Fedha za EPA zilikorudishwa zaliwa tena; Peter Noni wa EPA, Simon Group wa UDA ndani.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fedha za EPA zilikorudishwa zaliwa tena; Peter Noni wa EPA, Simon Group wa UDA ndani..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Nov 4, 2011.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  KAMATI ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imebaini ufisadi mwingine wa mabilioni ya fedha kwenye marejesho ya zile zilizochotwa awali kifisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA). Fedha hizo zaidi ya Sh50 bilioni zilizorejeshwa na Rais Jakaya Kikwete kutangaza kuwa zitatumika kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo nchini, zinadaiwa kuchotwa kwenye Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) kwa amri iliyotoka kwa vigogo serikalini.

  Mkurugenzi wa TIB, Peter Noni alikiri jana mbele ya POAC kuwa sehemu ya Sh20 bilioni zilizotolewa na Hazina kwenda kwenye benki hiyo kwa ajili ya dirisha la kilimo, Serikali iliamuru zitolewe kama mkopo kwa wafanyabiashara ambao iliwataja kwa majina.Mkurugenzi wa TIB, Peter Noni alikiri jana mbele ya POAC kuwa sehemu ya Sh20 bilioni zilizotolewa na Hazina kwenda kwenye benki hiyo kwa ajili ya dirisha la kilimo, Serikali iliamuru zitolewe kama mkopo kwa wafanyabiashara ambao iliwataja kwa majina.

  Ingawa baadhi ya wabunge walimtaka mkurugenzi huyo wa TIB awataje kwa majini vigogo hao, Makamu Mwenyekiti wa POAC, Deo Filikunjombe, alisita na kumtaka Noni asitaje majina hayo. Noni alitaja mbele ya kamati hiyo kuwa moja ya kampuni zilizochukua fedha hizo na sasa zinaonyesha wasiwasi katika kuzirejesha ni Simon Group Ltd. Nyingine ni kampuni tano za kuuza maua nje ya nchi zenye makao yake makuu mjini Arusha, zikiwepo Tengeru Flowers na Mount Meru Flowers.

  Kwa kweli sakata la EPA ni ufisadi taslimu na linatia kichefuchefu sana. Toka Rais alipomteua Peter Noni kuwa Mkurugezi TIB nlijua lengo ilikuwa ni kufanya haya yaliyotokea. Peter Noni alihusika katika wizi wa fedha za EPA akiwa mfanyakazi BOT. Hivyo kuteuliwa kwakwe kuiongoza TIB ilikuwa ni kuhadaa wananchi na kuficha ukweli.

  Kwa Rais kumteua mtuhumiwa wa wizi wa EPA kuiongoza TIB na Baadaye kutudanganya kuwa hizo hela keshazipeleka TIB na kumkabidhi Peter Noni ni kutufanya wananchi viazi, wapumbavu na mazezeta. Kimsingi hapa Rais amejipambanua kama mhusika ktk hili sakata la EPA. Ukichunguza kwa undani unaweza kukuta hizo fedha hazikupelekwa kabisa TIB, ila kwa kuwa TIB inaongozwa na mtuhumiwa wa huo ufisadi tumedanganywa tu.

  Hivi nini hasa sababu ya sisi wananchi kufanywa wapumbavu??Hivi Rais hakuona mwingine wa kumweka TIB zaid ya huyu Peter Noni ambaye ni mtuhumiwa wa EPA pia???hivi kweli sisi wananchi hatuna cha kufanya katika ujinga kama huu???kwann tuliowaamini kutuongoza leo wamekuwa wanatuhujumu??Nini hasa sababu ya kuwa na serikali isiyoaminika kama hii? Kama inashindwa kuaminika kwa fedha ndogo kama hizi kwa nn tuwaamin kwa kuwaachia nchi na rasilimali zake?

  Hivi hakuna utaratibu wa kuondoa viongozi wezi kama hawa? Nani aliyeiamuru TIB kukopesha hao walioshindwa kurudisha hizo fedha???Naomba tumjue aliye amuru, PCCB, wataalam wa Intellejensia (KOVA na Mwema) hamuoni kama kunaharufu ya Rushwa hapo???Hakuna kitu mnaweza fanya hapo kwa Kiongozi aliyeagiza hela ya wananchi zitoke kienyeji?

