FBI ndani ya Tanzania, kazi ipo

FBI ndani ya Tanzania, kazi ipo

MAOFISA wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), wamekubali kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri Evaristus Mushi yaliyotokea Zanzibar Februari 17, mwaka huu.

Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizopatikana jana maofisa hao wako nchini na tayari wamekutana na baadhi ya viongozi wa Serikali kwa ajili ya kuanza kazi hiyo.

Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa maofisa hao walikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kwa ajili ya kuangalia ni namna gani watafanya shughuli zao katika upelelezi huo.

Kutua kwa maofisa hao kumekuja baada ya kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete katika salamu zake za rambirambi baada ya mauaji ya Padri Mushi kuwa ameliagiza Jeshi la Polisi kutumia nguvu zake zote pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama vya hapa nchini na mashirika ya upelelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji hayo.

Pamoja na ushiriki wa FBI, pia Serikali inazungumza na nchi nyingine rafiki ili kushirikiana nao katika upelelezi ya matukio mengine ya mauaji ya hivi karibuni.

Taarifa zinaeleza kuwa maofisa wa Serikali wamezungumza na taasisi za upelelezi za nchi tano ili kuongeza nguvu katika kazi hiyo.
Taasisi nyingine inayotajwa kwamba huenda ikashiriki katika uchunguzi huo ni Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Uingereza ya Scotland Yard.

Hatua hizi zinakuja baada ya Dk Nchimbi kutoa tamko la Serikali, Jumapili iliyopita, akidai kuwa mauaji ya Padri Mushi yalikuwa ya kigaidi hivyo Serikali itachukua hatua kali kuhakikisha waliohusika wanakamatwa.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa Serikali ya Tanzania kushirikiana na asasi za kimataifa katika ku chunguza matukio ya uhalifu na yale ya kigaidi.
Hii itakuwa mara ya pili kwa FBI kuja nchini kufanya operesheni kubwa ya upelelezi. Mwaka 1998, walifika kuchunguza kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani na kugundua ilikuwa kazi ya Kundi la Al-Qaeda.

Pia mwaka 1984 walikuja wapelelezi kutoka Scotland Yard kuchunguza kuungua kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima alithibitisha Serikali kuanza mazungumzo na mashirika mbalimbali ya upelelezi duniani kwa ajili ya kushirikiana nayo kuchunguza mauaji ya Padri Mushi.

Alisema tayari wameanza kufanya mazungumzo na mashirika hayo kutoka nchi mbalimbali, lakini alisema ni mapema mno kuyataja... “Ilatukikamilisha kila kitu tutawaiteni na kuwaeleza hatua tuliyofikia, ila tumeanza kufanya mazungumzo nayo. Kama unavyojua Rais Kikwete alitoa agizo hilo, sisi tumeanza kulitekeleza.”

Waziri Silima alisema kwanza wataanza kuchunguza mauaji ya Padri Mushi... “Tutaanza kuchunguza kwanza chanzo cha mauaji haya ili tujue kila kitu.”

Watuhumiwa wakamatwa
Polisi Zanzibar inawashikilia watu kadhaa wakihusishwa na mauaji ya Padri Mushi.

“Tumekamata watu kadhaa kuhusiana na kifo cha Padri na tunaendelea kuwahoji na wengine tutawaachia,” alisema Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa jana.

Source: Mwananchi

Iko wapi Intelejensia inayo ona vurugu za CDM kabla ya kufanyika kwa mikutano yao? Mbona tunafanyana wajinga jamani? Intelejensia ya nchi hii ni kwaajili ya CHADEMA tu? Hao FBI wanajua kiswahili au watakuwa wanarekodi na kuweka kwenye program za tafsiri??

Waache wakali bata Zenji ila ukweli tunao Watanzania wenyewe na Jeshi letu la Polisi ambalo taarifa za Kiintelejensia zinapatikana kwenye Maandamano ya CHADEMA tu.
 
Safi sana FBI pia waje na kwny uchaguzi 2015 upinzani wanalalamika sana waje wawaumbue upinzani na madai yao mbuzi
 
shehe ilunga nae anahitaji kuchunguzwa na watu wa hayo mashirika?!!
 
Duuuhhh....Hiv Kesi ya Mwangosi iliishia wap raia??, Vip na Kesi ya Dokta Ulimboka nae...Naomba hii ya Padri watu wachukuliwe hatua kweli siyo porojo
Itabidi wakati FBI wanaendelea na uchunguzi wa mauaji ya Padri Mushi, wapeleleze pia mauaji ya Mwangosi na kutekwa kwa Dr Ulimboka, ili usanií tuliofanyiwa na Kova kuhusu yule mkenya wake kichaa ambaye anadaí ndiye aliyemteka Ulimboka na yule Polisi aliyemfyatulia bomu Mwangosi kwa amri ya RPC Kamuhanda ili mbivu na mbichi zifahamike katika utata mkubwa uliogubika kesí hizo mbili!!
 
CCM wameharibu jeshi letu na sasa wamelitosa,limebaki kufanya kazi za siasa tu.!
 
Hii nchi inaenda kubaya, tukiendelea hivi nayo itabinafsishwa
 
Usalama wa taifa hawawezi kufanya jambo lolote kilewo. Wanalinda maslahi ya Chama Tawala (CT).
Ni aibu kubwa ila naanza kuwa na hisia tofauti katika hili suala. Nahisi ni njama tu zimefanyika ilihali wakijua watawashirikisha wana usalama toka maeneo mengine ya duniani. Nahisi kuna upigaji wa hela unataka kufanyika au kuna uwezekano mkubwa hii ni pressure from US ikiwa ni njia ya kuja kuchukua wese na gesi iliyopo hapa.
Mda bado upo na tuendelee kujifunza kwa kadri ya muda tuliopewa.
 
