Fatma Karume akwaa kizingiti kingine, Jamhuri yakata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,563
1626161062195.png

PICHA: Fatma Karume

Jamhuri imewasilisha nia ya kukata rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu uliotengua uamuzi wa kumfuta katika orodha ya mawakili, Fatma Karume.

Nia hiyo ya kukata rufani imekwamisha maombi ya Fatma kupitia Wakili wake, Peter Kibatala, ya kutaka Msajili wa Mahakama Kuu atoe amri na kuelekeza mteja wake aendelee kufanya kazi ya uwakili.

Wakili Kibatala aliandika barua kwa Msajili wa Mahakama Kuu, akiomba mteja wao Karume aendelee kufanya kazi ya uwakili kama Mahakama hiyo ilivyoamuru Juni 21, mwaka huu.

Katika barua hiyo aliomba Msajili wa Mahakama Kuu aamuru na kuelekeza kwamba leseni namba 848 ya Karume iliyozuiliwa iendelee kutumika kwa kazi ya uwakili.

Msajili Sharmilla Sarwatt katika majibu yake aliwafahamisha kwamba mlalamikiwa Jamhuri katika rufani namba 2/2020 iliyokuwa Mahakama Kuu aliwasilisha nia ya kukata rufani akipinga uamuzi wa Mahakama hiyo uliotolewa Juni 21, mwaka huu.

Mahakama Kuu Masjala Kuu ilitengua uamuzi wa Kamati ya Mawakili iliyomfuta Karume katika orodha ya mawakili nchini.
Uamuzi huo ulitolewa na jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu, likiongozwa na Jaji Issa Maige, Jaji Deo John Nangela na Jaji Edwin Kakolaki.

Jopo hilo lilitoa uamuzi huo kutokana na rufani iliyokatwa na Karume akipinga uamuzi wa kusimamishwa uwakili uliotolewa na Kamati ya Mawakili.

Karume alifutiwa uwakili na kamati hiyo Septemba 23, mwaka 2020 kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na Adelardus Kilangi, akimtuhumu kukiuka maadili ya taaluma kwa kutumia lugha ya kumdhalilisha wakati akiwasili hoja za maandishi katika shauri alilokuwa akimwakilisha mteja wake Ado Shaibu.

Jaji Kiongozi, Dk. Eliezer Feleshi, alimsimamisha uwakili kwa muda Karume kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa na mawakili wa serikali katika kesi waliyokuwa wakimwakilisha Profesa Kilangi na Dk. John Magufuli na kuelekeza malalamiko hayo yasikilizwe na kamati.

Mahakama Kuu katika uamuzi wake wa kutengua ilikubaliana na sababu moja pekee ya rufani hiyo ambayo ilitosha kutengua uamuzi wa kamati hiyo.

Katika sababu hiyo ambayo Mahakama Kuu ilikubaliana nayo, Karume kupitia kwa wakili wake alidai kuwa kamati haikuwa na mamlaka ya kusikiliza malalamiko ya Profesa Kilangi kwa kuwa ilikuwa inakiuka uamuzi wa Jaji Kiongozi.

Mawakili wanaomtetea Fatma, Peter Kibatala na Dk. Rugemeleza Nshalla walipinga uamuzi wa kumsimamisha uwakili mteja wao uliotolewa na Kamati ya Maadili baada ya Jaji Kiongozi, Eliezer Feleshi mwaka 2019 kuelekeza shauri hilo likasikilizwe na kamati hiyo na kabla ya kufanya hivyo kamati ilianza kusikiliza malalamiko ya Kilangi.

Jopo hilo baada ya kupitia hoja mbalimbali zilizowasilishwa lilitengua adhabu ya kufutiwa uwakili na kutoa amri kwa ajili ya utekelezaji.
Mahakama katika uamuzi wake iliamuru malalamiko yapelekwe katika Kamati ya Mawakili watakaotoa uamuzi dhidi ya Karume.
"Kwa uamuzi huo Fatma atakuwa na nafasi ya kujitetea, amerudishiwa uwakili wake, hivyo anayo haki ya kujitetea," alisema Dk. Rugemeleza Nshalla.

Pia Mahakama Kuu iliamuru Msajili wa Mahakama hiyo ndio apeleke malalamiko kwenye kamati ya mawakili. Mahakama Kuu ilifuta mwenendo wote wa kamati ya maadili ya mawakili na kwamba hoja zao za kupinga kufutiwa uwakili Karume zilikuwa 13.

Karume alisimamishwa kazi huku sababu yake ikitajwa kuwa kile alichokizungumza katika kesi iliyofunguliwa na Ado.
Mawakili wa serikali walilalamikia maneno yalioandikwa na Karume wakati walipokua wakifungua kesi hiyo Mahakama Kuu.

Anadaiwa kuandika "hata iwapo kesi hii itashindwa, ataendelea kupambana nayo, rais akiondoka madarakani mwaka 2020 au kama ataondoka 2025 au kama mahakama itabadilika ataendelea kupambana”.
 
Mimi si Mwanasheria lakini kosa linalotajwa kutendwa na wakili Fatuma Karume ni la "kukiuka maadili ya uwakili wake"

Msingi wa kosa lake ulitokana na kuandika hivi alipokuwa anamtetea Ado Shaibu ktk kesi yake na eti hii ndo ikasababishwa kusimamishwa kwake uwakili...

"....hata iwapo kesi hii itashindwa, ataendelea kupambana nayo. Hata Rais Magufuli akiondoka madarakani mwaka 2020 au hata kama ni 2025 au hata kama mahakama itabadilika atarndelea kupambana...."

Sijui maadili ya Uwakili mimi kwa sababu mimi si wakili/mwanasheria, lakini kama hiyo statement hapo juu "ilikiuka maadili ya uwakili" basi professional ya sheria/uwakili ina shida na mapungufu makubwa...

Lakini all in all, huyu Dada Fatuma Karume, waliamua kumpunguza nguvu tu simply kwa sababu tu ya upinzani wake dhidi ya utawala wa wasukuma chini ya Mwendazake John P. Magufuli....!!
 
Kuna viumbe vinaitwa MaCCM vina roho dhaifu sana .
Yaani Shangazi wa Taifa kukataa ushenzi wao, wanataka kumuonyesha roho mbaya.
Nchi ya hovyo sana hii.
Na bi, Chokochoko yupo yupo tu mara atubanie sauti. mara atulegezee macho.
 
View attachment 1851406
PICHA: Fatma Karume

Jamhuri imewasilisha nia ya kukata rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu uliotengua uamuzi wa kumfuta katika orodha ya mawakili, Fatma Karume.

Nia hiyo ya kukata rufani imekwamisha maombi ya Fatma kupitia Wakili wake, Peter Kibatala, ya kutaka Msajili wa Mahakama Kuu atoe amri na kuelekeza mteja wake aendelee kufanya kazi ya uwakili.

Wakili Kibatala aliandika barua kwa Msajili wa Mahakama Kuu, akiomba mteja wao Karume aendelee kufanya kazi ya uwakili kama Mahakama hiyo ilivyoamuru Juni 21, mwaka huu.

Katika barua hiyo aliomba Msajili wa Mahakama Kuu aamuru na kuelekeza kwamba leseni namba 848 ya Karume iliyozuiliwa iendelee kutumika kwa kazi ya uwakili.

Msajili Sharmilla Sarwatt katika majibu yake aliwafahamisha kwamba mlalamikiwa Jamhuri katika rufani namba 2/2020 iliyokuwa Mahakama Kuu aliwasilisha nia ya kukata rufani akipinga uamuzi wa Mahakama hiyo uliotolewa Juni 21, mwaka huu.

Mahakama Kuu Masjala Kuu ilitengua uamuzi wa Kamati ya Mawakili iliyomfuta Karume katika orodha ya mawakili nchini.
Uamuzi huo ulitolewa na jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu, likiongozwa na Jaji Issa Maige, Jaji Deo John Nangela na Jaji Edwin Kakolaki.

Jopo hilo lilitoa uamuzi huo kutokana na rufani iliyokatwa na Karume akipinga uamuzi wa kusimamishwa uwakili uliotolewa na Kamati ya Mawakili.

Karume alifutiwa uwakili na kamati hiyo Septemba 23, mwaka 2020 kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na Adelardus Kilangi, akimtuhumu kukiuka maadili ya taaluma kwa kutumia lugha ya kumdhalilisha wakati akiwasili hoja za maandishi katika shauri alilokuwa akimwakilisha mteja wake Ado Shaibu.

Jaji Kiongozi, Dk. Eliezer Feleshi, alimsimamisha uwakili kwa muda Karume kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa na mawakili wa serikali katika kesi waliyokuwa wakimwakilisha Profesa Kilangi na Dk. John Magufuli na kuelekeza malalamiko hayo yasikilizwe na kamati.

Mahakama Kuu katika uamuzi wake wa kutengua ilikubaliana na sababu moja pekee ya rufani hiyo ambayo ilitosha kutengua uamuzi wa kamati hiyo.

Katika sababu hiyo ambayo Mahakama Kuu ilikubaliana nayo, Karume kupitia kwa wakili wake alidai kuwa kamati haikuwa na mamlaka ya kusikiliza malalamiko ya Profesa Kilangi kwa kuwa ilikuwa inakiuka uamuzi wa Jaji Kiongozi.

Mawakili wanaomtetea Fatma, Peter Kibatala na Dk. Rugemeleza Nshalla walipinga uamuzi wa kumsimamisha uwakili mteja wao uliotolewa na Kamati ya Maadili baada ya Jaji Kiongozi, Eliezer Feleshi mwaka 2019 kuelekeza shauri hilo likasikilizwe na kamati hiyo na kabla ya kufanya hivyo kamati ilianza kusikiliza malalamiko ya Kilangi.

Jopo hilo baada ya kupitia hoja mbalimbali zilizowasilishwa lilitengua adhabu ya kufutiwa uwakili na kutoa amri kwa ajili ya utekelezaji.
Mahakama katika uamuzi wake iliamuru malalamiko yapelekwe katika Kamati ya Mawakili watakaotoa uamuzi dhidi ya Karume.
"Kwa uamuzi huo Fatma atakuwa na nafasi ya kujitetea, amerudishiwa uwakili wake, hivyo anayo haki ya kujitetea," alisema Dk. Rugemeleza Nshalla.

Pia Mahakama Kuu iliamuru Msajili wa Mahakama hiyo ndio apeleke malalamiko kwenye kamati ya mawakili. Mahakama Kuu ilifuta mwenendo wote wa kamati ya maadili ya mawakili na kwamba hoja zao za kupinga kufutiwa uwakili Karume zilikuwa 13.

Karume alisimamishwa kazi huku sababu yake ikitajwa kuwa kile alichokizungumza katika kesi iliyofunguliwa na Ado.
Mawakili wa serikali walilalamikia maneno yalioandikwa na Karume wakati walipokua wakifungua kesi hiyo Mahakama Kuu.

Anadaiwa kuandika "hata iwapo kesi hii itashindwa, ataendelea kupambana nayo, rais akiondoka madarakani mwaka 2020 au kama ataondoka 2025 au kama mahakama itabadilika ataendelea kupambana”.
Yaani nchi hii mtu akisoma kidegree cha sheria eti ndo anajua kila kitu. Wenzetu wanapiga hatua katika sayansi,technolojia na kilimo
sisi tumebaki kuwa taifa la wanaharakati eti kwa sababu tunajua sheria basi tunaweza kufanya tunachotaka.
Ukitizama utagundua kuwa taifa letu limekosa ajenda mahususi kwenye elimu kitu pekee amabacho kitawafanya vijana wa taifa hili kuweza kupata uwezo wA kujiajiri na kutafuta fursa katika sehmu nyingine za dunia.
Tunachopaswa kufanya kwa sasa ni kuhakikisha kila mwananchi kufanyia kazi taalunma yake kwa manufaa ya taifa sio kuwa wajuaji tu wasiokuwa na masaada kwa taifa.
 
Huyu dada atashinda, siku zote shetani huwa hataki maendeleo ya watu naona watu bado wanaishi enzi ya dikteta.
Kwani si mlisema alifanyiwa yale kwa maagizo ya dikteta? Na baada ya dikteta kufariki maamuzi yakabatilishwa kwa amri ya mama yenu mwana democrasia?

Sasa hiki kinachoendelea ni nini?

Kuna viumbe vinaitwa MaCCM vina roho dhaifu sana .
Yaani Shangazi wa Taifa kukataa ushenzi wao, wanataka kumuonyesha roho mbaya.
Nchi ya hovyo sana hii.
Na bi, Chokochoko yupo yupo tu mara atubanie sauti. mara atulegezee macho.
Si yote hayo mlisema ameondoka nayo marehemu na sasa mnapumua?

Na bado! Mpaka siku akili ziwakae sawa
 
Yaani nyie legacy ya Mwendawazimu mnashida sana, hata iweje KICHAA kafa yaani alishakufa , kuoza na kunuka, tukaitia mpaka gundi mdomoni. TUKAFUKIA 😂
Kujipa moyo unaruhusiwa .
FUNZA tu wanatoka kwa MAVI yake..
DADEKI..!
 
Back
Top Bottom