  Kwa utaratibu huu wa kutoa mikopo kwa kujuana, TIB itasurvive? Tunapoelekea naona Serikali itatutia kidole jichoni, nadhani inatosha.................................Nakaribisha mawazo yenu wanaJF nn kifanyike kukomesha hii hali.

  Mwananchi 03/11/2011​
   
 2. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hii nchi inaongozwa na fisi mwitu, hawa jamaa wanatamaa mpaka inatia kinyaa! Majizi yenye kufikiria matumbo yao tuu, wanaacha wagonjwa wafe kwa kukosa madawa mahospitalini, wanafunzi wanakaa chini, shule hazina walimu, wanafunzi wa vyuo hawana mikopo, foleni za magari kila kukicha, wao wanachowaza matumbo yao tuu. Ipo siku.
   
 3. R

  Rugemeleza Verified User

  #3
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Vigogo watafuna marejesho ya EPA [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 03 November 2011 21:27 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Deo Filikunjombe (katikati) akiwasisitizia jambo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Uwekezaji (TIB) Peter Noni (kulia) na Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya Benki hiyo Mgana Msindai mara baada ya kupitishwa hesabu za benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.Picha na Said Powa

  Leon Bahati na Furaha Maugo
  KAMATI ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imebaini ufisadi mwingine wa mabilioni ya fedha kwenye marejesho ya zile zilizochotwa awali kifisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).Fedha hizo zaidi ya Sh50 bilioni zilizorejeshwa na Rais Jakaya Kikwete kutangaza kuwa zitatumika kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo nchini, zinadaiwa kuchotwa kwenye Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) kwa amri iliyotoka kwa vigogo serikalini.

  Mkurugenzi wa TIB, Peter Noni alikiri jana mbele ya POAC kuwa sehemu ya Sh20 bilioni zilizotolewa na Hazina kwenda kwenye benki hiyo kwa ajili ya dirisha la kilimo, Serikali iliamuru zitolewe kama mkopo kwa wafanyabiashara ambao iliwataja kwa majina.

  "Mbaya zaidi, baadhi ya wafanyabiashara waliopewa mikopo hiyo wanaonekana kukwama kurejesha, huku wakitoa ahadi ambazo hawazitekelezi," Noni alisema.

  Wabunge wengi wa POAC walionyesha kushangazwa na jinsi serikali ilivyoingilia kati TIB na kuchagua watu ambao wanapaswa kupatiwa mikopo.Huku miongoni mwa wabunge hao wakisema wana taarifa za vigogo walioingia mlango wa nyuma na kuchukua tena fedha hizo katika mazingira ya kifisadi, waliendelea kumbana Noni kwa maswali.Ingawa baadhi ya wabunge walimtaka mkurugenzi huyo wa TIB awataje kwa majini vigogo hao, Makamu Mwenyekiti wa POAC, Deo Filikunjombe, alisita na kumtaka Noni asitaje majina hayo.

  Miongoni mwa wabunge waliotaka majina ya vigogo hao yawekwe hadharani ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya aliyesema, "Nina habari kuwa baadhi ya vigogo walihusika katika kupata mikopo hiyo… Naomba uyataje majina yao."

  Filikunjombe, alisema hakuna haja ya kutaja majina ya vigogo hao ambao alisema miongoni yamo kwenye taarifa waliyopatiwa kuhusu utendaji mzima wa TIB.

  Lakini Noni ambaye alikuwa anasaidiwa pia na wasaidizi wake kujibu baadhi ya maswali mazito yaliyoulizwa na wabunge, alisema hakuna tatizo kutaja baadhi ya kampuni zilizohusika kwenye mikopo hiyo ambayo sasa inawatoa jasho TIB.

  Noni alitaja mbele ya kamati hiyo kuwa moja ya kampuni zilizochukua fedha hizo na sasa zinaonyesha wasiwasi katika kuzirejesha ni Simon Group Ltd.Nyingine ni kampuni tano za kuuza maua nje ya nchi zenye makao yake makuu mjini Arusha, zikiwepo Tengeru Flowers na Mount Meru Flowers.
  Kuhusu Kampuni ya Simon Group, ambayo ilielezwa kuwa ilikopeshwa Sh5 bilioni Noni alisema; "Tumekutana nao mara kadhaa na kutoa ahadi lakini hawakuzitekeleza."
  Aliongoza kuwa kampuni za kuuza maua nje ya nchi zilieleza tatizo lililowafanya kushindwa kurejesha mikopo hiyo kulingana na makubaliano kwamba, ni hasara waliyoipata kutokana na mdororo wa kiuchumi duniani.

  Alifahamisha kuwa kutokana na hali hiyo, Serikali iliwaonea huruma na kuwaongezea kipindi cha miaka miwili kulipa deni hilo, muda ambao pia umeonekana kutotosha.

  Ila akaahidi kwamba TIB itaanza mchakato wa kuwabana wadeni hao kwa kunadi mali ambazo ziliwekwa rehani wakati wa kuchukua mikopo hiyo.

  "Uandaaji na usafirishaji wa maua walisema unahitaji gharama kubwa… Walilazimika kupitia Nairobi (Kenya)… Serikali iliona huruma ikawaongezea kipindi cha kulipa deni hilo," alisema Noni huku wabunge wengi wakionyesha shauku ya kuendelea kumbana kwa maswali.

  Miongoni mwa maswali yaliyoulizwa ni kwa nini TIB ilikubali kutoa mkopo kwa biashara ambazo hazitabiriki? Noni aliweka wazi kwamba, benki hiyo haikuhusika katika mchakato wa kuchambua na kuridhia mikopo kutolewa kwa kampuni hizo.

  Filikunjombe ambaye ni Mbunge wa Ludewa, alishangazwa na jinsi Serikali ilivyoingilia uhuru wa TIB na kuweka wazi kwamba si mara ya kwanza Serikali kuingilia mashirika ya umma kiutendaji na kwamba, historia inaonyesha kila ilipofanya hivyo iliziingiza taasisi hizo kwenye mzozo.

  "Serikali iliwahi kuingilia kati na kushawishi Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania) kuingia mikataba (ya kuzalisha umeme wa dharura) na Richmond na Dowans na kusababisha mzozo," alitoa mfano Filikonjombe.
  Hivyo, akaonya TIB kuhusu kupokea maagizo holela Serikalini kwa sababu mzigo wa matatizo yatakayotokea, itajiweka kando na kuiachia taasisi hiyo ya umma lawama na vibano kutoka kwa wananchi.
  Mapendekezo ya Kamati
  Ili kuikoa benki hiyo, Filikunjombe alitoa mapendekezo sita ambayo miongoni mwake ni kuitaka TIB ijitegemee na kufanya kazi zake kama shirika la umme lenye uwezo wa kufanya maamuzi yake ya kiutendaji bila kuingiliwa na wanasiasa serikalini.

  "Mhakikishe hamuingiliwi na Wizara ya Fedha au Serikali katika suala la utoaji wa mikopo," alishauri Filikonjombe.
  Mapendekezo mengine ni muundo wa manunuzi katika taasisi yao uendane na sheria ya manunuzi, kuwa ni mikakati ya kushindana kibiashara na benki nyingine na kuhakikisha kuwa mtaji unakua.

  Katika hatua nyingine, POAC ilishangazwa kuona kuwa kati ya zaidi ya Sh50 bilioni zilizokusanywa kwenye marejesho ya fedha zilizochotwa EPA, ni Sh20 bilioni pekee zilizoifikia TIB.
  Wabunge hao walielezea kushangazwa na kitendo cha Menejimenti ya TIB kupokea fedha hizo tu na kushindwa kuishinikiza Serikali itoe fedha zaidi.

  Noni alisema kuwa TIB haikuwa na mamlaka ya kuishinikiza Serikali ili iipatie fedha zote za marejesho ya EPA.
  "Sisi tulichopewa ndiyo hicho. Hatukuwa na sababu ya kudai fedha zaidi," alisema huku akizidi kuzua mtafaruku wa maswali kwa wabunge hao.

  Wabunge wengi walionyesha kuamini kuwa fedha zote zilipelekwa TIB baada ya Serikali kuahidi kuwa fedha za marejesho hayo zitapelekwa kwenye shughuli za kilimo.

  TIB ndiyo benki iliyoanzishwa na Serikali kwa malengo ya kuinua kilimo nchini ambacho kinategemewa na asilimia 80 ya Watanzania.Wananchi wengi wanaojishughulisha na kilimo nchini ndio wanaogubikwa na wimbi la umasikini kuliko sekta nyingine.

  Hata hivyo, Serikali imeamua kuanzisha kampeni ya Kilimo Kwanza, yenye lengo la kufanya sekta hiyo kuwa yenye manufaa na inayoweza kuleta utajiri tofauti na mwonekano wa sasa wa kuwa ni ya kundi la wasio na taaluma.
  Taarifa nyingine zilizopatikana jana baada ya kamati hiyo kumaliza kikao chake ni kwamba sehemu ya marejesho ya fedha za EPA, mbali na zile Sh20 bilioni zilizopelekwa TIB, zilitolewa kwa moja kwa moja kwa kampuni za pembejeo za kilimo.

  Hata hivyo, baadhi ya wabunge walielezea kutokuwa na imani kama fedha hizo zilitumika kikamilifu kwa ajili ya pembejeo hizo za kilimo.

  Mmoja wa wabunge kutoka CCM ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini alisema kuna uwezekano fedha hizo zimeliwa na wajanja.

  "Hata ukiangalia suala la marejesho halikuwekwa wazi, maana Rais (Kikwete) mwenyewe alisema zimekusanywa Sh53 bilioni, mara wengine wakasema 60 bilioni na wengine 70 bilioni.Alisema kama ufisadi uliweza kupenya hadi fedha zilizotolewa kwenye taasisi makini ya benki (TIB) basi hakuna shaka hata zilizotolewa kimyakimya ziliingia kwenye mikono hiyo ya mafisadi.
  Hata hivyo, gazeti la serikali liliwahi kumnukuu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mohamed Muya, akisema katika mgawanyo wa fedha za EPA, wizara hiyo ilipewa Sh40 bilioni ambapo Sh30 bilioni zilitumika kwa ruzuku ya pembejeo ya mbolea hali ambayo imesaidia katika uzalishaji. 


  "Kutokana na ruzuku hizi, hata idadi ya wakulima wanaopata vocha za ruzuku hiyo imeongezeka kutoka wakulima 500,000 hadi wakulima milioni 1.5 mwaka huu na kupitia Kamati ya Maafa na ya Usalama wa Chakula, hali ya chakula mwaka huu ni nzuri kuliko mwaka jana," alisema Muya.   Alisema katika fedha hizo za EPA, Sh10 bilioni zilizobaki zilitumika katika maeneo matatu ya kilimo ambayo ni Mfuko wa Pembejeo ambao ulipewa Sh3 bilioni, Wakala wa Mbegu wa Taifa Sh1 bilioni na kutatua matatizo ya visumbufu kama vile nzige, kweleakwelea na viwavijeshi Sh6 bilioni.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Chanzo: Mwananchi
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,307
  Likes Received: 22,111
  Trophy Points: 280
  Kikewete piga chini, eidha umeshindwa kazi ya kudhibiti wizi, au na wewe ni mwizi.
   
 5. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,084
  Likes Received: 7,314
  Trophy Points: 280
  Au vyote kwa pamoja!!!
   
 6. Nkoboiboi

  Nkoboiboi JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nami naanza safari ya kujipeleka jela kama Lema..... Nchi hii kwisha......!!!!!
   
 7. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,997
  Likes Received: 2,653
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa watu mbona wanatudharau sana?yaani wameshatufanya kama mandondocha,hivi watatuchezea mpaka lini?Amka Tanzania.
   
 8. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  kelele zooote zile.. kuanzia baba yao na wanae wote walafi...Nyumba ina mende hadi kwenye friji sasa sijui tutahifadhi wapi kiporo!!inauma kweli hadi maneno ya kusema hayatoki
   
 9. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ninakerwa mimi na mafisadi, laiti kama ningepewa nafasi ya kuongoza nchi hata kwa wiki moja wangenikoma. Ufisadi ni ubinafsi uliokithiri ambao unasababisha mateso na maudhi ya moyo physically and mentally. Ingelikuwa ni amri yangu, napiga risasi wote.
   
 10. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,601
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Eti serikali iliwaonea huruma! Hii serikali kama ingekuwa na huruma isingeacha wananchi wake wafe kwa kukosa panadol.,, na ingeshughuilikia madai yote inayodaiwa na watumishi wake, lakini pia ingechukulia hatua kali za kisheria wale wote waliothibitika kwa ufisadi..ulodidimiza ustawi wa Tanzania hii. Yako mengi ya kusema na yanayotia kichefchef.. Na si kweli kuwa serikali inahuruma si kweli kabisa.
   
 11. HT

  HT JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  sasa huyu deo amekataa asiwataje kwa nini? Hizo pesa si ni zetu?
   
