Fastjet flight delay at Mwanza

Jumatano nilikua na route ya saa saba mchana Dar to KIA. nimefika airport nimemaliza scanning mlango wa kwanza napoenda kwenye check in naambia wameconcel safari mpaka kesho. Hakuna siku niliyochukia kama siku hiyo
 
Unadhani 'Mapanga Shaa' atakuwa na bei fare kama za Fastjet?
 
Walikuwa na route nne kwa siku saa 12 alfajiri,saa 4 asubuhi mchana na usiku

Wametusaidia sana ingawa kulikuwa na matatizo ya hapa na pale. Siwezi kuwabeza. Mwaka wa tano nasafiri nao kwa bei poa.
 
Kila napotaka kusafiri nao nakuta bei juu poa tu ipo siku ndoto yangu itatimia
 
Acha kubeza, FJ imekuwa msaada mkubwa sana kwa wasafiri hapa nchini, bila shaka hata wewe ndio ndege yako ya kwanza kupanda..
Ni kweli kabisa ila sasa kuahirisha/kufuta safari kumeongezeka!!!
 
Ilitarajiwa kuondoka saa4:30pm imeahirishwa na inasemekana imeondoka at 2pm????
 
Hii kampuni nayo itakuwa kufani.... Ngoja vibajaji vya JPM vianze kazi..... Itakuwa ndo mwisho!!!
Nani apande ndege ya kwenda mwanza kwa masaa matatu wakati fastjet ni saa moja tu?
 

Yaani hiyo mitumba yao na nauli zisizoeleweka zitakuwa historia. Rais JPM hongera. Tuko na wewe kwa hali na mali! Mwenyezi Mungu akutangulie katika kila ufanyalo kwa manufaa ya watu wako.
 
Atc wakitaka wafanikiwe wanatakiwa kufanya kama mashirika mengine ya ndegw yanavyofanya, kuwa na wing ya ndege za bei rahisi ambazo hizo zitashindana na watu kama fastjet
 

Hahahaaa balaa nusura hatari...
 
Ilitarajiwa kuondoka saa4:30pm imeahirishwa na inasemekana imeondoka at 2pm????

Hehehehehee habari kaiandika kiswahili halafu muda kauripoti kiingereza hata mie nimejiuliza weeh mwisho nikaamua kuacha. Itakuwa njaa ilimzidia ukijumlisha na hasira lazima achapie hehehhe
 
FastJet wako kwenye mchakato wa kuacha kutumia zile Airbus zao na kuhamia kwenye ndege ndogo za Embraer. Hadi sasa wameshaacha kutumia baadhi ya zile Airbus kwahiyo kuna upungufu mkubwa wa ndege kwente fleet yao. Katika siku hizi kabla hawajaanza kurusha Embraer tegemeeni usumbufu mwingi tu katika safari zao....ndege hazitoshi kuhudumia route zao
 
Wakati mmoja nikiwa Jomo Kenyatta Airport nasubiri KQ ya Entebbe nikawa naangalia board za taarifa za ndege mbali mbali zinazotarajiwa kutua na kuruka kutoka kiwanjani hapo. List ilikuwa ndefu. Ni route moja tu ya Nairobi - Dar ya FastJet iliyokuwa na cancellation! Nikajiwazia TZ yetu!!!??
 

Hayo masaa uliyoandika ni sawa kweli? Ndege iliondoka 2pm badala ya 4.30pm?
 
Kwahiyo huu uzi wanao changia ni wenye hadhi ya kuchenga mawimbi kwa mkuyati wa chuma eeehh..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…