavyodai yeye, akaishia kunishauri nijaze fomu ya madai halafu atafuatilia! Sio siri nimeondoka na stress.

Tafadhali naombeni ushauri wa ninachoweza kufanya nipate hela yangu. Naomba msaada wa taratibu zinazopasa kufuata kudai haki yangu!
 
Pole. Uzuri umejaza fomu ya malalamiko. So una kwa kuanzia. Ingekuwa ni atms za ndani ya nchi, ingekuwa rahisi tu maana yale mamashine yana kamera nasikia. Fuatilia bwana, si unajua customer care za kibongo, huenda taarifa yake si sahihi.
 
...Hizo benk zinatisha kusema kweli. Kuna dada mmoja hapa jamvini jina limenitoka alikuwa na bank account CRDB tawi la Buguruni. Account ile aliitumia kuweka pesa tu hakuwahi kutoa hata mara moja kwa kipindi cha miezi sita kama sikosei. Siku moja anaenda kuweka pesa akaambiwa hii account haipo tena mwenye account kachukua pesa zake zote na kufunga account. Nachokumbuka baada ya kusumbuana na bank aliweza kurudishiwa pesa zake zote lakini hakutaka tena kuendelea na account ile. Bank zinatisha kusema kweli watu wataanza tena kuweka pesa majumbani mwao maana wengi wamenza kukosa imani na mabenki....kula nao sahani moja mpaka kieleweke.
 
Mkuu pole sana,kwa kifupi Bank zetu hapa Tanzania kumekuwa na uhuni sana kiasi kwamba wafanyakazi wengi wamekuwa siyo waaminifu na wamekuwa hawatoi ushirikiano mzuri kwa wateja wao pindi wanapopatwa na matatizo.Aisee komaa nao mpaka kieleweke hakuna cha non-local ATM wala nini ni wao hao hao.Itabidi tuanze kutunza pesa nyumbani kama mdau alivyoshauri hapo juu maana Mabank yetu yamekuwa ya hovyo.Kila la kheri
 
Pole. Uzuri umejaza fomu ya malalamiko. So una kwa kuanzia. Ingekuwa ni atms za ndani ya nchi, ingekuwa rahisi tu maana yale mamashine yana kamera nasikia. Fuatilia bwana, si unajua customer care za kibongo, huenda taarifa yake si sahihi.

Mkuu unaamaanisha 'Non local NBC ATM' maana yake ni nje ya nchi? Meneja anadai ni ATM za benki nyingine si NBC!
 
Mkuu unaamaanisha 'Non local NBC ATM' maana yake ni nje ya nchi? Meneja anadai ni ATM za benki nyingine si NBC!

ni ATM za bank nyingine tofauti na NBC,ambazo zina accept mastercard kwa mfano CRDB!
Kingine jaza hiyo fomu ya ku claim hela yako utaipata tu,bank hamna mambo ya kisanii,kama mtu kachukua hela itaonekana tu,muda,mahali na picture,so uzipanic
 
Wako hakuna kitu kizuri kwa ssa kama kudeal na bank ndogo ndogo ni more efficient kuliko hizo zilizokuwa mpaka
wameshindwa kuzimanage.

Hata kwa wenzetu watu wanapigwa vile vile ingawa wao wanatechnolojia nzuri kufuatilia
na kukamata wahusika
 
Kila ATM ina camera inayorekodi matokeo. Unachotakiwa ni kujaza fomu kama ulivyofanya. wataangalia video na muda pesa ilipotolewa na kukuita umtambue mtoaji.
Swala zima linaweza kuchukua from two weeks to three months. So for now hiyo pesa iondoe kwenye mahesabu yako. Jitahidi kuwa unaomba feedback kila baada ya wiki tatu. na risiti yako ya hiyo siku usiitupe.
Iwapo itagundulika kuwa aliyefanya hivyo ni mfanyakazi wa bank, unaweza kuifungulia bank mashtaka na kudai fidia.
 
nbc ndio mchezo,wamezidi ndio maana wateja wamekimbia hakuna deposit tena!very soon inakufa kabisa.kwa sasa ipo BOT
 
aisee pole! nami milishawahi ibiwa CRDB hela zilikuwa zinatolewa kwenye ATM za EXIM, nikajaza fomu zao na kufuatilia kila mara mwishowe zikarudishwa. mi nafikiri mabenki inabidi wajitahidi kuzuia wizi huu, la sivyo watu wataacha kuweka.
 
Hilo linatokea kwa zile ATM ambazo ni haziko Compliance na VISA Conditions kwa kuogopa gharama kubwa!! Hence wajanja wanaweka kimashine kwenye ATM,na kuchomoa wakiwa hata nje ya Nchi!! baada ya kujaza Form itakuchukua si chini ya nwezi mmoja(say 45 dys) kurejeshewa pesa km ikithibitika si makosa yako!! nakushauri katoe fedha zako au iwe blocked,kwani lazima watachukua tena na tena na tena!! pole
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom