Fastjet kupunguza wafanyakazi

Fastjet kupunguza wafanyakazi

Wanajua bombedier inakuja kwa hiyo biashara hakuna.
Ni sawa na ujio wa bajaji kwa teksi na daladala kwenye usafirishaji.
 
Flight nyingi Walikuwa wanaenda mswaki,na nimesikia wanabadilisha aina ya ndege,wanaondoa Airbus mbili,wanaacha moja ambayo itatumika kwa safari za nje,na wataleta E190 kwa safari za ndani...
 
Nauli za Fastjet ni Cheap? nani kasema? Nimemkatia Wife DAR-MBEYA-DAR miezi miwili kabla 457,000/=
 
Nawaonea huruma hasa wale wadada na wakaka wa cabin crew. Redundancy isikie tu kwingine , usiombee ikukute, especially kama ulikuwa ujajipanga.
 
Wapate hizo hela za redundancy waje wawekeze kwenye vibiashara mtaani japo kisaikolojia itawaathiri mana hawajazoea,kuna kampuni nyingine zinawapunguza wafanyakazi kimyakimya mana mambo si mazuri


Fao la kujitoa lina utata mkuu
 
jumamos iliyopita nilienda mwanza.. return ticket ilikuwa 762,000.. hapo huwez sema cheap. sema nilikuwa nawah mazishi ilikuwa lazima nisafiri...

na baada ya kuingia kwenye ndege siti zaidi ya nusu zilikuwa tupu bila abiria...

nikajua tu game la maisha limekuwa ngumu kwetu wengi... usafiri wa ndege ni anasa sasa
 
Hivi zile ndege za Air Tanzania lini zinafika? na zile fly over vipi nazo.
 
Fastjet si nafuu hata kidogo, ukizingatia ukipata emergence nauli imepotea bora PW wana system zinazoeleweka. Wafunge biashara tu hao Fastjet.
 
Back
Top Bottom