Fastjet ya Mwanza-Dar ime-abort take off!

Fastjet ya Mwanza-Dar ime-abort take off!

Da! hakuna usafiri na uogopa kama ndege, ktk maisha yangu ndege nimepanda mara 2 tena kwa matatizotu sivinginevyo, pole sana

unapokuwa juu karibu na mbinguni let say 25,000+ feet above see level,unamuomba Mungu akushikilie tu ufike salama.hakuna kingine zaidi ya hicho.
 
Hapo kwenye red, uwe makini na uandishi wako. Natumaini ulikuwa wataka kuandika take-off. Katika wakati ambapo rubani anatakiwa kuchukua maamuzi magumu ni kuahirisha kupaa huku tairi ya mbele imeshanyanyuka, kuahirisha kutua huku umeshakaribia gusa chini na kufanya crash landing.

well said,hata mimi nadhani alitaka kusema take-off.it is not necessary tair ya mbele iwe imeshanyanyuka but kama keshachochea(release full power for takeoff) at that speed then aka abort,bado inakuwa ni abortion katika takeoff,but you should keep in mind that every landing is a crash-i mean a controlled crash
 
Ndege ni usafiri mzuri ila ikifikia kwenye landing na final take off huwa nakuwa mwoga sana.
 
Mkuu ajali za ndege zinatokea mara ngapi Tanzania ukilinganisha na ajali za magari? ndege ni usafiri ulio salama!

Inaweza kuwa sahihi lakini uoga wa nafsi huwa haupingiki waweza ogopa hata jongoo wakati hana meno, kiukweli hakuna usafiri ninaougopa kama ndege, kiukweli niwapo ndani ya treni naelekea kgm hujisikia amani saana pia nipandapo meli hujisikia aman
 
Je hao ndege wapo salama?
Mlinde hizo ni maliasili zetu!
 
Wakuu,

Naandika hapa huku mapigo ya moyo yapo juu sana. Natokea Mwanza muda huu na flight ya saa8:25 fastjet kurudi Dar. Tumefika kwenye run-way na mbio zikaanza za kutafuta speed ya kupaa, wallahiiii ndege si wakakatiza ghafla juu na si tayari Kasuku (fastjet) yupp kibati... Aiseee zimefungwa break mpaka tumehama ndani pamoja na mikanda kufungwa.

Nashukuru tuko salama na imebidi turudi tutoke nje ya ndege. Tumerudi terminal ndege inakaguliwa

Hiyo airline ndio ya kusafiria kwani marubani wako makini na safety procedures zinazingatiwa!!
 
January mwaka huu nilienda mwanza. Nimepanda ndege mara nyingi, lakini hii sijawahi kuiona. Wakati wa kushuka ndege ilikuwa inayumbayumbs utadhani mabawa yatang'oka. Watu waliaza kutubu dhambi na wengine kusema Mungu mikononi mwako naiweka roho yangu
 
Ilikuwa imekaguliwa lakini kwakuwa imegonga ndege hai wakati inatake off,lazima ifanyiwe ukaguzi mwingine ili kuangalia km haikupata madhara makubwa iweze kuendelea na safari.

Pole sana sana ila Mpwa wangu hili jina lako hili. Nakuomba libatize tena
 
Uwanja wa ndege Mwanza kuna tatizo la (ndege hai) wengi maana hata ile ndege ya jeshi ilipata ajari kisa ndege hai kaingia kwenye injini ya ndege
Mchawi aliyetuloga watanzania alishakufa...yaani huwa hatujishughulishi na chanzo cha tatizo hadi tatizo litokee. Hapo airport Mianza kuna kundi kubwa la ng'ombe wanalishwa hapo uwanjani, nasikia ni wa meneja wa uwanja,kuna aina flani za ndege viumbe ambao upenda sana kuwa karibu na malisho ya mifugo:nyangenyange,nk pia pamoja na kuzuia kilimo cha mpunga jirani na uwanja kumbe zoezi hilo lililenga hasa kutoa nafasi ya malisho ya mifugo na sasa kuna kilimo cha mbogamboga jirani kabisa na uwanja yote hayo ni kivutio cha ndege pori kuwepo hapo muda mwingi.

Kama haitoshi uwanja huu hakuna sehemu ya kuhifadhi taka na hivyo takataka hutupwa pale inapopita barabara ya kwenda Igombe..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom