FASTJET: My first and last experience

FASTJET: My first and last experience

Tiba

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2008
Posts
4,607
Reaction score
3,187
Wana Jamvi,

Siku ya tarehe 26 April 2013, nilikutana na mkasa wa hawa jamaa zetu wa Fastjet na tangia siku hiyo nilinuia, kutokufikiria kutumia usafiri wa hii ndege tena. Kisa chenyewe kilikuwa hivi;

Nilisafiri kwa gari binafsi kutoka Dar kwenda Arusha tarehe 21 April 2013 na nilitarajia kurudi Dar Ijumaa ya tarehe 26 April 2013 kwa kutumia ndege ya Fastjet iliyokuwa iondoke Arusha (KIA) saa 3:30 usiku. Nilikuwa na tiketi mkononi. Taratibu za Fastjet ni kuripoti dakika 40 kabla ya muda wa ndege kuondoka. Nilikodisha taxi kutoka Arusha na nilifika KIA saa 2:40 usiku. Nilipofika, taxi iliyonipeleka pale iliondoka. Kufika mlangoni, walinzi wakanimbia kwamba nimechelewa na kwamba counter tayari imefungwa na hakuna mtu wa kunicheck in. Nilimkuta na Bwana mwingine aliyekuwa amenitangulia kufika na yeye akibembeleza kuruhusiwa kuingia. Wale walinzi walikataa katakata na ukweli ni kwamba pale counter hakukuwa na mtu hata mmoja. Kwa kushirkiana na msafiri mwenzangu niliyemkuta pale, tulianza jitihada za kutaka kuonana na mwakilishi wa Fastjet pale uwanjani. Jitihada zetu za kumwona mwakilishi wa Fastjet hatimae zilifanikiwa lakini to our suprise, yule Bwana alikuwa too arrogant kupita kiasi. Alitwambia hakuna msaada wowote anaoweza kutupatia. Ndege ilikuwa bado iko pale uwanjani. Wakati tukiendelea kumbembeleza, aliitwa kwenye radio call na hivyo akatutaka tutoke ofisini kwake na kwamba angekuja kutusikiliza baadae lakini akasema msaada pekee anaoweza kutupa ni kutukatia ticket nyingine kwa ajili ya ndege ya Jumamosi asubuhi tarehe 27 April 2013.

Baadae tulipata taarifa kwamba ndege haiwezi kuondoka kwa kuwa imepata hitilafu na kwamba abiria ambao tayari walikuwa wamepanda wameshushwa na kurudi waiting room. Yule mwakilishi wa Fastjet hakurudi tena ofisini pale ingawaje tuliendelea kumsubiri. Kwa kuwa nilikuwa na mkutano muhimu wa kuhudhuria Dar Jumamosi tarehe 27 April 2013, nilianza kufanya mpango wa kuangalia uwezekano wa kupata seat kwenye ndege ya Precision Air iliyokuwa iondoke Arusha (KIA) saa 1:55 asubuhi kuelekea Dar. Bahati nzuri nilimpata mwakilishi wa Precision Air pale uwanjani ambaye baada ya mawasiliano alinihakikishia kunipatia seat kwenye hiyo ndege. Tatizo sikuwa na cash ya kulipia hiyo ticket ambayo gharama yake ilikuwa Tshs. 195,000 one way. Baada ya kuhakikishiwa seat, nililazimika kukodisha taxi ya kunirudisha mjini ili kupata hela za kulipia ticket ya Precision kutoka kwenye ATM. Nilifanikiwa kupata hela na baada ya hapo kazi ya kutafuta hotel ikaanza. Nilipata Hotel na nililala karibu saa 6 usiku.

Saa 11:30 alfajiri tayari nilikuwa kwenye ofisi za Precision Air pale Arusha ili kupanda shuttle kwenda KIA. Kufika tu, nikaambiwa tayari shuttle ilikuwa imeondoka hivyo nalazimika kutumia usafiri wangu kwenda KIA (Ukweli ni kwamba shuttle ilikuwa haijaondoka na wala ilikuwa haijafika ila mlinzi anashirikiana na taxi drivers kudanganya abiria ili wakodishe taxi zao). Nilifanya hivyo na kufanikwa kufika Dar kwenye saa 3:45 asubuhi Jumamosi. Wakati turuka pale KIA, ile ndege ya Fastjet tuliiacha pale na sijui iliondoka saa ngapi. Abiria walilala pale uwanjani bila huduma yoyote hata maji ya kunywa hawakupewa.

Nia ya kuleta uzi huu ni kuwaambia wana Jamvi kwamba wakati mwingine rahisi ni ghali. Safari hii ilinigharimu pesa nyingi sana kwa kuwa tu nilitaka ticket rahisi ya Fastjet (Tshs. 107,000) one way lakini matokeo yake niliingia gharama zifuatazo;

1. Ticket ya Fastjet Tshs. 107,000
2. Taxi Arusha KIA x 3 Tshs. 150,000
3. Hotel tarehe 26/4 Tshs. 50,000
4. Ticket ya Precision Tshs. 195,000
Jumla Tshs. 502,000

Nilinuia hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kujaribu kusafiri na Fastjet na ilikuwa mara ya mwisho pia. Sitakaa nithubutu kufanya makosa tena hata kama Fastjet wata improve huduma kwa wateja na kuajiri watu wanaoweza kuwasiliana kwa heshima na wateja.

Tiba
 
Pole sana Tiba, ndo mambo ya usafiri wa anga nchi zetu za kiafrika. Utadhani ndo ilikuwa mwisho wa kufanya hiyo biashara!! Anyway, ungewasiliana na makao makuu usikie wanasemaje!!
 
Na hiyo story ya reporting time ya dk. 40 kabla ya ndege kuondoka we uliipata wapi?
 
Pole sana Tiba, ndo mambo ya usafiri wa anga nchi zetu za kiafrika. Utadhani ndo ilikuwa mwisho wa kufanya hiyo biashara!! Anyway, ungewasiliana na makao makuu usikie wanasemaje!!

RedDevil, ungejua nilivyokuwa nimekasirika usiku huo baada ya majibu ya huyo mwakilishi wao, kwa kweli hilo sikulifikiria kabisa kuongea na mtu yeyote kutoka Fastjet na hata leo hii hamu sina kabisa.

Tiba
 
pole sana kwa yaliyokukuta na gharama kubwa uliyotumia

Victor, nimekwisha poa lakini itabaki kwenye kumbukumbu zangu daima, usiku ule ulikuwa mbaya sana kwangu. Nashukuru tu kwamba nimepata kitu cha kujifunza, rahisi ni ghali.

Tiba
 
Na hiyo story ya reporting time ya dk. 40 kabla ya ndege kuondoka we uliipata wapi?

Herg, am I wrong?, ndivyo ilivyo mkuu kwa ufahamu wangu na hii si story ni utaratibu wao.

Tiba
 
Pole sana.
Lakini taabu yote ya nini, ungepanda tu Luxury Bus kutoka Arusha mpaka Dar, na ungepata faida zifuatazo:

1/Gharama Nafuu(Nauli Haidizi Tsh 30,000/=)

2/Ungepata wasaa wa kufanya utalii wa ndani.

3/Hakuna gharama za ziada zilizojificha(eg.Taxi, VAT, Lugagge Charge nk)
 
Wapuuzi sana hawa Fastjet

Kumbe ilikuwa tusafiri pamoja siku hiyo, hzi pen names za JF balaa.....

Nilikuwa na malalmiko na hawa Fasjet nikaandika mail kwenda kwa customer care wao

customer.tanzania@fastjet.com,

sales.tanzania@fastjet.com

Nikajipinda kuandika kiingereza hadi leo sijajibiwa.

Pole TB

Mkuu Masanilo,

Pole sana kumbe tungeweza kuwa kwenye flight moja siku hiyo. Hebu niambie hiyo ndege iliondoka saa ngapi kesho yake? Au na wewe uliamua kuwakimbia? Usitarajie wakujibu hata siku moja, hiyo imetoka.

Tiba
 
Victor, nimekwisha poa lakini itabaki kwenye kumbukumbu zangu daima, usiku ule ulikuwa mbaya sana kwangu. Nashukuru tu kwamba nimepata kitu cha kujifunza, rahisi ni ghali.

Tiba
Mkuu issue sio gharama bali ni ubabaishaji wa huduma za usafiri hapa Tanzania.
Usumbufu wa usafiri wa ndege upo pia Precision Air, tena upo sana tu.
Let be fair.
 
Sasa ulipofika precision kama muda ulikuwa umewahi why umuulize mlinzi badala ya kuingia ndani ofisini kwao au kuzunguka nyuma zinapopack shuttle zao?jamani mjifunze kuuliza kwa right person mkifika Ulaya mtazubaa mabarabarani sio kila unayemkuta ni muelekezaji
 
Pole sana kwa matukio na samahani kwa nitakayoyasema.

Nilishaona kwa macho yangu, desk check ya Turkish Air ikiwa imefungwa saa moja kabla. Ila alikuwepo Mbabe mmoja akapiga simu kwa mama mmoja ndani na wakafungua ingawa wafanyakazi wa Turkish Air walishasema kuwa hadi kesho.
Naona nyie mlikosa mtu kama huyo.

Ila nashindwa kuelewa kitu kimoja, ninavyofahamu mie ni kuwa kwa sasa kwa sheria za ulinzi zilivyo uwanja wa ndege, unatakiwa ufike masaa mawili kabla yaani dakika 120 kabla. Sasa wewe nani alikuambia unafika dakika 40 kabla? Dakika 40 kabla ni kuwa ndiyo mnajiandaa kwenda kuingia kwenye ndege tayari na si kwamba ndiyo unafanya Check-In.
Naona ukaja tena kuchelewa hata Bus la kwenda KIA. Yaani hata Bus likakuacha jamani? Nalo sijui utasingizia nini?

Pole sana kwa tukio ila kumbuka kuwa uwanja wa ndege unatakiwa kufika saa MBILI kabla popote pale duniani labda kama umesha Check-In online na huna mzigo, yaani unafika tu na kuingia ndani kusubiri kupanda ndege.
 
Pole sana.
Lakini taabu yote ya nini, ungepanda tu Luxury Bus kutoka Arusha mpaka Dar, na ungepata faida zifuatazo:

1/Gharama Nafuu(Nauli Haidizi Tsh 30,000/=)

2/Ungepata wasaa wa kufanya utalii wa ndani.

3/Hakuna gharama za ziada zilizojificha(eg.Taxi, VAT, Lugagge Charge nk)

Mkuu Asante kwa ushauri, lakini kumbuka walioweka usafiri wa ndege sio wajinga kivile, kuna mazingira inafaa kusafiri kwa gari na mazingira mengine yana dictate matumizi ya usafiri mbadala. On this particular case, ilikuwa ni muhimu kusafiri kwa ndege kurudi Dar ili kupambana na muda!!!!

Tiba
 
Back
Top Bottom