Nilipomuona Mzee Warioba anapanda jukwaani kuhakikisha Lowassa haingii Ikulu, nikaanza kupata picha halisi ya Lowassa na genge lake.
Mzee Warioba ni kati ya wazee wachache wenye busara na hekima waliobaki nchini. Maneno na matendo yake yanabeba fikra fikirishi kwa watu wapevu kifikra.
Nchi yetu ilikuwa mbioni kutumbukia kwenye shimo la mauti. Mungu amefanya kazi yake iliyotukuka kupitia kwa wazee kama Mzee Warioba ili Lowassa na genge lake wasiingie Ikulu.
CHADEMA kama chama kupitia kwa Mbowe na Tundu Lissu kilikuwa kinajinadi kama mkombozi wa Watanzania, kimegeuka kuwa maajenti wa kuididimiza Tanzania.
Mungu bado analipenda taifa letu.