CCM wameharibu jeshi letu na sasa wamelitosa,limebaki kufanya kazi za siasa tu.!

Kwani walipoajiri makada kufanya kazi za kipolisi ulikuwa wapi ??au walikuwa wakiuwa waislamu na ilikuwa ni sawa tu??
 
MAOFISA wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), wamekubali kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri Evaristus Mushi yaliyotokea Zanzibar Februari 17, mwaka huu.

Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizopatikana jana maofisa hao wako nchini na tayari wamekutana na baadhi ya viongozi wa Serikali kwa ajili ya kuanza kazi hiyo.

Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa maofisa hao walikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kwa ajili ya kuangalia ni namna gani watafanya shughuli zao katika upelelezi huo.

Kutua kwa maofisa hao kumekuja baada ya kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete katika salamu zake za rambirambi baada ya mauaji ya Padri Mushi kuwa ameliagiza Jeshi la Polisi kutumia nguvu zake zote pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama vya hapa nchini na mashirika ya upelelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji hayo.

Pamoja na ushiriki wa FBI, pia Serikali inazungumza na nchi nyingine rafiki ili kushirikiana nao katika upelelezi ya matukio mengine ya mauaji ya hivi karibuni.

Taarifa zinaeleza kuwa maofisa wa Serikali wamezungumza na taasisi za upelelezi za nchi tano ili kuongeza nguvu katika kazi hiyo.
Taasisi nyingine inayotajwa kwamba huenda ikashiriki katika uchunguzi huo ni Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Uingereza ya Scotland Yard.

Hatua hizi zinakuja baada ya Dk Nchimbi kutoa tamko la Serikali, Jumapili iliyopita, akidai kuwa mauaji ya Padri Mushi yalikuwa ya kigaidi hivyo Serikali itachukua hatua kali kuhakikisha waliohusika wanakamatwa.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa Serikali ya Tanzania kushirikiana na asasi za kimataifa katika ku chunguza matukio ya uhalifu na yale ya kigaidi.
Hii itakuwa mara ya pili kwa FBI kuja nchini kufanya operesheni kubwa ya upelelezi. Mwaka 1998, walifika kuchunguza kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani na kugundua ilikuwa kazi ya Kundi la Al-Qaeda.

Pia mwaka 1984 walikuja wapelelezi kutoka Scotland Yard kuchunguza kuungua kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima alithibitisha Serikali kuanza mazungumzo na mashirika mbalimbali ya upelelezi duniani kwa ajili ya kushirikiana nayo kuchunguza mauaji ya Padri Mushi.

Alisema tayari wameanza kufanya mazungumzo na mashirika hayo kutoka nchi mbalimbali, lakini alisema ni mapema mno kuyataja... “Ilatukikamilisha kila kitu tutawaiteni na kuwaeleza hatua tuliyofikia, ila tumeanza kufanya mazungumzo nayo. Kama unavyojua Rais Kikwete alitoa agizo hilo, sisi tumeanza kulitekeleza.”

Waziri Silima alisema kwanza wataanza kuchunguza mauaji ya Padri Mushi... “Tutaanza kuchunguza kwanza chanzo cha mauaji haya ili tujue kila kitu.”

Watuhumiwa wakamatwa
Polisi Zanzibar inawashikilia watu kadhaa wakihusishwa na mauaji ya Padri Mushi.

“Tumekamata watu kadhaa kuhusiana na kifo cha Padri na tunaendelea kuwahoji na wengine tutawaachia,” alisema Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa jana.

Source: Mwananchi

Dah kina borafya silima na majanhaweed wao....loh naona hapa kuna kuadhirika
 
Yaaani tunashindwa kumkamata hata muuaji hadi tuite FBI?? Kwani ule "mkono mrefu wa serikali" ulikatika? au sikuhizi umepooza au umepata kiharusi? au ni mrefu tu kwa wanachadema??? Hahahahahaaaaa kazi ipo
CC: zumbemkuu MANI saudari

""""Yakhe huyo ntoto alomuua Padiri Mushi ni ntoto wa Makame mimi Shamte nikinkamata nitaleta uhasama yakhe!! Bora waje FUBIA hao wankamate venyeweI!!!!""""
 
Nkobe iliwahi kugusia mkasa ule wa kuangusha utawala wa Gadafi kwamba baada ya NATO kuharibu kabisa ile nchi bado waliwapelekea "bill" ya gharama za kazi ile; hawa viongozi wetu wamewaita tuu hao wapelelezi au wameangalia na "cost implication" kwa nchi hii yetu maskini wa kutupwa?
 
Last edited by a moderator:
Yaaani tunashindwa kumkamata hata muuaji hadi tuite FBI?? Kwani ule "mkono mrefu wa serikali" ulikatika? au sikuhizi umepooza au umepata kiharusi? au ni mrefu tu kwa wanachadema??? Hahahahahaaaaa kazi ipo
CC: zumbemkuu MANI saudari
Na huo mkono mrefu ni wa kukamata viongozi wa chadema tu, ikija kwa akina Ilunga unakuwa mfupi.
 
Siamini kama wanaweza kuja kukagua mabusha ya wapemba
 
Wajaribu kwenda kule MOSAD and CIA and likely FBI ila hapo wakali zaidi ni hao Israel Mosad mara moja watakamatwa na kufikishwa mahakamani wote maana wayahudi walizoea mambo kama haya
 
Back
Top Bottom