Fedha zetu matopeni tena?

Fedha zetu matopeni tena?

Screenshot_20221122-151438_Twitter.jpg
 
Nadhani ni muda sasa ndugu Kadogosa kujiuzulu nafasi ya ukurugenzi madudu ni mengi uongo mwiiiingi
Lini uliona mwafrika akajiuzulu cheo chake mkuu? Sisi tukipewa nafasi hatujui uwajibikaji, coz kiuhalisia ukikosea unatakiwa uwaachie wenye uwezo waendelee, huo ndio uwajibikaji.
 
Sijui shida huwa ni nini? Nchi hii akitawala Muislam tunalizwa kwa kuibiwa akitawala Mkristo anapambana kujenga uchumi na kukandamiza wanachi sijui sasa tutafute mpagani? Mama anafeli sana!
 
Hii nchi hakuna kesi ya serikali ikashinda.

Hao wanasheria sijui mawakili ni kama wanakomoa.

Wauze tu kila kitu.

Sembe leo kilo ni 2000, mchele kilo 3000, maharage kilo 3600. Maji hakuna kabisa, umeme mgao mkali.

Tumeshapoteza mwelekeo.
Tupo wepesi kama karatasi angani
 
Hii nchi hakuna kesi ya serikali ikashinda.

Hao wanasheria sijui mawakili ni kama wanakomoa.

Wauze tu kila kitu.

Sembe leo kilo ni 2000, mchele kilo 3000, maharage kilo 3600. Maji hakuna kabisa, umeme mgao mkali.

Tumeshapoteza mwelekeo.
Sembe hutokana na mahindi makavu kusagwa,Michele hutokana na mpunga,vyote na maharage hulimwa,kalime upate unafuu wa maisha,acha kulialia,hakuna pinda wa kukulimia ili maisha yawe rahisi kwako
 
Huo kidogo mbona mwingi huu hapa

Benki ya Dunia (WB) imeipatia Tanzania mikopo nafuu ya TZS trilioni 1.24 kwa ajili ya miradi miwili, mmoja wa kusambaza umeme vijiji (REA) na mwingine wa kukabiliana na mafuriko katika Bonde la Mto Msimbazi, Dar es Salaam.
Hiyo REA ndio tulioambiwa hakuna Umeme wa 27,000/ kila siku inakuwa afadhali ya jana.
Brother Mshana Jr hii inaweza kuwa ni laana huko kwenye mambo ya kiroho. Tunahitaji kafara kubwa au ibada nzito kuvunja huu mkosi. Lile nina Tanganyika linafikirisha sana
 
Hii nchi hakuna kesi ya serikali ikashinda.

Hao wanasheria sijui mawakili ni kama wanakomoa.

Wauze tu kila kitu.

Sembe leo kilo ni 2000, mchele kilo 3000, maharage kilo 3600. Maji hakuna kabisa, umeme mgao mkali.

Tumeshapoteza mwelekeo.
Na ingekuwa treni zinafika huko, zingekamatiwa huko huko kama ilivyokuwa kwa ndege
 
Hii nchi hakuna kesi ya serikali ikashinda.

Hao wanasheria sijui mawakili ni kama wanakomoa.

Wauze tu kila kitu.

Sembe leo kilo ni 2000, mchele kilo 3000, maharage kilo 3600. Maji hakuna kabisa, umeme mgao mkali.

Tumeshapoteza mwelekeo.
Kwani tangu lini aliyeshiba akamkumbuka mwenye njaa
 
Mabehewa 30 na vichwa 2 vya treni za SGR mali ya TRC vinapigwa mnada 25/11/2022, Germany kufuatia mgogoro wa @tzrailways na EUROWAGON Railways Limited (Turkey), iliyopewa kazi ya kukarabati na kutia nakshi. TRC wamelipa Sh. 23 bilioni (35% ya kazi).

Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalçın Aydemir amesema wataanza na mnada wa mabehewa 17 ya awali katika mnada huo (hadi sasa wateja wawili wamepatikana kutoka Serbia), na mabehewa 13 na vichwa 2 vya treni za mwendokasi vitasubiri hadi mteja apatikane na kisha watavipiga mnada.

Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kampuni ya EUROWAGON ya kutoka Turkey ziliingia makubaliano Oktoba 2020 kwa ajili ya ujenzi (ukarabati na utiaji nakshi) wa vichwa viwili vya treni ya umeme na mabehewa 30 ya abiria ambao ulitegemewa kukamilika ifikapo Novemba 2021.