 12. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,840
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  JAMANI WANA JF LET CONNECT DOTS TUSIWE WASAHULIFU!! SIMON GROUP KAKOPA 5 Billions TIB!!! Kweli Tanzania ni zaidi tuijuavyo!! Hii ndio Kampuni iliyomlipa Iddi Simba Consultancy fee ya milioni 300!! Ndio Iliyochukua UDA kwa bei ya Jalalani!! Jee tutafika? Nani Yupo Nyuma ya Pazia?[HR][/HR]
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Noni alitaja mbele ya kamati hiyo kuwa moja ya kampuni zilizochukua fedha hizo na sasa zinaonyesha wasiwasi katika kuzirejesha ni Simon Group Ltd.....Kuhusu Kampuni ya Simon Group, ambayo ilielezwa kuwa ilikopeshwa Sh5 bilioni Noni alisema; “Tumekutana nao mara kadhaa na kutoa ahadi lakini hawakuzitekeleza.”


  Simon Group Ltd ndio wale walionunua UDA?

  Kuna kitu sijaelewa hapa, kama mkopajii anashindwa kulipa deni kwa nini TIB wasipige mnada assets zao? Walikopa kwa collateral assets gani? Kila mara tunaona nyumba za wakopaji zinauzwa na bank kwa sababu wameshindwa kulipa deni kwa nini TIB wanafanya mazungumzo na matapeli?

  Pia nahisi huyu makamu mwenyekiti wa POAC Deo Filikunjombe ni msanii. Amepitishaje mahesabu ya TIB wakati kuna madudu kama haya?
   
 14. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Haya ndio mambo yatakayoiua amani ya Tanzania. Ikitokea 'wanaume' wa kazi wakaratibu maandamano basi kila asiye na ubongo atasema CHADEMA wanaleta fujo. Sasa hii kama sio dharau ni nini?

  Hawa watu wanatufanya sisi ma-bimkubwa tusio na ubongo. Kama hakuna njia ya ku-deal na hawa watu separately basi nguvu ya umma itachukua mkondo wake. Ni suala la wakati tu
   
 15. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kulindana ndo jadi yetu...
  huenda na yeye yumo...
   
 16. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  hawa simon group wana uhusiano gani na kilimo kwanza kama pesa ya EPA ilitolewa kwa ajili ya kilimo??
   
 17. K

  Kiponya Member

  #17
  Nov 4, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtaniwia radhi kwa swali nitakalouliza! Hivi tangu hao wanaodaiwa kushindwa kulipa wamekopeshwa mpaka sasa ni muda gani? uelewa wangu unaniambia kuna kitu kinaitwa grace period kwenye mkopo na fedha nyingi kama hizo say 5 billion huwezi kukopa na kuanza kulipa mara moja. Kumbukumbu zangu zinaniambia kwamba tangu wamekopeshwa muda si mrefu kiasi cha kushindwa kulipa.
   
 18. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Jk anahusika 100% bila kumumunya maneno!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 19. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280

  Kiukweli wezi wetu ni wachache sana, Yani ni walewale kila siku!
  Huwezi hamini zunguka kote utakuta MKUBWA wao ni yuleyule kwasasa KIKWETE!!
  Na akitoka wataweka mwingine.
   
 20. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  [TABLE="align: center"]
  [TR="bgcolor: #FFFFFF"]
  [TD]TENGERU FLOWERS LTD[/TD]
  [TD="bgcolor: #CCCCCC, colspan: 2"]MARK C. NGALO
  GENERAL MANAGER[/TD]
  [TD="width: 244"]P. O. BOX 3003
  ARUSHA
  Tel: +255 27 2553834
  Fax: +255 27 250 8092
  Cell: +255 754 858588
  E-mail: teflo@habari.co.tz
  Website: www.tengeruflowers.com[/TD]
  [TD="width: 284, bgcolor: #CCCCCC"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  [TABLE="width: 920, align: center"]
  [TR]
  [TD="width: 176, bgcolor: #00CCCC"]MT. MERU FLOWERS LTD
  [/TD]
  [TD="width: 175, bgcolor: #336666"]HERWIG TRETTER
  CEO
  [/TD]
  [TD="bgcolor: #00CC99, colspan: 2"]P. O. BOX 285
  ARUSHA
  Tel: +255 27 2553041
  Fax: +255 27 2553179
  E-mail: ht@mount-meru-flowers.com
  Website: www.mount-meru-flowers.com
  [/TD]
  [TD="width: 284, bgcolor: #3366CC"]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...