Fedha za Stanbic ziligharimia kampeni UKAWA?

Fedha za Stanbic ziligharimia kampeni UKAWA?

wanaccm ni vinara wa ufisadi
Ni kweli wana CCM ni vinara wa ufisadi lakini kwa sasa CHADEMA pia wameamua wawe nao vinara wa ufisadi wakiongozwa na Lowassa ili waweze kupambana na CCM.
 
Nilipomuona Mzee Warioba anapanda jukwaani kuhakikisha Lowassa haingii Ikulu, nikaanza kupata picha halisi ya Lowassa na genge lake.

Mzee Warioba ni kati ya wazee wachache wenye busara na hekima waliobaki nchini. Maneno na matendo yake yanabeba fikra fikirishi kwa watu wapevu kifikra.

Nchi yetu ilikuwa mbioni kutumbukia kwenye shimo la mauti. Mungu amefanya kazi yake iliyotukuka kupitia kwa wazee kama Mzee Warioba ili Lowassa na genge lake wasiingie Ikulu.

CHADEMA kama chama kupitia kwa Mbowe na Tundu Lissu kilikuwa kinajinadi kama mkombozi wa Watanzania, kimegeuka kuwa maajenti wa kuididimiza Tanzania.

Mungu bado analipenda taifa letu.

Tatizo lako Msemakweli ni Mnafiki sana.
Mbona huzungumzii pesa za Tegeta Escrow Account zilizobebwa kwenye masandarusi na magunia zilipelekwa wapi?
Tena Ambazo ni nyingi mara 25 ya hizo maana ni Billion 306.
Inamaana haujui kuwa zilitumika kufanyia kampeni za CCM?
kuwa mkweli na kweli itakuacha huru.
Wewe ni mnafiki sana tena sana.
 
Na huyo Mungu ni Mungu gani anayependa unafiki wako????
 
Tatizo lako Msemakweli ni Mnafiki sana.
Mbona huzungumzii pesa za Tegeta Escrow Account zilizobebwa kwenye masandarusi na magunia zilipelekwa wapi?
Tena Ambazo ni nyingi mara 25 ya hizo maana ni Billion 306.
Inamaana haujui kuwa zilitumika kufanyia kampeni za CCM?
kuwa mkweli na kweli itakuacha huru.
Wewe ni mnafiki sana tena sana.
Kama unataka pia tuchambue hoja za Tegeta Escrow account unaweza kuleta thread!

Hili ni jukwaa huru kwa kila mwanachama kuleta hoja au kuchangia hoja.

Kama unadhani mimi ni mnafiki, hizo ni fikra zako na uhuru wako kuishi katika mtazamo huo.

Hoja iliyopo mezani ni Fedha za Stanbic ziligharimia kampeni za UKAWA?

Changia kama una hoja mbadala!
 
Lowassa alikuwa na mamluki wa kutosha. Wengine mliwaona wakitoa matamko hadharani kule Dodoma. Wengine mkawapatia na zawadi ya ubunge. Hivyo mngetulia kwanza mahakama ya mafisadi iwe fully operational

Mahakama ya Mafisadi inayoshughulikia Dagaa badala ya kambale.
yaani katibu mkuu Uchukuzi ni Fisadi Waziri Mwakyembe ni Msafi.
 
Kuna mambo mabaya sasa yamefanyika nchini!

Ukweli huchelewa kufika na naamini kuna siku ukweli zaidi utatufikia.

Ukweli kama kutumia zaidi ya bilioni 2 kwa ajiri ya semina elekezi ni ufisadi wa aina yake.

Alikuwa anafanya nani? Ukawa au CCM?
 
Kama unataka pia tuchambue hoja za Tegeta Escrow account unaweza kuleta thread!

Hili ni jukwaa huru kwa kila mwanachama kuleta hoja au kuchangia hoja.

Kama unadhani mimi ni mnafiki, hizo ni fikra zako na uhuru wako kuishi katika mtazamo huo.

Hoja iliyopo mezani ni Fedha za Stanbic ziligharimia kampeni za UKAWA?

Changia kama una hoja mbadala!

Hata fedha za Tegeta Escrow zilitokea Stambic Bank tena kwa magunia ili kugharamia kampeni za CCM na ni pesa nyingi sana.
Kama una Uzalendo hata kidogo tu ungewataja waliochota hizo billion 306 ambazo nyingi sana.
 
Nilipomuona Mzee Warioba anapanda jukwaani kuhakikisha Lowassa haingii Ikulu, nikaanza kupata picha halisi ya Lowassa na genge lake.

Mzee Warioba ni kati ya wazee wachache wenye busara na hekima waliobaki nchini. Maneno na matendo yake yanabeba fikra fikirishi kwa watu wapevu kifikra.

Nchi yetu ilikuwa mbioni kutumbukia kwenye shimo la mauti. Mungu amefanya kazi yake iliyotukuka kupitia kwa wazee kama Mzee Warioba ili Lowassa na genge lake wasiingie Ikulu.

