mfupa aliyo ushindwa fastjet ATCL itauweza?kampuni binafsi ya usafiri wa anga, Fast Jet imeamua kupunguza wafanyakazi ili kwenda sambamba na gharama za uendeshaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Fast Jet, John Corse
ametoa taarifa kwa gazeti la The Citizen inayoeleza kuwa watapunguza wafanyakazi kutokana na mabadiliko ya kimuundo na uendeshaji.
“Wateja wamepungua, hawapandi ndege sasa. Hivyo ili kampuni ipate faida, ni lazima ipunguze baadhi ya wafanyakazi ili kuendana na gharama za uendeshaji,” anasema Corse kwenye taarifa hiyo.
Alipoulizwa kama sababu ya kupunguza wafanyakazi inaweza kuwa inatokana na mikakati ya kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Corse amejibu: “Si kwa sababu ATCL inafufuliwa bali ni changamoto za kibiashara.”
Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alitangaza kuwa ndege mbili ambazo Serikali iliahidi kuzinunua zitafika nchini kati ya Septemba 19 na 25.
Chanzo:Mwananchi
wametuibia vya kutosha
Blaza unafosi mitazamo yako ndio iwe ya umma... Sounds like propaganda kwa sana!
from jborg to dsm begi lilipotea week mbili ndo likaja kupatikana wamechukua huko vitu kibao hadi underwearUmeibiwa nini?
Umejuaje kama kafosi..kuna ubaya gani akitoa mtazamo wake?Blaza unafosi mitazamo yako ndio iwe ya umma... Sounds like propaganda kwa sana!
Wameiba nini hasa?wametuibia vya kutosha
Siasa na reality ni vitu viwili tofauti kabisa na ndio maana kila siku mnaumbuka.Blaza unafosi mitazamo yako ndio iwe ya umma... Sounds like propaganda kwa sana!
Kwenye kila mada yake lazima aweke link za mada zake za nyuma, huko ni kulazimisha ugwiji wa JF kama jamaa mmoja hivi...Umejuaje kama kafosi..kuna ubaya gani akitoa mtazamo wake?
Ni kweli na ni kwasababu kuna watu huwa ni wabishi sana hivyo yanapotimia huwa ni budi tuwakumbueshe na kuwaonya waache ubishi.Kwenye kila mada yake lazima aweke link za mada zake za nyuma, huko ni kulazimisha ugwiji wa JF kama jamaa mmoja hivi...
Lakini na wewe ni mpenda umaarufu mwepesi. Vipi tabiri zenu za duru za kisiasa zikienda fyongo, huwa mnafufua thread pia?Ni kweli na ni kwasababu kuna watu huwa ni wabishi sana hivyo yanapotimia huwa ni budi tuwakumbueshe na kuwaonya waache ubishi.