FBI Hawapo Arusha, polisi ni wazushi!

FBI Hawapo Arusha, polisi ni wazushi!

Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
5,143
Reaction score
3,209
Hivi jamani hawa polisi wa Tanzania huwa wanafanya mambo haya kwa faida ya nani? Inashangaza sana kututangazia kwamba FBI wapo Arusha wanasaidiana na polisi wetu kufanya uchunguzi kuhusu mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa CHADEMA, ilihali ni uongo mkubwa kabisa.

Kusema ukweli, hata mimi ningeshangaa kama polisi waliorusha bomu na kupiga watu risasi wangeleta FBI kufanya uchunguzi. Maana kisheria na taratibu FBI huwa hawana unafiki, na hawana tabia ya kuandika report za uongo. Kwa hakika wangewaumbua polisi wauaji wa Tanzania na serikali yake ya kigaidi.

Juzi hapa viongozi wa CHADEMA wamelalamika kwamba hawajakutana na FBI hata mmoja kwa ajili ya kuwauliza chochote kuhusiana na mlipuko, na walionyesha kushangaa kwamba hao FBI wanafanya kazi na nani! Lakini taarifa za uhakika kutoka ubalozi wa marekani kama zilivyoripotiwa na gazeti la The citizen zinaonyesha kwamba FBI hawapo Arusha, na kamanda wa polisi wa Arusha alipoulizwa alithibitisha hilo.

Sasa ninajiuliza walipotutangazia kwamba FBI wapo Arusha walitaka nini? Ni dhahiri walitaka kupika report ya uongo na kukizushia kesi chadema na ili wasingizie kwamba FBI ndiyo wamegundua hayo!

Hivi katika haya, tuendelee kuwa na imani na jeshi la polisi? Hivi CCM wameshindwa kabisa kucheza fair game hadi watake kufanya haya jamani?

US security agents not in Arusha, says embassy - National - thecitizen.co.tz
 
Tatizo baadhi ya Wabongo wakiona wazungu wanaranda randa mjini basi wanadhani ni FBI.

Kila mzungu ni FBI. Hata USSS Canine Unit waliodaiwa kwenda ofisini kwa Kova na ku-perform security sweeps nao eti ni FBI.

Haijalishi mzungu ni raia wa wapi. Anaweza akawa anatokea Estonia huko. Kwa Wabongo atakuwa FBI tu.
 
FBI wapo Arusha. Acheni kupotosha watu nyie. Hivi nyie Bavicha mbona wambea sana?
 
Kama polisi ama propaganda machine ya ccm ndo walioi fabricate hiyo habari ya fbi kuwepo Arusha,basi pengine walijiandaa kupata fbi feki ili waipate hiyo video ambayo chadema wanadai kuwanayo.Ama pia mbinu ya kuwazuga na kwasahaulisha wananchi.
 
The good thing is that I always respect your opinions. You always try as much as possible to be neutral and objective. So I consider this comment is more of a joke rather than a serious allegation against BAVICHA. You are provided the link; you got to prove what is written!
 
Tatizo baadhi ya Wabongo wakiona wazungu wanaranda randa mjini basi wanadhani ni FBI.

Kila mzungu ni FBI. Hata USSS Canine Unit waliodaiwa kwenda ofisini kwa Kova na ku-perform security sweeps nao eti ni FBI.

Haijalishi mzungu ni raia wa wapi. Anaweza akawa anatokea Estonia huko. Kwa Wabongo atakuwa FBI tu.
Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, taarifa za awali za kuwepo kwa FBI wakifanya uchunguzi wa bomu la Soweto zilitolewa na kamanda wa operation. Sasa sidhani kama watu waliibuka na hoja ya FBI baada ya kuona wazungu, maana kama ni wazungu Arusha ndiyo nyumbani. Bye the way, kama hizi habari zingekuwa ni za mitaani, the citizen wasingezipa umhimu mkubwa hivyo kiasi cha kumwandikia email balozi wa marekani.
 
Jeshi la Vilaza hata sio la kuliamini...maana wao wanashindana kwa ukubwa wa matumbo lakini sio utendaji.
 
Ni aibu ya hali ya juu Mkuu kwa polisi kutoa kauli za uongo. Polisi magamba kutoa kauli za uongo ni jadi yao kwa miaka mingi sasa. Halafu eti bado wanaaminika kuweza kuwalinda Watanzania na mali zao!!!!

Kama polisi ama propaganda machine ya ccm ndo walioi fabricate hiyo habari ya fbi kuwepo Arusha,basi pengine walijiandaa kupata fbi feki ili waipate hiyo video ambayo chadema wanadai kuwanayo.Ama pia mbinu ya kuwazuga na kwasahaulisha wananchi.
 
Ni aibu ya hali ya juu Mkuu kwa polisi kutoa kauli za uongo. Polisi magamba kutoa kauli za uongo ni jadi yao kwa miaka mingi sasa. Halafu eti bado wanaaminika kuweza kuwalinda Watanzania na mali zao!!!!

Mkuu kwa wenzetu uongo wa hadharani hivi ni kosa kubwa sana la kumcost mtu kazi yake.Lakini kwa bongo wala si big deal.
 