TRC ilisitisha mkataba huo Februari 25, 2022 kwa madai kwamba EUROWAGON wamechelewesha kazi na mazungumzo hayajawahi kuendelea. Kampuni ya RINA ilipewa kazi ya kuthibitisha kazi ya ukarabati na utiaji nakshi mabehewa hayo na kuthibitisha kwamba kazi hiyo imekamilika kwa 50%.

Hivyo EUROWAGON Railways Limited wanataka malipo ya Sh. 10 bilioni, ambayo ni 15% ya kazi iliyothibishwa na RINA kwamba kazi ya ukarabati na utiaji nakshi ilifanyika kwa 50% na malipo ya Sh. 23 bilioni ni kwa ajili ya 35% ya kazi hiyo. Malipo haya yalifanyika Desemba 14, 2020

Baada ya kuvunja mkataba huo Februari 25, 2022 na EUROWAGON, TRC wakaingia mkataba na kampuni nyingine kwa ajili ya ukarabati wa mabehewa na kutia nakshi. Kampuni hizo ni Zeller KG Engineer (Austria), Baltic Port Service GmbH na Lueckemeir Transport Logistics GmbH (Germany)

EUROWAGON kupitia Mwanasheria Duygu Seda, wakamuandikia barua Mkurugenzi wa TRC kwamba Tanzania Railways Corporation (TRC) wamevunja mkataba kwa njia ambazo siyo halali. TRC walivunja mkataba kwa kigezo cha EUROWAGON kushindwa kuwasilisha Dhamana ya Utendaji (performance Bond)

Mwanasheria wa EUROWAGON, Duygu Seda katika barua hiyo kwa Mkurugenzi wa TRC amemueleza kwamba kutokana na sheria za EU, Germany, Turkey na Austria na makubaliano kati ya EU na Turkey, TRC hawaruhusiwi kufika yalipo mabehewa na vichwa vya SGR wala kusafirisha isipokuwa EUROWAGON.

TRC hawakununua vichwa na mabehewa mapya kwa ajili ya SGR, isipokuwa, EUROWAGON waliopewa zabuni walinunua vichwa 2 na mabehewa 30 kutoka kampuni ya Reli inayomilikiwa na serikali ya Germany, DB Regio, ili kuvikarabati na kuvitia nakshi nakshi, kisha vilisajiliwa kuwa mali ya TRC

Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalcin Aydemir anasema kwamba TRC walimpa kazi bila dhamana ya Utendaji (Bank/performance guarantee) lakini ghafla TRC wakabadili gia angani na kuidai. Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa anasema EUROWAGON wanatapatapa tu hawana hoja.

TRC June 17, 2022 ilisema imesitisha mkataba na kampuni ya EUROWAGON, iliyokuwa ikitengeneza mabehewa hayo baada ya kushindwa kukamilisha ukarabati vichwa 2 na mabehewa 30 ya abiria, kwa ajili ya majaribio hayo, ni kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk

Vifaa hivyo kutoka EUROWAGON vilitakiwa kukamilika Novemba, 2021, TRC ilisitisha mkataba na kuwataarifu kwa barua Februari 25, 2022 na kuendelea na kazi ya kukamilisha ukarabati unaotarajiwa kukamilika Agosti mwaka 2022,” alisema mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk

Kwa mujibu wa Tanzania Railways Corporation, taarifa waliyoeleza kwa waandishi wa habari June 15, 2022, walisema Mkataba kati yao na EUROWAGON unaipa TRC haki ya kuchukua jukumu la kukamilisha ukarabati iwapo mzabuni atashindwa kuzingatia masharti ya mkataba.

YETU MACHO!

Credit: MMM Twitter

View attachment 2424022
Tumsifie mama anaupiga mwingi kwenye hii issue ya mabehewa.
 
Kukana, kwa serikali yetu ni kawaida sana..!! Walishawahi kana ZANZIBAR ilipojiunga na OIC, walishakana LOLIONDO ilipouzwa..!! hayo yote yalipelekea Stan Katabalo kuuwawa na gazeti lake lililojulika kama motomoto lilifungiwa maisha..!!

By the way, Mpaka wanavunja, walishalipa shilingi ngapi? Na kama walilipa, zipo wapi hadi sasa?
 
Back
Top Bottom