Fathers'day -kina baba wanaowakataa watoto wao kisa nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fathers'day -kina baba wanaowakataa watoto wao kisa nini?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tausi Mzalendo, Jun 19, 2011.

 1. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwanza nawapongeza wababa wote kwa mchango wao mkubwa katika kuleta watoto duniani, kuwapenda wake zao au kuwajali mama wa watoto wao na watoto na pia kubeba majukumu yao.HONGERENI SANA KWA SIKU YA LEO.

  Hata hivyo nina maswali machache kwa wale wababa wote waliowahi au wenye mpango wa kuwakataa watoto wao:
  1.Je wangekataliwa na baba zao wangejisikiaje?

  2. Nini kinamfanya Mwanamme amkatae mtoto wake wakati anajua kabisa aliwahi "kupanda "mbegu '? Dhamira haiwasuti?

  3.Mwanamke anapokataliwa mwanaye na baba mhusika anajisikiaje?
  4. Mtoto aliyekataliwa na babaye anapokuja kutambua anajisikiaje?
  Michango yenu tafadhali
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mmh.. haya maswali magumu lakini yanagusa sehemu sehemu; kwenye swali la pili nadhani (naweka msisitizo kwenye kudhani) wapo wanaume ambao wanajua kabisa wapenzi wao hawakuwa waaminifu so kumkataa mtoto ni ishara ya kujihami kuwa nisije kushakiziwa mtoto asiye wangu - hasa wanapoangalia shows kama za Maury au Jerry Springer..!!
   
 3. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  @ MMKJJ,
  Naheshimu mawazo na mchango wako.Ukiacha huko kujihami kwa kudhania wakati kuna namna nyingi za kujua kama mtoto ni wako ama la, je wanaume wanapomwadhibu mama hawaoni adhabu kubwa anaipata mtoto ambaye hakuomba mmsababishe kuja duniani/

  . Kwamba mama hakuwa mwaminifu, sidhani kunakuja kama kishtukizo.Mwanaume unapojamiiana na mwanamke bila kinga unategemea nini?
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Namba moja siwezi kuwajibia ila mengine naweza kwasababu nimeona kwa mtu wangu wa katibu sana!!

  2. Kukwepa/kukataa na kuogopa majukumu.Kama ambavyo kuna wadada hua wanatoa mimba na kutupa vichanga kisa eti hawako tayari kulea au hawana uwezo ndivyo ilivyo kwa wanaume.Inakua rahisi kwao kusema sio wangu na hata kama ni wangu simtaki kwasababu kwa wakati huo haitamcost kitu iwapo mwanamke atasema tu “sawa bwana“.

  3. Maumivu...unyonge...mtu anahisi kuzalilika maana mara nyingi kukataliwa kwa mtoto hua inaendana na dhana ya kwamba mama hakua mtulivu...sio mjanja...hana akili na mengineyo.Hivyo maumivu yanakuwepo bila kusahau aibu mbele ya jamii.Mwanaume akimkataa mtoto kwa baadhi ya watu mama/mwanamke ndo hua anaonekana wa ajabu na sio anaekataa mwanae.

  4.Anajisikia vibaya...anamchukia baba mzazi na kumwona hana maana.Nnaemjua mimi baba yake alianza kujisogeza akiwa na miaka 15 mtoto akawa anaenda kumsalimia bibi yake ila hakujali sana kuhusu baba.Ila alivyofikisha miaka 18 baba yake alikua anauliza kwanini haendi kumsalimia mtoto akamuuliza ili iweje...akamjibu siunakuja tu kumsalimia baba yako?!Mtoto akamwambia baba yangu ni yule anaejua mpaka leo nimekula na kuvaa nini pia ninesoma wapi.Miaka 20 baba akampigia mama kumwuliza mbona humruhusu mtoto kuja kwangu mama akamwambia hayo sio maamuzi yangu bali ni yake mwenyewe...ongea nae huyu hapa.Mtoto akamwambia baba yake sitaki mahusiano na wewe nilishakwambia na ukiendelea kunifuatilia ntakuua.Hawezi kufanya kitu kama hicho ila hayo maneno yanaonyesha ni kwa kiasi gani aliumia na kitendo alichofanya baba yake.Ila anampenda sana mama yake ...hilo linanipa furaha!
   
 5. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Lizzy,
  Hapo nimependa maana lawama za wanawake kutupa watoto zipo sana na ni sawa walaumiwe.Mara nyingi "wanaume wanapotupa watoto" hawalaumiwi.Umefika wakati nao waangaliwe vingine!
   
 6. N

  Ngo JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tausi Mzalendo;
  Naheshimu mawazo na mchango wako.Ukiacha huko kujihami kwa kudhania wakati kuna namna nyingi za kujua kama mtoto ni wako ama la, je wanaume wanapomwadhibu mama hawaoni adhabu kubwa anaipata mtoto ambaye hakuomba mmsababishe kuja duniani/

  Kwamba mama hakuwa mwaminifu, sidhani kunakuja kama kishtukizo.Mwanaume unapojamiiana na mwanamke bila kinga unategemea nini?

  Maswala ya DNA kwenye ulimwengu wa tata kwani yameanza lini Tausi? Tofauti na DNA kuna njia ipi unayoweza kuthibitisha kama mtoto ni wako? Ni wakina mama wangapi wameolewa lakini wamebambika waume zao watoto wa wanaume wengine na wahusika hawajui?. Si wote wanaweza kumdu gharama za kwenda kupima DNA hasa huku bongo hivyo wahusika (wanaume wanakataa watoto) wakijuwa kuwa hawakuwa peke yao kimapenzi na mdada ndiyo maana wanakuwa wagumu kukubali mimba---mtoto kama watakuwa hawana uwakika wa kutosha. Hata kwenye hizo shows alizozitaja Mzee Mwanakijiji, sababu kubwa ya wababa kukataa watoto wao kama hawajapima DNA ni wadada kuwa na mahusiano na mtu zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Wakipima DNA na majibu yakasema watoto ni wakwao wote huwa wanakubali majukumu ya kulea watoto wao.


  Kwa hiyo, issue siyo kutotumia kinga bali mtoto ni wa nani? Ndo tatizo kubwa kwa mwanaume. Kwa wale wanaojitowa akili na watoto ni wao na DNA imethibitisha kwakweli hapo sijui sababu zaidi ya kusema ''si wanaume wote are good fathers''.
   
 7. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Lakini wengine labda wanamchukia mama mtoto na siyo mtoto..!!! so inakuwa ni sababu ya kuhalalisha tu chuki iliyoko kwa mama mtu.
   
Loading...