Namsifu waziri mkuu Pinda yeye husema na kufanya ayafanyayo na inapofika siku kama ya kesho anakwenda zake Kanisani Kungama na kusamehewa huko anasubiri matukio mengine .
 
Radhia Sweety, hebu soma Citizen ya leo! Afisa habari wa ubalozi wa Marekani kakanusha hao FBI wako wametoka wapi?

Unafikiri radhia hajui ukweli. Achana nae huyo amekosa radhi za wazazi wake. Mwana mtoka pabaya. Anabisha kila kitu, au ni list ya lumumba?
 
Ni kweli Mkuu inasikitisha sana lakini ndio ukweli halisi. Hata rais wa nchi anaweza kudanganya hadharani na bado akaendelea kupeta. Maadili nchini kwetu ni SIFURI halafu tunadai eti tuna Tume ya maadili ya viongozi!!!

Mkuu kwa wenzetu uongo wa hadharani hivi ni kosa kubwa sana la kumcost mtu kazi yake.Lakini kwa bongo wala si big deal.
 
The good thing is that I always respect your opinions. You always try as much as possible to be neutral and objective. So I consider this comment is more of a joke rather than a serious allegation against BAVICHA. You are provided the link; you got to prove what is written!

I'll take a liberty to make some corrections on your English.
''Neutral'' and ''objective'' mean the same thing. So ''objective'' in ''You always try as much as possible to be neutral and objective'' is just redundant.
Another thing: ''I consider this comment is more of a joke rather tha a serious allegation against BAVICHA'' should be correctly written as ''I consider this comment to be a joke rather than a serious allegation...''
Finally, your last sentence should have been worded: ''You have to provide a link to provide a proof for your allegations.'' More clearly: ''Can you provide a proof to support your allegations?''
I hope it does help.
 
Hivi jamani hawa polisi wa Tanzania huwa wanafanya mambo haya kwa faida ya nani? Inashangaza sana kututangazia kwamba FBI wapo Arusha wanasaidiana na polisi wetu kufanya uchunguzi kuhusu mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa CHADEMA, ilihali ni uongo mkubwa kabisa.

Kusema ukweli, hata mimi ningeshangaa kama polisi waliorusha bomu na kupiga watu risasi wangeleta FBI kufanya uchunguzi. Maana kisheria na taratibu FBI huwa hawana unafiki, na hawana tabia ya kuandika report za uongo. Kwa hakika wangewaumbua polisi wauaji wa Tanzania na serikali yake ya kigaidi.

Juzi hapa viongozi wa CHADEMA wamelalamika kwamba hawajakutana na FBI hata mmoja kwa ajili ya kuwauliza chochote kuhusiana na mlipuko, na walionyesha kushangaa kwamba hao FBI wanafanya kazi na nani! Lakini taarifa za uhakika kutoka ubalozi wa marekani kama zilivyoripotiwa na gazeti la The citizen zinaonyesha kwamba FBI hawapo Arusha, na kamanda wa polisi wa Arusha alipoulizwa alithibitisha hilo.

Sasa ninajiuliza walipotutangazia kwamba FBI wapo Arusha walitaka nini? Ni dhahiri walitaka kupika report ya uongo na kukizushia kesi chadema na ili wasingizie kwamba FBI ndiyo wamegundua hayo!

Hivi katika haya, tuendelee kuwa na imani na jeshi la polisi? Hivi CCM wameshindwa kabisa kucheza fair game hadi watake kufanya haya jamani?

US security agents not in Arusha, says embassy - National - thecitizen.co.tz

Ninakumbuka kilichosemwa officially na Mkuu wa Mkoa ni kuwepo kwa Wachina kufuatilia kujua bomu hilo liliuzwa kwa taasisi au mtu gani. Ambayo pia sikuamini kwa sababu haihitaji wachina kuja huku kufanya hilo wakishapata namba za bomu lenyewe. Nafikiri hili la FBI lilivumishwa tu - at least sikumbuki kusikia au kuona taarifa maalumu kuhusisha FBI.
 
Kiingereza cha Lukolo kwenda kwa Radhia KIPO SAHIHI, tena cha HALI YA JUU SANA.
 
Radhia Sweety, hebu soma Citizen ya leo! Afisa habari wa ubalozi wa Marekani kakanusha hao FBI wako wametoka wapi?

labda anadhani na huyu afisa wa ubalozi ni BAVICHA maana watu wengine bila kutaja BAVICHA hawaingizi siku.
 
I'll take a liberty to make some corrections on your English.
''Neutral'' and ''objective'' mean the same thing. So ''objective'' in ''You always try as much as possible to be neutral and objective'' is just redundant.
Another thing: ''I consider this comment is more of a joke rather tha a serious allegation against BAVICHA'' should be correctly written as ''I consider this comment to be a joke rather that a serious allegation...''
Finally, your last sentence should have been worded: ''You have to provide a link to provide a proof for your allegations.'' More clearly: ''Can you provide a proof to support your allegations?''
I hope it does help.

sasa hapo ume sahihisha nini kama sio uchizi.cdm inawachanganya kweli.
 
Back
Top Bottom