CHADEMA kama chama kupitia kwa Mbowe na Tundu Lissu kilikuwa kinajinadi kama mkombozi wa Watanzania, kimegeuka kuwa maajenti wa kuididimiza Tanzania.

Mungu bado analipenda taifa letu.
Pokea Like yangu. Yaani ni full wizi tu ndani ya chadema. Nina hoshindwa kuelewa kwa nini wanaoshabikia chadema na lowasa hawaelewi kuwa tabia ni ngozi na ngozi ni mtu na huwa haibadiliki? Kama lowasa aliweza kutumia hela kuibadili system ya Chadema na ndivyo wana ccm tunaamini Dr Magufuli ataibadili ccm na serikali yake. Nakumbuka kuna rafiki yangu alirogwa na uchadema alinitukana sana matusi ya nguoni nikamuambia lowasa ataendelea kuwa mwizi hata iweje, lakini siku hizi keshaniomba msamaha. Mnaoshabikia chadema torokeni au fukuzeni jizi lowasa ndiyo watanzania tutawaelewa otherwise chadema ya sasa ni mafisadi
 
Mahakama ya Mafisadi inayoshughulikia Dagaa badala ya kambale.
yaani katibu mkuu Uchukuzi ni Fisadi Waziri Mwakyembe ni Msafi.
Hujui tofauti ya katibu mkuu na waziri kiutendaji wewe!? Hebu thibitisha ufisadi wa Mwakyembe
 
Waliochukua hela Stanbic kwenye magunia ni Msafiri Marwa (Mume wa Salama Kikwete), Sospeter Muhongo, Eliakim Maswi, na Harbinder Singh Sethi. Wote hao hakuna mwana UKAWA
 
Tuwekee ushahidi wa wazi kama ule wa Escrow, wa walio chota hela kwenye Sandarusi sio hiyo figisu yako wala haieleweki

Wee naweee!!! Basi jiongeze kidogo. Yaani wewe unaambiwa watu walibeba fedha kwenye viroba na sandarusi na maboksi, na hiyo ni taarifa ya PCCB kwa CAG halafu hao watu hawajulikani. Na wewe unakubali tena kwa kusikitika na anakaa nayo moyoni na mawazoni mwako zaidi ya mwaka sasa ukiamini upuuzi huo. Kwa sababu waleta taarifa hizo hawakuleta majina ya waliochukua fedha hizo stanbic ili hali waliwaona jua kuwa ni figisu figisu za taarifa hicho kitu hakikutokea kwa jinsi hiyo surely there must be a different version ya hii story tumeaminishwa
 
Tatizo lako Msemakweli ni Mnafiki sana.
Mbona huzungumzii pesa za Tegeta Escrow Account zilizobebwa kwenye masandarusi na magunia zilipelekwa wapi?
Tena Ambazo ni nyingi mara 25 ya hizo maana ni Billion 306.
Inamaana haujui kuwa zilitumika kufanyia kampeni za CCM?
kuwa mkweli na kweli itakuacha huru.
Wewe ni mnafiki sana tena sana.

Kuhusu fedha zilizobebwa ktk masandarusi kule Stanbic si Mbowe wala Zitto atakayekuwa tayari kuona ripoti nyingine tofauti na ile ya Zitto ikusomwa tena bungeni kwasababu na wao walilamba.Jiulize,kwanini hawakutaka kusoma majina ya waliokwapua fedha za ESCROW kupitia account ya Stanbic wakati kamati ya PAC ikiwasilisha ripoti yake bungeni?Na Mbowe aliiunga mkono kwa 100% licha ya uadui wake na Zitto,nini kilichowaunganisha mahasimu hawa wa kisiasa?ni uzalendo wao kwa taifa lao au maslahi yao binafsi ndiyo yaliyowaunganisha?Zitto aliitwa msaliti na kuwadi wa mafisadi...Leo imekuwaje Mbowe amwamini ghafla?
 
CCM ilikuwa ndiyo kiwanda cha kuzalisha mafisadi.

Mvumbuzi, mjenzi na msimamizi wa kiwanda hicho alikuwa ni Lowassa!
Na mzee wa watu kajichokea 'ufisadi' ameamua kuhama. Huku nyuma kaacha watoto wa kifisadi tele kama akina JK, Rzimoko, wahusika wa EPA, Escrow, TRA, TRL, TPA, n.k...yaani choo kimefurika kinyesi ile mbaya. Maana tangu amestaafu kazi ya uzalishaji wa mafisadi almost miaka 10 iliyopita, production ya mafisadi imekuwa ikiongezeka kwa kasi ikiongozwa na mkuu wa kaya his ekselense himself!

MsemajiUkweli na wanaCCM wenzako mnachekesha sana. Maana mnashikilia usemi wenu huo ambao hata ninyi hamuuamini eti Lowassa ndiye alikuwa fisadi PEKEE nchi hii. Hata ninyi mnajua si kweli, ila mnajaribu kubahatisha huku mkiomba wasio wanaCCM wachache wanaweza kuwaamini. Ni sawa na kushikilia utando wa buibui huku ukitegemea utakusaidia kukuzuia usiporomoke down the cliff!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom