Fedha za EPA zilikorudishwa zaliwa tena; Peter Noni wa EPA, Simon Group wa UDA ndani..

NDIYO MAaNA MI NAONA HIYO MISAADA BORA WASITUPATIE.. KWA SABABU TUNA VIONGOZI WEZI, MAFISADI NA WABINAFSI.
 
Dawa ya mafisadi ni KUNYONGWA. Bila kufika mahali tukachinjana kwanza hawa washenzi hawatatuheshimu, na wataendelea kutufanya kama shamba la bibi siku zote.
 
Duh hii kali sasa! hivi haya maandamano tuyaanze lini! kwa sababu za kuanzisha maandamano yatakayopewa ulinzi ni Waingereza na Ushoga lakini tunaunganisha humo humo ya Dowan na haya ya Epa
 


Thursday, 03 November 2011 21:27

zimeliwa.jpg
Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Deo Filikunjombe (katikati) akiwasisitizia jambo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Uwekezaji (TIB) Peter Noni (kulia) na Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya Benki hiyo Mgana Msindai mara baada ya kupitishwa hesabu za benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.Picha na Said Powa​


Leon Bahati na Furaha Maugo - Mwananchi.

KAMATI ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imebaini ufisadi mwingine wa mabilioni ya fedha kwenye marejesho ya zile zilizochotwa awali kifisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).Fedha hizo zaidi ya Sh50 bilioni zilizorejeshwa na Rais Jakaya Kikwete kutangaza kuwa zitatumika kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo nchini, zinadaiwa kuchotwa kwenye Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) kwa amri iliyotoka kwa vigogo serikalini.

Mkurugenzi wa TIB, Peter Noni alikiri jana mbele ya POAC kuwa sehemu ya Sh20 bilioni zilizotolewa na Hazina kwenda kwenye benki hiyo kwa ajili ya dirisha la kilimo, Serikali iliamuru zitolewe kama mkopo kwa wafanyabiashara ambao iliwataja kwa majina.

"Mbaya zaidi, baadhi ya wafanyabiashara waliopewa mikopo hiyo wanaonekana kukwama kurejesha, huku wakitoa ahadi ambazo hawazitekelezi," Noni alisema.

Wabunge wengi wa POAC walionyesha kushangazwa na jinsi serikali ilivyoingilia kati TIB na kuchagua watu ambao wanapaswa kupatiwa mikopo.Huku miongoni mwa wabunge hao wakisema wana taarifa za vigogo walioingia mlango wa nyuma na kuchukua tena fedha hizo katika mazingira ya kifisadi, waliendelea kumbana Noni kwa maswali.
Ingawa baadhi ya wabunge walimtaka mkurugenzi huyo wa TIB awataje kwa majini vigogo hao, Makamu Mwenyekiti wa POAC, Deo Filikunjombe, alisita na kumtaka Noni asitaje majina hayo.

Miongoni mwa wabunge waliotaka majina ya vigogo hao yawekwe hadharani ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya aliyesema, “Nina habari kuwa baadhi ya vigogo walihusika katika kupata mikopo hiyo… Naomba uyataje majina yao.”

Filikunjombe, alisema hakuna haja ya kutaja majina ya vigogo hao ambao alisema miongoni yamo kwenye taarifa waliyopatiwa kuhusu utendaji mzima wa TIB.

Lakini Noni ambaye alikuwa anasaidiwa pia na wasaidizi wake kujibu baadhi ya maswali mazito yaliyoulizwa na wabunge, alisema hakuna tatizo kutaja baadhi ya kampuni zilizohusika kwenye mikopo hiyo ambayo sasa inawatoa jasho TIB.

Noni alitaja mbele ya kamati hiyo kuwa moja ya kampuni zilizochukua fedha hizo na sasa zinaonyesha wasiwasi katika kuzirejesha ni Simon Group Ltd.Nyingine ni kampuni tano za kuuza maua nje ya nchi zenye makao yake makuu mjini Arusha, zikiwepo Tengeru Flowers na Mount Meru Flowers.

Kuhusu Kampuni ya Simon Group, ambayo ilielezwa kuwa ilikopeshwa Sh5 bilioni Noni alisema; “Tumekutana nao mara kadhaa na kutoa ahadi lakini hawakuzitekeleza.”
Aliongoza kuwa kampuni za kuuza maua nje ya nchi zilieleza tatizo lililowafanya kushindwa kurejesha mikopo hiyo kulingana na makubaliano kwamba, ni hasara waliyoipata kutokana na mdororo wa kiuchumi duniani.

Alifahamisha kuwa kutokana na hali hiyo, Serikali iliwaonea huruma na kuwaongezea kipindi cha miaka miwili kulipa deni hilo, muda ambao pia umeonekana kutotosha.

Ila akaahidi kwamba TIB itaanza mchakato wa kuwabana wadeni hao kwa kunadi mali ambazo ziliwekwa rehani wakati wa kuchukua mikopo hiyo.

“Uandaaji na usafirishaji wa maua walisema unahitaji gharama kubwa… Walilazimika kupitia Nairobi (Kenya)… Serikali iliona huruma ikawaongezea kipindi cha kulipa deni hilo,” alisema Noni huku wabunge wengi wakionyesha shauku ya kuendelea kumbana kwa maswali.

Miongoni mwa maswali yaliyoulizwa ni kwa nini TIB ilikubali kutoa mkopo kwa biashara ambazo hazitabiriki? Noni aliweka wazi kwamba, benki hiyo haikuhusika katika mchakato wa kuchambua na kuridhia mikopo kutolewa kwa kampuni hizo.

Filikunjombe ambaye ni Mbunge wa Ludewa, alishangazwa na jinsi Serikali ilivyoingilia uhuru wa TIB na kuweka wazi kwamba si mara ya kwanza Serikali kuingilia mashirika ya umma kiutendaji na kwamba, historia inaonyesha kila ilipofanya hivyo iliziingiza taasisi hizo kwenye mzozo.

“Serikali iliwahi kuingilia kati na kushawishi Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania) kuingia mikataba (ya kuzalisha umeme wa dharura) na Richmond na Dowans na kusababisha mzozo,” alitoa mfano Filikonjombe.

Hivyo, akaonya TIB kuhusu kupokea maagizo holela Serikalini kwa sababu mzigo wa matatizo yatakayotokea, itajiweka kando na kuiachia taasisi hiyo ya umma lawama na vibano kutoka kwa wananchi.
Mapendekezo ya Kamati
Ili kuikoa benki hiyo, Filikunjombe alitoa mapendekezo sita ambayo miongoni mwake ni kuitaka TIB ijitegemee na kufanya kazi zake kama shirika la umme lenye uwezo wa kufanya maamuzi yake ya kiutendaji bila kuingiliwa na wanasiasa serikalini.

“Mhakikishe hamuingiliwi na Wizara ya Fedha au Serikali katika suala la utoaji wa mikopo,” alishauri Filikonjombe.
Mapendekezo mengine ni muundo wa manunuzi katika taasisi yao uendane na sheria ya manunuzi, kuwa ni mikakati ya kushindana kibiashara na benki nyingine na kuhakikisha kuwa mtaji unakua.

Katika hatua nyingine, POAC ilishangazwa kuona kuwa kati ya zaidi ya Sh50 bilioni zilizokusanywa kwenye marejesho ya fedha zilizochotwa EPA, ni Sh20 bilioni pekee zilizoifikia TIB.
Wabunge hao walielezea kushangazwa na kitendo cha Menejimenti ya TIB kupokea fedha hizo tu na kushindwa kuishinikiza Serikali itoe fedha zaidi.

Noni alisema kuwa TIB haikuwa na mamlaka ya kuishinikiza Serikali ili iipatie fedha zote za marejesho ya EPA.
“Sisi tulichopewa ndiyo hicho. Hatukuwa na sababu ya kudai fedha zaidi,” alisema huku akizidi kuzua mtafaruku wa maswali kwa wabunge hao.

Wabunge wengi walionyesha kuamini kuwa fedha zote zilipelekwa TIB baada ya Serikali kuahidi kuwa fedha za marejesho hayo zitapelekwa kwenye shughuli za kilimo.

TIB ndiyo benki iliyoanzishwa na Serikali kwa malengo ya kuinua kilimo nchini ambacho kinategemewa na asilimia 80 ya Watanzania.Wananchi wengi wanaojishughulisha na kilimo nchini ndio wanaogubikwa na wimbi la umasikini kuliko sekta nyingine.

Hata hivyo, Serikali imeamua kuanzisha kampeni ya Kilimo Kwanza, yenye lengo la kufanya sekta hiyo kuwa yenye manufaa na inayoweza kuleta utajiri tofauti na mwonekano wa sasa wa kuwa ni ya kundi la wasio na taaluma.
Taarifa nyingine zilizopatikana jana baada ya kamati hiyo kumaliza kikao chake ni kwamba sehemu ya marejesho ya fedha za EPA, mbali na zile Sh20 bilioni zilizopelekwa TIB, zilitolewa kwa moja kwa moja kwa kampuni za pembejeo za kilimo.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge walielezea kutokuwa na imani kama fedha hizo zilitumika kikamilifu kwa ajili ya pembejeo hizo za kilimo.

Mmoja wa wabunge kutoka CCM ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini alisema kuna uwezekano fedha hizo zimeliwa na wajanja.

“Hata ukiangalia suala la marejesho halikuwekwa wazi, maana Rais (Kikwete) mwenyewe alisema zimekusanywa Sh53 bilioni, mara wengine wakasema 60 bilioni na wengine 70 bilioni.Alisema kama ufisadi uliweza kupenya hadi fedha zilizotolewa kwenye taasisi makini ya benki (TIB) basi hakuna shaka hata zilizotolewa kimyakimya ziliingia kwenye mikono hiyo ya mafisadi.

Hata hivyo, gazeti la serikali liliwahi kumnukuu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mohamed Muya, akisema katika mgawanyo wa fedha za EPA, wizara hiyo ilipewa Sh40 bilioni ambapo Sh30 bilioni zilitumika kwa ruzuku ya pembejeo ya mbolea hali ambayo imesaidia katika uzalishaji. 


“Kutokana na ruzuku hizi, hata idadi ya wakulima wanaopata vocha za ruzuku hiyo imeongezeka kutoka wakulima 500,000 hadi wakulima milioni 1.5 mwaka huu na kupitia Kamati ya Maafa na ya Usalama wa Chakula, hali ya chakula mwaka huu ni nzuri kuliko mwaka jana,” alisema Muya. 



Alisema katika fedha hizo za EPA, Sh10 bilioni zilizobaki zilitumika katika maeneo matatu ya kilimo ambayo ni Mfuko wa Pembejeo ambao ulipewa Sh3 bilioni, Wakala wa Mbegu wa Taifa Sh1 bilioni na kutatua matatizo ya visumbufu kama vile nzige, kweleakwelea na viwavijeshi Sh6 bilioni.

My Take:
Hawa Simon group wamefanya biashara kwa muda gani na wana mtaji kiasi gani? Ni hawa wanaotaka kununua UDA na sasa wamekopa EPA duh! kweli bongo tambarareeeeee!!!!!!!!!
 
Nina uchungu sana,hizo fedha hazitalipwa kamwe kama zilivyoliwa za stimulus package na commodity support.wana jf na wananchi tuache porojo tureact kwa vitendo bila hivyo ni ndoto nchi kuendelea.
 
Kuliwa kwa hizi fedha na wajanja ni mwendelezo wa EPA kwani ilishazungumzwa humu janvini kuwa kuchaguliwa kwa NONI kwenda kuongoza TIB baada ya yeye kuwa alikuwa mhusika mkubwa wa EPA haikuwa ajali!! Sasa Noni huyo huyo anaimbia kamati ya bunge kuwa aliamriwa na serikali azipe kampuni fulani fulani pesa[ bila shaka Simon group ni moja wapo kwani Ridhwani ni mshiriki wa hii kampuni] na hivi sasa zinashindwa kurejesha mikopo!! Ni vyema wabunge wakambana huyu bwana aseme nani walimshinikiza kutoa hiyo mikopo na kwa mashariti gani. Haswa haswa hii kampuni ya kitapeli ya Simon group ambayo inahusishwa na kuifisadi kampuni ya umma ya UDA. Mambo ya kishenzi kama haya Rais makini anatakiwa ayatolee maneno makali lakini anapokaa kimya na mwanae kuhusika watu huamini kuwa na yeye yuko nao. Ni vizuri viongozi wakajifunza kwa hayo yanayowapata wenzi wao hivi sasa.
 

Mabilioni ya fedha za EPA yatoweka
• Wabunge washikwa na mshangao

na Hellen Ngoromera
Tanzania Daima




ZAIDI ya sh bilioni 61 zilizodaiwa kurejeshwa na baadhi ya watuhumiwa wa wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete, hazijulikani ziliko baada ya Benki ya Rasilimali Nchini (TIB) iliyotakiwa kuzipokea kudai kuwa hazijawafikia.(WanaJF tulihoji baada ya kauli ya Kikwete kwamba sh 61 billioni zimerudishwa, tulihoji zimewekwa bank ipi na pia tulitaka bank account # iwekwe hadharani ili tuweze kuthibitisha...kumbe ulikuwa UWONGO MTUPU!!)

Kashfa hiyo mpya iligundulika jana wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ilipokuwa ikipitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyokagua hesabu za benki hiyo kwa mwaka 2010/2011.

Mkurugenzi wa TIB, Peter Noni, aliwaambia wajumbe wa kamati hiyo kuwa benki yake haijawahi kupokea fedha hizo za EPA, badala yake ilipewa sh bilioni 20 tu kwa ajili ya kile kilichoitwa dirisha dogo la kilimo na si vinginevyo.
Noni alitoa kauli hiyo kutokana na swali la Mbunge wa Viti Maalumu Zainab Kawawa (CCM) aliyetaka kujua kama TIB ilipewa fedha za EPA na mwenendo wa makusanyo ya madeni yaliyokopwa na mashirika au watu binafsi.
Noni alieleza pamoja na sh bilioni 20 za dirisha la kilimo, katika bajeti ya mwaka jana serikali kupitia Wizara ya Fedha na Uchumi iliwapatia sh bilioni 50 kama mtaji wa benki na kwamba hata mwaka huu pia itawapatia kiasi kama hicho.

Baada ya hoja hiyo, mkurugenzi wa TIB alishindwa kutoa majibu ya moja kwa moja zaidi ya kujikanganya akisema hafahamu kuhusu fedha za EPA na hawakuona haja ya kufuatilia kuhusu fedha nyingine kwa kuwa hizo ndizo walizoahidiwa.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filikunjombe (CCM), alimhoji mkurugenzi huyo: "Rais mwenyewe ameagiza kwamba fedha tunakupa je mkurugenzi wetu Noni vipi hii hela umeifuatilia?"
Akijibu hilo Noni alisema, "Nilichosema ni kwamba kuna fedha zimekuja kutoka Wizara ya Fedha kwa ajili ya kuanzisha dirisha la kilimo na hizo fedha tumeshazipokea na tumezitumia, taarifa ya matumizi yake tumewaletea.

"…TIB ilipewa fedha na tunaendelea kufuatilia mtaji kutoka Wizara ya Fedha kwa sababu tuliambiwa tungepewa mtaji na hatujaambiwa kama zinatokana na makusanyo ya EPA."
Baada ya wabunge wa kamati hiyo kumshambulia kwa maneno wakitaka kujua kwa kina ziliko fedha hizo huku wakionyesha kutoridhishwa na majibu yake, Noni alisema, "Kwanza naomba radhi sana kama katika kujibu nimekosea kwa sababu ya kutoelewa swali, napenda kusema kwamba hizo fedha sh bilioni 20 tulizopokea mchakato wake ulianza Desemba, 2009 na utoaji wa mikopo ulianza rasmi Mei mwaka jana."
Wabunge wengine waliozungumzia suala la EPA ni pamoja na Ester Bulaya (CCM), Eshter Matiko (CHADEMA) na Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM) wakitaka maelezo ya kina kutoka kwa mkurugenzi na timu yake.

Kawawa alieleza masikitiko yake kuhusu suala la EPA, huku Bulaya akishangazwa na hatua ya Noni kukataa kujibu maswali aliyoulizwa ilhali alikuwa anaohojiwa na kamati yenye mamlaka sawa na Bunge.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa POAC, Filikunjombe, alieleza kwamba katika hesabu nyingi zilizopitiwa imeonekana kwamba baadhi ya utekeleza wa mambo katika benki hiyo unatokana na maagizo yanayotolewa na serikali badala ya TIB kufanya mambo yake bila kuingiliwa.

"Tunatoa maagizo kwamba amueni wenyewe kuhusu mambo yenu, siasa tuachieni wanasiasa. Tazameni maamuzi ya Richmond, Dowans tusingependa muingiliwe kwani yakiwa mabaya mnatupiwa mzigo," alisema Filikunjombe.

Serikali iliwaamuru wafanyabiashara waliojichotea fedha hizo kiasi cha sh bilioni 133 kuzirudisha kwa hiyari yao wenyewe ambapo ilidaiwa kwamba zaidi ya sh bilioni 61 zilikuwa zimerejeshwa katika taasisi mbalimbali ikiwemo TIB.

Mei mwaka huu kamati hiyo ilimhoji Gavana wa Benki Kuu (BoT) Profesa Benno Ndullu ambaye alieleza kutojua ziliko fedha hizo kwa maelezo kuwa ni mali ya serikali na ofisi yake ni mtunzaji wa fedha za serikali.

Hoja ya kutojulikana kwa fedha hizo mahali ziliko iliwahi kuibuliwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, miezi michache iliyopita, lakini serikali ilikanusha ikidai kuwa ni maneno ya siku zote ya wapinzani.

Katika hatua nyingine, Bulaya alihoji kuhusu kilimo akieleza kuwepo kwa malalamiko mengi ya mradi wa maua kutofanya vizuri hivyo alitaka kuwafahamu wamiliki wake.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, hadi sasa sh bilioni 2.3 zilizokopwa tangu mwaka 2004 kwa ajili ya kuendesha mradi wa maua hazijarudishwa hadi sasa akadai kwamba kuchelewa huko kunatokana na baadhi ya vigogo kujiingiza kwenye suala hilo na cha ajabu ni kwamba wadaiwa hao wanataka kuomba tena.Kabla mkurugenzi hajajibu makamu mwenyekiti alizima hoja ya mbunge huyo iliyotaka kutajwa kwa majina ya wamiliki wa miradi hiyo akisema taratibu za kibenki jina la mkopaji ni siri na kwamba hata kwenye taarifa waliyonayo hakuna majina ya vigogo wanaomiliki kampuni za maua zinazodaiwa.

Simon Group yalipuliwa

Katika hatua nyingine TIB imesema kampuni ya Simon Group ambayo imewekeza katika Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) ni miongoni mwa wadaiwa sugu walio kwenye orodha ya mufilisi kwa kushindwa kurejesha deni la sh bilioni tano.

Noni alisema hayo baada ya Filikunjombe kutaja baadhi ya wadaiwa sugu wa benki hiyo kwa mujibu wa vitabu vya hesabu za TIB zilizofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) vya mwaka 2010/2011.
Miongoni mwa wadaiwa waliotajwa ni Ali Adawi ambaye ni mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya Dowans.(Mhhhhh!)

Akijibu hilo, Noni alitetea urejeshaji wa deni la Dowans kwa maelezo kuwa unaonyesha tija huku akikiri kwamba kampuni ya Simon Group inasuasua kwenye marejesho hali inayoilazimu TIB kujipanga kwa ajili ya kufilisi mali za kampuni hiyo ili kufidia deni.
Filikunjombe alikwenda mbali zaidi akaeleza kwamba pamoja na Simon Group kudaiwa kiasi hicho cha fedha bado wana madeni mengi kwenye benki tofauti.Kutokana na madeni hayo licha ya kupitishwa kwa hesabu zake, kamati iliiagiza TIB kusimama yenyewe na kufanya utafiti kabla haiajatoa mikopo na kumtaka Msajili wa Hazina kupendekeza Wizara ya Fedha kufanya uhakiki kuhusu miradi ya maua.



 
Patamu hapo,hela wanakula wenyewe kwa wenyewe tu,alafu hela ni za wananchi,sio mchezo hii ndio bongo bana kila mtu anafanya anavyotaka yeye maana mkulu mwenyewe yupo kwenye kundi la wezi raha sana...
 
Watanzania wanapiga kura kama vipofu, halafu wanalalama kama vichaa!

Hawakuchaguliwa hawa Mkuu!!! bali walichakachua uchaguzi kuanzia wa baadhi ya Wabunge mpaka wa Urais kwa kutumia Tume ya uchaguzi ya Magamba na vyombo vya dola.
 
Nimepitia mabandiko yote katika uzi huu na nilichoona ni kuwa SIMON GROUP ni wadaiwa sugu wa TIB na inaelekea mikopo hiyo walichukua muda mrefu hadi kuonekana wameshindwa kulipa. Hizi pesa za 'kilimo kwanza' ni za hivi karibuni na haingii akilini wakopaji wa hizi hela tena kwenye uwekezaji wa kilimo warejeshe ndani ya miaka 2?
 
KAMATI ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imebaini ufisadi mwingine wa mabilioni ya fedha kwenye marejesho ya zile zilizochotwa awali kifisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA). Fedha hizo zaidi ya Sh50 bilioni zilizorejeshwa na Rais Jakaya Kikwete kutangaza kuwa zitatumika kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo nchini, zinadaiwa kuchotwa kwenye Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) kwa amri iliyotoka kwa vigogo serikalini.

Mkurugenzi wa TIB, Peter Noni alikiri jana mbele ya POAC kuwa sehemu ya Sh20 bilioni zilizotolewa na Hazina kwenda kwenye benki hiyo kwa ajili ya dirisha la kilimo, Serikali iliamuru zitolewe kama mkopo kwa wafanyabiashara ambao iliwataja kwa majina.Mkurugenzi wa TIB, Peter Noni alikiri jana mbele ya POAC kuwa sehemu ya Sh20 bilioni zilizotolewa na Hazina kwenda kwenye benki hiyo kwa ajili ya dirisha la kilimo, Serikali iliamuru zitolewe kama mkopo kwa wafanyabiashara ambao iliwataja kwa majina.

Ingawa baadhi ya wabunge walimtaka mkurugenzi huyo wa TIB awataje kwa majini vigogo hao, Makamu Mwenyekiti wa POAC, Deo Filikunjombe, alisita na kumtaka Noni asitaje majina hayo. Noni alitaja mbele ya kamati hiyo kuwa moja ya kampuni zilizochukua fedha hizo na sasa zinaonyesha wasiwasi katika kuzirejesha ni Simon Group Ltd. Nyingine ni kampuni tano za kuuza maua nje ya nchi zenye makao yake makuu mjini Arusha, zikiwepo Tengeru Flowers na Mount Meru Flowers.

Kwa kweli sakata la EPA ni ufisadi taslimu na linatia kichefuchefu sana. Toka Rais alipomteua Peter Noni kuwa Mkurugezi TIB nlijua lengo ilikuwa ni kufanya haya yaliyotokea. Peter Noni alihusika katika wizi wa fedha za EPA akiwa mfanyakazi BOT. Hivyo kuteuliwa kwakwe kuiongoza TIB ilikuwa ni kuhadaa wananchi na kuficha ukweli.

Kwa Rais kumteua mtuhumiwa wa wizi wa EPA kuiongoza TIB na Baadaye kutudanganya kuwa hizo hela keshazipeleka TIB na kumkabidhi Peter Noni ni kutufanya wananchi viazi, wapumbavu na mazezeta. Kimsingi hapa Rais amejipambanua kama mhusika ktk hili sakata la EPA. Ukichunguza kwa undani unaweza kukuta hizo fedha hazikupelekwa kabisa TIB, ila kwa kuwa TIB inaongozwa na mtuhumiwa wa huo ufisadi tumedanganywa tu.

Hivi nini hasa sababu ya sisi wananchi kufanywa wapumbavu??Hivi Rais hakuona mwingine wa kumweka TIB zaid ya huyu Peter Noni ambaye ni mtuhumiwa wa EPA pia???hivi kweli sisi wananchi hatuna cha kufanya katika ujinga kama huu???kwann tuliowaamini kutuongoza leo wamekuwa wanatuhujumu??Nini hasa sababu ya kuwa na serikali isiyoaminika kama hii? Kama inashindwa kuaminika kwa fedha ndogo kama hizi kwa nn tuwaamin kwa kuwaachia nchi na rasilimali zake?

Hivi hakuna utaratibu wa kuondoa viongozi wezi kama hawa? Nani aliyeiamuru TIB kukopesha hao walioshindwa kurudisha hizo fedha???Naomba tumjue aliye amuru, PCCB, wataalam wa Intellejensia (KOVA na Mwema) hamuoni kama kunaharufu ya Rushwa hapo???Hakuna kitu mnaweza fanya hapo kwa Kiongozi aliyeagiza hela ya wananchi zitoke kienyeji?

Kwa utaratibu huu wa kutoa mikopo kwa kujuana, TIB itasurvive? Tunapoelekea naona Serikali itatutia kidole jichoni, nadhani inatosha.................................Nakaribisha mawazo yenu wanaJF nn kifanyike kukomesha hii hali.

Mwananchi 03/11/2011​

Kampuni za maua zilipewa mkopo na Serekali kupitia Bank Kuu chini ya usimamizi wa TIB miaka ya 2004/2005. Kampuni zilizopewa mkopo huo chini ya mfuko ulionzishwa na Mh Mramba wa kukuza export of high value crops/products with critical mass and employment creation (Export Guarantee Scheme) ni pamoja na Kiliflora, Tengeru Flowers, Tanzania Flowers Ltd, La Fleur d'Afrique Ltd (Hii ni kampuni ya Mheshimiwa Felix Mrema aliyekuwa mbunge wa CCM Arusha mjini) na Gomba Estate. Kampuni hizi zilipewa mabilioni ya fedha na toka wakati huo urudishwaji wa mikopo hii umekuwa wa kusua sua, nadhani LDF ya Mrema haijarudisha hata senti moja hadi leo
Kampuni zilijenga hoja kwa Serekali na BOT kuwa KIA imekuwa kama gofu kwa kuwa hakuna ndege za mizigo zinatua pale kwa kuwa hakuna mzigo wa kutosha. Zililalamika kuwa zinapeleka maua Nairobi na hivyo yanapoteza freshness kwa at leat 2 days. Hivyo zikaomba serekali izikopeshe ziweze kuongeza uzalashaji, kukuza ajira na kuufanya uwanja wa KIA UWE FUNCTIONAL. Hizi kampuni wakati zinaomba huu mkopo zilikuwa HOI na madeni makubwa ya ndani na nje ya nchi, zilikuwa hazikopeshekiki na wadeni walishaanza mchakato wa kuziflilsi. BOT ilizilipia madeni hayo kuzifanya ziwe bankable- restructuring, and yet zikawa sio bankable na BOT ikazipa fedha kwa mabilioni.

Kinachoniuma na kunishangaza ni kama serekali imeendelea kushindilia mikopo mingine mipya kwa kampuni hizi hata baada ya kushindwa kulipa mikopo ya awali ni ufisadi wa hali ya juu. TIB walipewa jukumu la kusimamia mikopo hiyo na wanajua fika uwezo wa kampuni hizi kiutendaji na kifedha, sasa iweje waendelee kuwachotea mabilioni hayo? Watanzania wenzangu tumuulize boss wa TIB ilikuwaje awape fedha wakati fedha za serekali mabilioni kw amabilioni hazijarejeshwa? LDF nadhani imekufa, je TIB imeishaifilisi kurecover fedha za walipa kodi? Hivi kwa nini viongozi wetu wamekosa uzalendo kiasi hiki. Ni vyema vyuo na shule vikaanza kufundisha kw alazima somo la uzalendo, it is getting out of control kwa hali hii ndugu zangu.

Mie nadhani hilo ni changa la macho, waandishi na wabunge msikubali jambo hilo, siamini kama TIB imetoa mikopo mipya kwa hizi kampuni, hata baada ya kushindwa kulipa mabilioni ya awali, si ajabu inatumia information za mikopo ya zamani iliyotolewa wakati huo kuficha ukweli. CHANGA LA MACHO HILO!!
 
Serikali yetu ni kama Club,haiko tena kuwasaidia watanzania,club members wako kwa ajili yao wenyewe na familia zao. Watanzania wacha wataabike kwani wanapenda mtu anaye waambia uwongo na si msemakweli.Wanapoambiwa ukweli wanasema mwongo.
Bado yapo machafu mengi tu ambayo hatuyajui,ndiyomaana nawafananisha na club tu.
 
Back
Top Bottom