Fastjet kupunguza wafanyakazi

Fastjet kupunguza wafanyakazi

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,981
WhatsApp Image 2016-09-10 at 12.44.38 PM.jpeg
WhatsApp Image 2016-09-10 at 12.44.36 PM.jpeg


Kampuni binafsi ya usafiri wa anga, Fast Jet imeamua kupunguza wafanyakazi ili kwenda sambamba na gharama za uendeshaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Fast Jet, John Corse ametoa taarifa kwa gazeti la The Citizen inayoeleza kuwa watapunguza wafanyakazi kutokana na mabadiliko ya kimuundo na uendeshaji.

“Wateja wamepungua, hawapandi ndege sasa. Hivyo ili kampuni ipate faida, ni lazima ipunguze baadhi ya wafanyakazi ili kuendana na gharama za uendeshaji,” anasema Corse kwenye taarifa hiyo.

Alipoulizwa kama sababu ya kupunguza wafanyakazi inaweza kuwa inatokana na mikakati ya kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Corse amejibu: “Si kwa sababu ATCL inafufuliwa bali ni changamoto za kibiashara.”

Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alitangaza kuwa ndege mbili ambazo Serikali iliahidi kuzinunua zitafika nchini kati ya Septemba 19 na 25.


Chanzo: Mwananchi
 
Hii ni hatari lakini ilikuwa inakuja. Ni muda mrefu sasa Fastjet ilikuwa inatoa warning kwamba hali yake ya kifedha ilikuwa mbaya.

Kilichoisaidia ilikuwa imesajiliwa London stock exchange kwenye mifuko mikubwa lakini investors sasa wamechoka share price kupungua kila mwaka.
 
Sasa hao walipunguzwa watarud mitaan watapaweza huku kilimo hakina manufaa tena bustani za mboga mboga hazna faida wakat gharama za madawa zipo juu haya wao wamezoea angani huku ardhini nipagum jaman wahurumien tu
 
Wapate hizo hela za redundancy waje wawekeze kwenye vibiashara mtaani japo kisaikolojia itawaathiri mana hawajazoea,kuna kampuni nyingine zinawapunguza wafanyakazi kimyakimya mana mambo si mazuri
 
I saw this coming. Flight nyingi wanajaza below half. Hii ni matokeo ya sera za Ngosha. Uchumi umedorora kwa mtu mmoja mmoja na taasisi kwa ujumla. Bahati mbata watz tunasahau haraka.
 
Wapate hizo hela za redundancy waje wawekeze kwenye vibiashara mtaani japo kisaikolojia itawaathiri mana hawajazoea,kuna kampuni nyingine zinawapunguza wafanyakazi kimyakimya mana mambo si mazuri
hali tete mkuu, wanaweza pata hela ya redundancy lakini ile ya pension nssf, pspf watusamehe mpaka wafike 55 yrs. dah ukilala nchale ukianka nchale.
 
Lazima tuishi kama mashetani, ahadi hii pekee ndio inayotimia kila kukicha, ile ya viwanda imebaki kwenye majukwaa tu.
 
I saw this coming after flying with Fastest 3times in the last 30 days. Everyone will be affected by fiscal policy of the current regime.
Lazima tuishi kama mashetani, ahadi hii pekee ndio inayotimia kila kukicha, ile ya viwanda imebaki kwenye maj haya mamboukwaa tu.
Aliyetoa hii kauli atakuwa anafurahia haya majanga yanayowapata watanzania wenzetu
 
na fao la kujito halipo, kweli tutaishi kama shetani
 
Back
Top Bottom